Kuna mshikaji wangu yupo taasisi fulani, akipiga mshindo ananipigia simu anauliza uko wapi? Kwanza sauti tu ntajua ehee! Kimelipuka huko.
Basi utasikia anasema wewe mjinga upo chini ya ulinzi, hapohapo ulipo kama ulikuwa unafanya kazi acha, kama unakula acha. Fasta chukua bodaboda au tax nipo sehemu fulani nalipa hukuhuku.
Basi nikifika nakuta jamaa kakaa anapata safari lager za baridi zinatoa jasho aisee! Huku kaagiza nyama safi nyeupe ambayo haina madhara na kachumbali pilipili. Hapo tutakunywa kula na hela za supu naondoka nayo.
Kwanza kwenye meza yetu wahudumu wanakuwa hawakauki.
Na mimi nikipiga mshindo vilevile kama yeye.
Hii dunia ni tamu jamani ukiamua.