Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Nera
Breed gani ya kuku wa mayai inafaa sehemu za baridi pia mayai yake yana ubora na makubwa,mfano kuna wauzaji kama interchik,silverland.....ambapo breed ni kama hyline,issa brown,bovan n.k..
black
 
Nahitaji kufanya biashara ya kuuza mbuzi, lakini nataka niwauzie viwandani jee ni viwanda gani wanalipa vizuri? Naomba ushauri
 
Tuwasiliane mkuu kwa ....PM. Niko Dar
 
Mtaalamu nisaidie tafadhali Dr. Ngombe wangu anakohoa muda mrefu Kama zaidi ya miezi 6. Nimempa dawa Kama tylosin, laxics ( Wakisema labda ana maji kwenye mapafu na hivyo mpe akojoe Sana ayatoe), Butalex, imisol lakini bado anakonda na kukohoa. Jua likiwaka kidogo tu anasimama kwenye kivuli nakutaguta maji yalipo anajitumbukiza. Ni ugonjwa gani na matibabu yake Ni Nini?

Tafadhali.
 
Seems mtaalamubwetu amekufa maana naona hajibu mahitaji
 
Tafuta mtaalamu aje amuone hyo ng'ombe, maelezo namna hii hayatoshelezi kutoa diagnostic
 
Mwenye utaalam wa ugonjwa wa ng'ombe unaoitwa Kipupwe, tiba na jinsi ya kuuepuka.
 
nimewahi kuwa na ngombe dizaini hii,nilitibu kila aina ya dawa Hadi gharama ilifika zaidi ya laki tatu bila unafuu,Iko siku nikampa Epson salt ,aliharisha sana ila baada ya hapo alibadilika na kupendeza mnoo na nikaghairi wazo la kumuuza ....sikujua tatizo lake lilikuwa nini lakini
 
Mkuu mbona yule 'mdudu' pendwa hujamtaja au imani yako hairuhusu?
Mawasiliano yako ya simu please
 
Habari Dr.

Ng'ombe alikuwa na uvimbe kwenye Chuchu za upande Mmoja. Dr alipokuja alimchoma Dexa kwa ajili ya kuondoa uvimbe na baadae akashauri itumike dawa ya Sindano kwa ajili ya MISTITIS. Baada ya Kutumia Sindano za MISTITIS kwa kumuwekea Ng'ombe kwa siku 3 Asubuhi na Jioni baada ya kumkamua.

MATOKEO
Siku za Mwanzo Ng'ombe alikuwa akitoa Maziwa kama yameganda kidogo na Maji.

Kwa Sasa anatoa Maji na Damu.

JE NIFANYEJE.

NB
Ni Chuchu 1 tu zingine 3 zipo vizuri na uvimbe umepungua kwa 90%. Ng'ombe pia anakula vizuri.





Ahsante.
 
Huyo daktari alikosea (naomba radhi hata kama mimi siyo daktari, but experience teaches) . Ni kawaida chuchu kuwa na mastitis hasa kama mkamuaji ni "mvivu" wa kukamua. Nina tatizo ilo hata hapa ninapoandika.

Dexa inaua maziwa kabisa, ngombe completely by 100% hatoa maziwa. That was a mistake!
Yamenipata yote hayo.
Nilitumia dawa gani:
1. Infusion jets kama Penikan, Utimast IMM, Intramast LC and many others. Weka infusion jet moja kwa chuchu hiyo. kwa siku tatu mfululizo

2. Penstrep - dawa nzuri sana. Intramuscular injection..1 cc per 20kg....then kuzuia systemic infection mchome na hiyo sindano. Then nipe mrejesho.
 
Dr Naomba Ushauri Nina Bata Bukuni Ndiyo Kwa Mara Ya Kwanza Nimefuga
Ametamia Mayai Manne Kuanzia Tarehe 20.07.2022 Mpaka Sasa Hadi Hajaangua Pia Bata Mwenyewe Ametoa Manyoya Yake Kiasi Kingi Mwilini Mwake Yapo Kwenye Mayai

Nimepata Hofu Kwakuwa Sina Uzoefu Lakini Chakula Anakula Vizuri Hasa Ukimpa Majani. Niendelee Kumwacha Tu Ama Labda Mayai Yatakuwa Yameharibika
 
(2. Penstrep - dawa nzuri sana. Intramuscular injection..1 cc per 20kg....then kuzuia systemic infection mchome na hiyo sindano. Then nipe mrejesho.)

1. Penstrep - Hii nimetumia kwa siku 3 Asubuhi na Jioni na angalau imezibua Chuchu na Jioni hii ametoa Majimaji ila siyo mengi, damu hajatoa.

2. Intramuscular injection..1 cc per 20kg....then kuzuia systemic infection mchome na hiyo sindano.

MKUU NADHANI IMEBAKI HII?


Ahsante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…