Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Salamu zimfikie ndugu Samia
Huku mtaani ndugu rais kuna malalamiko, wananchi wanasema hawakusomi, hawakuelewi, na nitakueleza nilichosikia huku mtaani!
1. Suala la tozo za miamala
Wananchi wanakusikilizia tu waone utafanya nini, lakini wameanza kuona dalili za wewe kupiga konakona. Kuna kila dalili ya hasira ya wananchi kuwa kubwa zaidi maana wanaona unawafanya kama watoto wadogo wa kudanganyadanganya
2. Uonevu wa jeshi la polisi juu ya wapinzani
Ndugu rais, sasa badala ya kushawishi kwa hoja, serikali yako imegeuka ya mabavu. Raia kwenye vijiwe vya kahawa, magazeti ya asubuhi wanashangazwa na miguvu unayotumia, wanauliza unawapeleka wapi?, mbona kila siku polisi wanaokamatakamata wapinzani, wamefanya kosa gani?
3. Kwenye Chanjo watu wanakwenda na kauli ya Magufuli kuwa chanjo hazifai
Binafsi naamini umeleta chanjo kwa nia njema, umefuata ushauri wa kisayansi. Hata hivyo sayansi ni kitu kimoja na perception ya wananchi ni kitu kingine, wananchi mtaani wanaamini kuna hela ya mzungu umechukua na unatafuta justification. Na hoja ambazo raia wanasema ni kuwa mbona wataalamu waliotwambia chanjo hazifai miezi michache iliyopita ndo haohao leo wanatwambia zinafaa, huko kufaa kumeanza lini. Watu wanaukubali msimamo wa hayati kwenye suala hili na wewe wanakuona kama mabeberu wamekuzidi nguvu
4. Influencers na kundi lililokuwa likikuunga mkono hapo awali linakukimbia kwa kasi
Wapo wale waliosimama kukutetea kwa hatua zako nzuri kabisa mwanzoni mwa utawala wako, watu kama akina Askofu Bagonza, watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii. Leo hii wameanza kujidistance na wewe, wanasema mabaya unayoanza kuyatenda kwa kufanya utawala wa kimabavu kupitia jeshi la polisi yanafuta mazuri uliyoyatenda kwenye siku zako za awali za utawala. Wakati kundi hili likikukimbia, lile kundi linalomkumbuka hayati bado halijakukubali sana, kwa hiyo usipokuwa makini unapoteza uungwaji mkono wa umma hivihivi, Labda uegemeze nguvu zako kwa vijana wa Simon Sirro, lakini hao ni wachache hawafiki hata 50000 nchi nzima, Sijui utawezaje.
5. Miradi ya Hayati hata uisimamie na kuifanikisha vipi, wananchi wanampa credit hayati.
Japo kwenye hili mimi binafsi naona wananchi hawana hoja ya msingi kwa sababu serikali ni taasisi endelevu lakini ukweli ni kuwa huku mtaani bado hawajakuidentify na kitu chako binafsi
Mwanzo raia walisema labda wewe utakuwa mwanademokrasia, mtenda haki lakini mtu wa maendeleo, leo hiyo credit wamekuondolea kwa sababu ya ukandamizaji na uonevu serikali yako inayoufanya kwa wapinzani, lakini wakati huohuo hata miradi unayoendelea kuifanya (Kitu ambacho ni kizuri) raia wanakuona unakamilisha kazi ya Magufuli. Ukipokea ndege, wanasema ni Magufuli huyo, Raia hawajakuelewa wewe ni Magufuli asiye Magufuli, Au ni Muungwana asiye Muungwana?
Mwisho:
Ndugu rais watanzania ni wapole sana lakini wakikuchukia watakuchukia kwelikweli. TENDA HAKI NA EPUKA UONEVU ili ukistaafu wakukumbuke kwa wema la sivyo watakunyanyapaa sana, Haya madaraka huwa yanaisha na yanapita usijisahau sana!