Dr, nina maswali mawili.
La 1: Nini chanzo cha nyayo za miguu kuhisi zina moto pidi unapokuwa umevaa viatu na ipi tiba yake?
La 2: Chanzo cha ugonjwa wa bawasiri( kuota uvimbe/vidonda kwenye njia ya haja kubwa na dawa yake ni ipi?
Asante.
kuhusu swali la kwanza
Viatu huwa unavaa kwa muda gani na ni aina gani ya viatu ambavyo huwa unavaaa?. Kwa maana kuna baadhi ya watu wakivaa viatu au aina Fulani ya viatu huwa inawapelekea nyayo au mguu kuuma.
Pia kuna ugonjwa Wa "miguu kuwaka moto"
Kuhusu swali la pili
Chanzo cha bawasili
Kuna sababu mbalimbali zinazopelekea MTU kupatwa na bawasili kama:
Kukaa chooni kwa muda mrefu ukiwa na lengo la kujisadia haja kubwa lakini pasipo kutoa hiyo haja au kutoa kidogo.
Vyakula vya kisasa tunavyo vitumia mfano nafaka zilizokobolewa na viwandani
Kutopata mlo kamili
Kukaa mda mrefu bila kwenda haja kubwa
Kufanya mapenzi kupitia haja kubwa (anal sex)
Kukaa mda mrefu bila kula chakula N.k
TIBA
Kunywa maji kwa wing I
Kula mlo kamili
Jiwekee mazoea ya kutokaa mda mrefu chooni pasipo haja
Kula chakula kwa wakati
Ulaji Wa matunda Mara kwa Mara
Kula vyakula vya asili visivyokobolewa mfano dona
NB: pia kuna aina za bawasili yaani
Inayoota kwa ndani na kuigundua siyo rahisi
Na inayoota inatokeza mpaka nje ya haja kubwa ambayo wakati Wa kujisaidia inaonekana
Na nyingine mda wote inakuwa nje
Jitahidi ufanyiwe checkups