Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Nashukuru sana mkuu nimeelewa vyema wacha nifuate hayo .
 
Mkuu samahani niliwapa kuku wangu wakubwa tylodox 200 japo si Kwa kuzingatia sana kwa kusuasua sasa nataka kesho nimchinje mmoja kwa kitoweo, kitaalam vipi naweza nikamchinja?
 
Mkuu natamani saana kujua mchanyiko wa chakula Cha kuku wa mayai nahitaji niwe natengeneza mwenyewe.
 
 
me pia kuku wangu kashindwa kusimama na wengine wanasumbuliwa na mafua yasiyo pona mkuu na jicho moja hasa ya kulia hujifumba nisaidie kwa ushauri nini cha kufanya
Habari ndugu,

nimeanza kufuga na case ya kuku kupata na mafua nimekumbana nayo . Ni kama wiki mbili zilizopita kuku walikuwa na mafua na dalili nilizokutana nazo ni kama hizo zako ila zingine ni kama:-
1. Kuku kupiga chafya hasa wanaokua (wenye wiki 6 hadi 12), wakubwa mafua tu yalikua yanatoka puani
2. Harufu mbaya mdomoni na jichoni
3. Jicho moja kuziba hasa kipindi cha asubuhi wanapoamka, then ukilizibua yanaweza toka maji maji au uchafu wenye harufu nao
4. Uzito kupungua kiujumla hasa kwa hao kuku wanaoendelea kukua
5. Vifo pia vilikuepo especially mwanzo kabisa mafua yanapowaanza japo sio vingi

Mimi nilitumia dawa inaitwa FLUBAN, inachanganywa na maji na mimi niliichanganya kwa kipimo cha 2x ya ujazo wa maji ambayo nataka hao kuku wanywe kwa muda wa siku 7. Leo hii kuku wote wamepona nashukuru Mungu, hakuna mafua, hakuna macho kuziba na uzito wao umerudi vizuri kabisa
 
Kuna majani yanatambaa jamii ya marando Ila majani yake uwa ni mapana yanaweka Maua baadae yanakuwa na vitunda vikikauka vinakuwa vigumu kama mawe . Uwa unatwanga Kisha unakuwa unamkamulia Yale maji kwenye chakula ukinuia kuwa aseme baada ya hapo mbwa uwa mkali sana unaweza fanya hata mwezi mzima ilo zoezi
 
theriogenology ngombe wangu anatoa maziwa lita 5 asubuhi na tatu jioni. nataka kumausha maana anakaribia kuzaa. Nifanyeje maana maziwa ni mengi kumwacha kumkamua anaweza kuugua mastitis.
 
Mkuu nimepoteza kuku zaidi ya 50 kwa sababu ya mafua na wengine bado wanaumwa wamenyong'onyea na hawawezi kula wenyewe mpaka niwasaidie. Wamekunywa dawa wiki sasa lakini siwaoni kupata unafuu, na dalili zao zinafanana na hizi ulizozionyesha, wacha nami niwapatie hii dawa ya fluban huenda ikaleta matokeo chanya.
Asante kwa kushea
 
Una case kama ya kwangu--mimi ni 70+
Nilichogundua ni either kuna dawa feki au kuku wetu wamekuwa resistant na dawa zao.
Cha ajabu ukiwapa dawa za binadamu wanaonyesha dalili za kupona.
Nimewapa antibiotics(rangi mbili) na majani wanaonyesha nafuu.
 
Una case kama ya kwangu--mimi ni 70+
Nilichogundua ni either kuna dawa feki au kuku wetu wamekuwa resistant na dawa zao.
Cha ajabu ukiwapa dawa za binadamu wanaonyesha dalili za kupona.
Nimewapa antibiotics(rangi mbili) na majani wanaonyesha nafuu.
Ni dawa gani umewapatia mkuu, na kipimo umefanyaje? Sasa nawapondea pilipili pamoja na tangawizi natia huo mchanganyiko kwenye maji yao ya kunywa lakini bado hawako sawa. Mpaka sasa wamekufa 120, nimechoka kabisa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…