Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Dr habari za asubuhi
ninauvimbe chini ya kidevu kati ya kidevu na koromeo leo ni siku ya tatu.
Sina kidonda sehemu yoyote na kichwa kinauma kiasi
nilitembelea mkoa wenye baridi sijui ndo sababu ,,,au ninyama ya mbuzi niliyokula??
Naomba msaada wako tafadhalii
 
Doctor nasumbuliwa na chunusi ndogo ndogo nimetumia Epidermal ,persol tube lakini zimedunda msaada plz?
doctor nasumbuliwa na tatizo la kufanya sna mapenzi kila saa nawaza mapenzi tu mimi ni wa kiume...
 
Doctor mm ni mjamzito wa miez minne na wiki mbili tatizo langu ni moja tuu ninatema sana mate je kuna njia mbadala yoyote inayoweza nisaidia nikaacha hili tatizo ujauzito wangu wa kwanza ulikuwa hiv hiv nilitema mpk siku niliyoenda kujifungua,nifanye nini ili hii hali ikate imenichosha sana
 
Dr kwanza nakupa hongera kwa moyo wako huo wa kujitolea..,Baada ya pongezi hzo naomba unisaidie tatizo langu, nina binti yangu wa kazi anawashwa kwenye vidole na pia ngozi inababuka, baada ya check up hospital wakasema ni fungus, akapewa dawa ya kupaka, akachomwa sindano ya power safe na vidonge vya Fluconazole kwa siku 7, baada ya kutumia hali ikapungua kdogo then ikarejea, nlipompeleka tena akapewa canditra vidonge kwa siku 7, amemaliza leo anasema ameanza kuwashwa, je nimpatie dawa gan tena??

Asante kwa pongezi lako mkuu. Tupo hapa kwaajili ya jamii na mimi naamini kwamba kuelimisha jamii ndiyo chanzo na njia pekee yakuboresha Afya ya wanannchi.

Naona binti huyo kapewa dawa nyingi sana. Ushauri wangu ni achukue dawa hizi. Alafu nipe mrejesho:

1. Hydrocortisone Cream
2. Terbinafine Cream
Hizi cream mbili utazichanganya na kuipakaa kutwa mara mbili kwa muda wa siku 14.
3. Cetirizine Tabs - Kidonge kimoja kila siku Usiku kwa muda wa siku 14.
4. Terbinafine Tabs - Kidonge kimoja kila siku Usiku kwa muda wa siku 14.

Asante.
 
Asante kwa pongezo.

Mkuu inaweza kuwa unayo Peripheral neuropathy. Naomba utumie dawa hii ni vitamin maalum kwaajili yakusaidia:

Neuroton kidonge kimoja kila siku kwa miezi moja. Asante.
 
Dr Mimi kuna siku nilikuwa nasafisha sikio la kulia na kijiti baadae nikahisi nguvu ya usikivu kwa hili sikio imepungua sana sana sana naona sikio la kushoto ndio linasikia vizuri je kuna uwezekano kuwa nilipasua ngoma ya sikio?

Uwezekano wa hilo lipo mkuu. Ushauri wangu ni uende kwa daktari wa sikio (ENT) na umueleze akufanyie vipimo. Asante.
 

Mkuu, pole sana na shida hilo. Ningekushauri umuone daktari bingwa wa fupa (Orthopedic Doctor) ili afanye vipimo vya
X-ray tena na akupe ushauri. Kwa sasa hivi kuondoa maumivu na kuongeza nguvu unaweza kutumia dawa hizi:

1. Glucosamine + Chondriotin Tablets - Kidonge kimoja kila siku kwa miezi moja.
2. Ketoprofen Gel - Utapakaa kwenye mgongo inapouma kutwa mara mbili.

Asante.
 
Dr pole na majukum ya kila ck
Dr shida yangu kubwa ni mwenza wangu wakat Wa period
Anakuwa na kizungu zungu
Mgongo unamuuma sana
Anaishiwa nguvu na
Miguu kukauka
Msaada wako dr nini tatizo gan hilo na nini tiba yake
Asante
mtr96

Mkuu, inaweza kuwa maumivu ya periods ya kawaida AU Ovarian Cyst AU Endometriosis.
Nakushauri umuone daktari bingwa wa wanawake (Gynecologist) ili ampime na akupe ushauri bora.
Asante.
 

Mkuu, niambie unavyoendelea baada ya siku 3. Je uvimbe unaongezeka? Je kichwa inaendelea kuuma? Je una homa?
 

Ushauri wangu ni umuone daktari bingwa wa wanawake. Asante.
 
Nini dawa ya kupunguza uzito mbali na kufanya Mazoezi? Tiba mbadala na tiba za kizungu

Ukweli ni huu: Kupunguza uzito ni vizuri ufanye mazoezi na kula chakula bora. Kupunguza vitu vyenye sukari na mafuta mengi. Na kula kwa kiasi. Lakini kwa wale wagonjwa waliofika uzito mkubwa sana sana kuna upasuaji unaweza kufanyika.
 
Mkuu natanguliza shukrani zangu za dhati..,
Ntafanya hvyo na nitarejea kwa mrejesho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…