Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Habari Daktari. Mimi nina tatizo la kukohoa mara kwa mara hususan koo huwa linakereketa sana. Nimetumia dawa nyingi bila afueni. Naomba msaada wako.

Mkuu, Sasa hivi ni muda wa allergy na ndiyo maana unapata tatizo hilo. Kabla sijakuandikia dawa, ningependa kujua umetumia dawa gani mpaka sasa?
 

Mkuu yaonyesha inaweza kuwa maji iliyopo kwenye kiungu ndani ya masikio ina tatizo au haipo sawa. Ningekushauri umuone daktari bingwa wa masikio, pua na koo (ENT Specialist). Wanapatikana Muhimbili pamoja na SANITAS Hospital.
 
ila tatizo langu nataka nipige bao mbili na kuendelea, ila nkishapiga moja tu sipatagi tena jingine zaiidi ni kumsababishia maumivu mwezangu kwa mda mrefu ninaocheza game bila kumwaga la pili,

1. Unakunywa maji ya idadi gani kwa siku?
2. Unapata maumivu au tatizo lolote wakati yakukojoa?
3. Unangoja muda gani baada ya bao la kwanza na kabla ya pili?
 
nashukuru kwa moyo wako wa kujitolea kutusaidia angalau kujua matatizo yetu na baadae kupata matibabu sahihi.
Mimi nina mfanyakazi wangu ana matatizo mawili
i)anapenda sana kutafuna mifuniko ya chupa za maji,soda kila wakati
2) analalamika sana kuumwa miguu wakati amekaa,hivyo mara nyingi anapenda miguu kukaa imenyooshwa juu ya kiti au kulala.hali hii ameishi nayo zaidi ya miaka 3
huyu ni jinsia ya kike umri wa miaka 29


Mkuu, Ningependa kupewa taarifa zaidi kidogo:
1. Je meno yake inamuasha au kuumpa maumivu yeyote?
2. Je anayo maumivu kwenye ufizi wa mdomo?
3. Je miguu yake imevimba?
4. Je anapata tatizo la ganzi kwenye miguu?
 
Heshima kwenu wadau,
Nina mtoto wangu wa kiume miaka 7,anasumbuliwa named tatizo la kuumwa na kitovu,Mara Kwa Mara.
Je Tiba yake ni nini?
Cc:MziziMkavu etc
Asanteni!

Mkuu, tatizo hilo ni vizuri ukamuone daktari bingwa wa watoto. Kuna Daktari moja anaitwa Dr. Rafia pale SANITAS Hospital. Anaweza kukusaidia pamoja na kupa ushauri mzuri zaidi.
 

Mkuu inabidi uje hospitali.
 
Je matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume (kama uuume kulegea, ...) yanatibiwa hosptalini???
Kuna wimbi kubwa la watu wasio na utaalamu wa tiba ila wanajinadi kutoa dawa.

Mkuu, Asante kwa swali zuri. Hakuna dawa za asili zinazosaidia kwenye hilo. Mara nyingi watu wanaouza hizi dawa wanachukuwa dawa kutoka pharmacy alafu wanachanganya na majani tu.

Kwaajili yakusaidia nguvu za kiume, Ndiyo kuna dawa inaitwa Sildenafil. Ukimeza kidonge moja saa moja kabla ya kitendo tatizo la kulegea haitakuwepo.
 
Mimi naomba kufahamishwa unaweza kutumia dawa gani ili kuzibua mirija ya uzazi iliyoziba shukran

Zipo dawa kama duphastone na zinginevyo za homoni ya wanawake. Lakini tatizo kama hilo na dawa kama hizo zinatolewa kwa ubora na madaktari bingwa wa wanawake (Gynecologist). Baada hawa madaktari bingwa wa wanawake washakupima wanaweza kukushauri dawa gani ni nzuri zaidi.
 
Nakohoa,hasa nyakat za jioni na asubuh,siumwi na chochote kingine,pia nikipigwa sana na upepo pia nakohoa zaidi hasa mida hiyo hyo

Yaonyesha una allergy.

Tafadhali chukua dawa hizi kama bado unayo tatizo hilo:

1. Ebastan 5mg, Kidonge kimoja kila siku asubuhi kwa muda wa wiki tatu.
2. Montelukast 5mg, Kidonge kimoja kila siku asubuhi kwa muda wa wiki tatu.
3. Pharmacoff Syrup, kunywa 10ml kutwa mara mbili kwa muda wa wiki mbili.

Asante.
 
Mtu akitaka kukuona mnapatikana wapi
 

Mkuu atumie dawa hizi alafu nipe mrejesho:

1. Omeflex Tablets; Kidonge kimoja asubuhi na moja jioni kila siku kwa muda wa miezi moja.
2. Neurobione Forte Tablets; Kidonge kimoja kila siku usiku kwa muda wa miezi moja.
 
Heshima yako mkuu ... Tatizo langu ni kunawakati mkono au mguu unakufa ganzi baada ya muda unaachia unakuwa sawa.linaweza kuwa tatizo?
 
naombeni msaad Wa dawa ya macho chanzo ni matumizi ya simi ,TV na kompyuta macho yanauma saana

Mkuu Ushauri wangu ni yafuatayo:

1. Punguza utimiaje wa simu, tv na kompyuta.
2. Punguza mwanga (brightness) unapotumia hizi vitu, haswa wakati wa usiku.
3. Tumia Saline Eye Drops. Weka Drop Mbili kila jicho usiku unapolala kutwa mara tatu kwa wiki kwa muda wa wiki mbili.
 
Mkuu atumie dawa hizi alafu nipe mrejesho:

1. Omeflex Tablets; Kidonge kimoja asubuhi na moja jioni kila siku kwa muda wa miezi moja.
2. Neurobione Forte Tablets; Kidonge kimoja kila siku usiku kwa muda wa miezi moja.
Nakushukuru Dr ngoja nivitafute.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…