Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

dr naomba kuelekezwa namna ya kufanya kygel exercise kwa mwanaume
 
Shukran jazilah!! ndugu daktari kwa kutusaidia ndugu zako kutokana na matatizo mbalimbali ya kiafya.
Mimi napenda kuuliza; hizi siku za karibuni nimepatwa na mabadiliko ya upigaji wa mapigo ya moyo!! Hayapigi kwa ile hali ya kawaida yamekuwa chini kidogo, ikiambatana na uchovu wa mwili, kutoweza kusimama kwa muda mrefu, kichefuchefu!! na kwenda haja ndogo mara kwa mara. Je ni nini sababu ya hali hii?
 
Asante Doctor.Mimi napenda kuuliza tatizo la kutoa makohozi kooni na mishipa ya shingo kuuma baadhi ya muda husababishwa na nini hasa? Tatizo hili halisababishi maumivu yoyote wakati wa kula chakula.
 
Dalili zako zinaonyesha una migraine. Je ulitumia dawa lolote lakupunguza maumivu ya kichwa?
Nilitumia paracetam na hedex lakin hazikutuliza maumivu, naona ugonjwa wenyew ni reccurent,, nimeambiwa nikapime macho kwa sababu nikiangalia naona vispots vidogo vidogo, huo ugonjwa wa migraine unatibika? Dalili za kuumwa macho pia si kuumwa kichwa?
 
U.T.I ni infection ya mirija ya mkojo. kama daktari alikupima na kweli unayo tatizo hilo, Basi nitakushauri hivi:
  1. Dawa Amoxiclav 500mg kutwa mara mbili kwa siku 7. (Hii dawa unaua vimelea na kuondoa maambukizi)
  2. Dawa Cital (Hii dawa itakusaidia kuondoa maumivu kwenye mirija ya kukojoa)
  3. Kunywa maji mengi kama lita 3 au 4 kila siku (unapokunywa maji unapunguza idadi ya vimelea)
Asante
Doctor samahani naomba kufahamu dawa nzuri kwa ajili ya maumivu ya tumbo na kiuno wakati wa hedhi kwa sababu nasumbuliwa na maumivu haya na ni makali sana kiasi cha kushindwa hata kutembea na muda mwingine huwa natapika sana hadi kuzimia. Nimetumia diclopar lakini nasikia sio nzuri kiafya. Je nifanyeje?
 
Mimi dr. Nimefurahi sana kupata nafasi ya kuuliza swali. NINA UGONJWA WA TINNITUS(Ear ringing/bunzing) Yani Nina mngurumo usiokwisha Kama Mlio wa friji katika sikio langu la kushoto , ambao nausikia kama unatokea kichwani ,kwa muda wa mwezi mmoja sasa. Naomba unipe maelezo kuwa unasababishwa na nini pamoja na Tiba yake.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Dokta nina tatizo la kutokwa na damu puani hasa kipindi cha joto. Tangia utotoni mpaka saiv. Sijui ni tatizo gani hilo
 
Kwanza pole na kazi dr mimi nasumbuliwa na tatizo la UTI niseme ni sugu mana nlienda kupima nkaadikiwa dawa mara ya kwanza nlichoma powerself tano bado nkawa naskia maumivu ya korodani moja ya kulia mpk sehem ya juu ya tumbo km eneo la kitovuni kwa pembeni upande wa kulia nkaenda tena kupima kwa utrasound nkaambiwa nimevimba korodani ndio sabb napata maumivu haya sasa nkaandikiwa dawa hizi doxyacyline 100mg bd 7/7,Metronidazole 400mg fid 7/7,Ciproflaxin500mg bd7/7,Brusfan 5/7 sasa nasikia maumivu tena upande uleule sehemu ya juu tumbo na korodani nashindwa kujua je nitumie dawa gani?
 
Dr nina tatizo la kuwashwa baada kutoka kuoga hasa nyakati za mchana au jioni. Nikioga asubuhi sana kuwashwa kunakuwa hakupo. Je tatizo ni nini hasa? Dawa ni nini? Kuwashwa huku hutokea sehemu mbali mbali mwilini kama miguuni, kwenye mapaja, mikono, mgongoni na tumboni. Na hudumu kwa dakika 3 mpaka kumi.
 
dokta samahani mm nasumbuliwa na tatizo la kulegea mishipa ya uume, mpaka inapelekea uume kutosimama vzur wakat Wa tendo la ndoa,, naomba ushauri Wa dawa gani nitumie ambayo haitaleta madhara huko mbeleni, na naweza kuipata wapi?
 
Huu ni ugonjwa gani?

Unapolala na mwenzi wako mnasex baada ya muda mfupi unasikia maumivu makali kwenye njia ya mkojo na kuanza kuona usaha, maana najua kama ni gono ukimaliza kusex utakaa muda ata siku moja kuona dalili..
 
mkuu nilikuwa naomba unielezee huu ugonjwa unaitwa MWEZI MCHANGA hivi hauna tiba ya kudumu kwel?na kwanini mtu anachanganyikiwa periodically and alternatively
 
U.T.I ni infection ya mirija ya mkojo. kama daktari alikupima na kweli unayo tatizo hilo, Basi nitakushauri hivi:
  1. Dawa Amoxiclav 500mg kutwa mara mbili kwa siku 7. (Hii dawa unaua vimelea na kuondoa maambukizi)
  2. Dawa Cital (Hii dawa itakusaidia kuondoa maumivu kwenye mirija ya kukojoa)
  3. Kunywa maji mengi kama lita 3 au 4 kila siku (unapokunywa maji unapunguza idadi ya vimelea)
Asante
Mkuu dawa hii Augmentin vipi uwezo wake?
 
Back
Top Bottom