Salamu zimfikie ndugu Samia
Huku mtaani ndugu rais kuna malalamiko, wananchi wanasema hawakusomi, hawakuelewi, na nitakueleza nilichosikia huku mtaani!...
Kuhusu tozo watanzania walio wengi wameelewa faida ya tozo.
watanzania wengi wanataka watoto wao wapate vyumba vya madarasa, madawati, matuidi ya vyoo, maji.
Hospitali vijijini, dawa na barabara zenye kupitika.
Watanzania wengi hawafurahishwi na siasa za kichochezi na zenye lengo la kuvunja amani ya nchi yetu zinazo endeshwa na viongozi wa chadema.
hivyo watanzania wengi wanataka Jeshi la polisi na vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuchukua hatua madhubuti bila kusita kwa wanaharakati au wanasiasa ambao wanajaribu kuvuruga amani ya nchi.
Watanzania wengi wamefurahishwa sana na jitihada za Rais namna alivyo lishughulikia janga la COVID 19 kitaalamu, na kuchukua hatua zinazo endana na maelekezo ya WHO na kisha kupokea chanjo zilizo thibitishwa kitaalamu na pia yeye binafsi kuonyesha mfano wa kuchomwa chanjo.
watanzania wote tupo tayari kuchanjwa.
Hongera sana kwa Rais Samia kwa kuchukua hatua kwa kila jambo kwa utulivu na umakini.