theriogenology
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 8,748
- 15,681
- Thread starter
-
- #461
Wapo mkuu ila bei yake imechangamka kidogo kama kweli unataka pure breed.Mkuu kama uko Dar naomba unielekeze jinsi ya kupata pupy 2 jike na dume wa mbwa aina hii. Mimi nipo tabata kimanga.View attachment 1466787
Ulzia kuna mbuz wanaitwa buha hio breed inapatikan sana maeneo ya kigoma wanauwezo wa kuzaa mpk mapacha watatu wanaweza kukusaidia kweny biashara yakoDr kwema vp nawezaje kupata mbegu ya mbuzi wale wanaozaa mapacha na je inawezekana nikawapandikiza mbuz hawa wa kawaida wakazaa mapacha?
Wengine wapo chato kwa wasubiDr kwema vp nawezaje kupata mbegu ya mbuzi wale wanaozaa mapacha na je inawezekana nikawapandikiza mbuz hawa wa kawaida wakazaa mapacha?
Shukrani Dr. Kwa maelekezo mazuri sana. Hizi Infra red light bulbs naweza pata kwenye Agrovet stores, ama ni kwenye maduka ya vifaa vya umeme?Mkuu vifaranga unaweza kuvilea kwa kutumia;
1. Charcoal brooder ( vyungu maalamu vinavyotumia mkaa )
- Kwa kawaida vinaweza chungu kimoja kinaweza kulea vifaranga mia moja, faida yake unatumia rasimali mkaa ambao ni rahisi kupatikana.
- Hasara yake ni kuwa itakulazimu kila baada ya masaa 2-3 kwenda kuongeza mkaa na pia hakikisha madirisha yako huyafungi yote kuruhusu hewa safi kuingia ili kuondoa hewa chafu ya carbonmonoxide inayozalishwa na mikaa.
2. Infared light bulb (balbu maalumu za umeme)
- Hizi huwa zinakuja na rangi nyekundu na ni malaamu kwa ajili ya kulelea vifaranga, taa moja ina uwezo wa kulea vifaranga 200.
- Faida yake ni kwamba inatoa joto stahiki kwa vifaranga, na pia haizalishi hewa chafu kama mkaa kwa hiyo ukiwasha huna haja ya kuamka usiku kwenda kukagua vifaranga.
- Hasara yake ni kuwa inatumia umeme mwingi kiasi na bei yake ni 50000 kwa taa moja.
3. Gas brooder ( Bruda ya gesi )
- Hii ni maalamu kwa ajili ya kulea vifaranga kwa kutumia gesi hivyo ni ghali kiasi na bruda moja ina uwezo wa kulea vifaranga zaidi ya 1000 na pia ni nzuri una uhakika wa kuvuna vifaranga vyako vyote kwa sababu haitoa hewa chafu.
NB: Hapo sasa ni wewe kuangalia mfuko wako unasemaje mkuu.
Mkuu hicho cheti msaidizi ni cha lazima ili ufungue hyo buashara na je kinapatikanaje pia hyo VTC ni cheti kinachopatikanaje?
Habari Mkuu, pole kwa kuuguliwa na mfugo wako ningependa kujua ulitumia njia gani kupima na kujua huyo ng'ombe yuko na Anaplasmosis ( Ndigana baridi) na Ulihakikisha vipi kuwa ng'ombe wako alipona ECF ( ndigana kali) na pia inaweza kuwa babesios.
Najua watu wengi huwa wanachanganya hayo magonjwa wakati wa kufanya diagnosis unaweza kuta unatibu anaplasmosis kumbe mfugo wako ana ECF..
Ndio maana dalili ni muhimu sana wakati wa kufanya diagnosis na dalili ukiwa expect mzuri unaweza kuwa correct kwa 60 % ila vipimo vya maabara ni 100%
Hivyo basi kama uko na uhakika ni anaplsmosis kweli jaribu kubadili dawa na tumia dawa hizo hapo chini;
View attachment 1105279
Hiki kifaa unaweza kukipata kwenye duka la kuuzia dawa na bidhaa nyingine za mifugo. Bei yake ni kati ya Tsh 50,000 hadi 80,000 kutegemeana na mahali ulipo. Mwaka juzi nilinunua kifaa hiki farmbase kwa Tsh 50000 tu. Karibu mkuu.Anaejua kifaa kinaitwa PIG SNARE kinauzaa bei gani na naweza kukipata wapi msaada please
Habari
Nina ng'ombe anajisaidia kinyesi chepesi muda sasa nawenzake kinyesi chao kizuri kiko kawaida.pia macho yake anayatoa sana mpaka yanaonekana makubwa kuliko kawaida.pia anakohoa kohoa.naomba msaada juu ya hili suala
Miaka kama mitatu anatoa hicho kinyesi na kukohoa kama mpakaAnakohoa na kutoa aina ya hicho kinyesi kwa mda gan?
Miaka kama mitatu anatoa hicho kinyesi na kukohoa kama mpaka
Mwezi wa saba mwaka huuMara ya mwisho kumpatia dawa za minyoo ni lini?