Mtaji milioni 25 - 30

Mtaji milioni 25 - 30

Unamaanisha kwenye biashara ya ufuta pesa ya mtaji ulioweka baada ya mauzo unapata faida mara 2 ya mtaji?Tupe na changamoto zake zipi

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Changamoto zake ni kuibiwa na watu wasio waaminifu. Maana wewe kama nigeni inabidi uwape vijana pesa ili wakanunue ufuta huko porini Kwa wakulima. Sasa Kuna watu unawapa pesa wanaenda kuweka heshima bar huku wakinigamba.

Kwa ufupi hii biashara inalipa kama utapata mzigo Kwa wakati na kuupeleka ghalani
 
Mkuu,Naelewa hali uliyo nayo.Kwanza kupata Loan ya 35 Milion ina maana una cashflow nzuri na pia una dhamana nzuri.Kwa vigezo hivyo wewe unaweza kufanya Biashara lakini PIA ninahisi utakuwa kwenye Ajira which means kufikiria aina nyingine ya Biashara tena inayoweza Generate kama uliyoiweza iko Very Trick.Ilaa naamini mawazo yapo Mengi.

Mimi nitakuja PM nikupe contacts zangu then Tuangalie namna ambavyo tunaweza kushauriana.Ila kwa kuangalia haraka haraka naona inabidi uangalie Fursa ya Biashara ambayo tayari inajiendesha ambayo unaweza ingia na kuanza kutengeneza Revenue Mapema.Biashara utayowekeza Wekeza Not More than 20M
Msiende kumuumiza huko PM. Huwa mnakuwa na lugha tamu kama hii uliyotumia kumbe moyoni ni mafisi.
 
1. Kama uko kijijini yaani siyo Dar, Arusha , Mwanza nunua mchomoko. Kadiria safari ya kulala na 50000 tu na mafuta full. Usiwake tamaa ya kuingiza laki.

2. Kama una banda tafuta afisa mifugo akuelekeze ufugaji wa kuku wa kienyeji. Usifanye bila maelekezo. Nunua incubator ya mayai 300 kwa gharama si zaidi ya milion.
3. Mpe mama mtaji wa tshs 3m. Mnunulie freezer 3kubwa na madell yasipungue 10. Nunua baiskeli na ajili vijana wauze barafu mashuleni. Utashukuru. Barafu zitakata Novemba. Hii pia inategemea ulipo. Mfano kwa Mfindi haiwezekani.

Kwa mraji huo biashara zote juu waweza kuzifanya kwa pamoja
 
Tudondolee mkuu imekaaje?

Iko vizuri ukiuza mzigo wa million 30 hukosi faida ya 4 million ukikosa bas 3 million hapo ushatoa kila kitu kuanzia gari, ushuru na pesa za kuhonga njiani.

Soya nzuri na iliyo nafuu ipo Zambia
Ukifika border unakatisha shilling kwa Kwacha na faida inakuwa nzuri ukikuta rate ya kwacha ipo chini

Kuhusu wateja wapo wa kutosha sababu utauzia border.

Alafu mimi ke usiniite mkuu [emoji1787]
 
Msiende kumuumiza huko PM. Huwa mnakuwa na lugha tamu kama hii uliyotumia kumbe moyoni ni mafisi.
Mkuu,Upo Sahihi,Naamni mpaka amefikia kuwa na uwezo wa kuwaza kutafuta alternative investment maana yake anao uwezo wa kufanya uamuzi na kutambua iwapo kuna dalili za kufanyiwa utapeli wa aina yoyte ile.Ila ni vizuri akakumbushwa Ili ajihadhari zaidi
 
Nitakutafuta aisee
Iko vizuri ukiuza mzigo wa million 30 hukosi faida ya 4 million ukikosa bas 3 million hapo ushatoa kila kitu kuanzia gari, ushuru na pesa za kuhonga njiani.

Soya nzuri na iliyo nafuu ipo Zambia
Ukifika border unakatisha shilling kwa Kwacha na faida inakuwa nzuri ukikuta rate ya kwacha ipo chini

Kuhusu wateja wapo wa kutosha sababu utauzia border.

Alafu mimi ke usiniite mkuu [emoji1787]
 
Biashara ya kukupa laki kwa siku kama faida ni ngumu kwa mtaji huo; nachoweza kukushauri; pombe zinanyweka sana, kama uko na urafiki na mtu mwenye pub, club au bar yenye mauzo mengi kwa siku, kaeni mjadili jambo.​
 
🀣🀣🀣 HAO WANAKUITA PM SIJUI DM SIJUI INBOX... Utarudi baada ya siku kadhaa kulaumu watu wa JF...
Una pesa nzuri ambayo hata mimi nikikujua unapatikana wapi ni rahisi kukutapeli kiulaini bila kiwembe kisu panga wala bunduki.... TAKE CARE young man
 
Kaa chonjo na hawa raia wanaokuita PM usije ukafa na presha maana ukiona mtu anacheka jua kuna anaelia...mawazo ya wadau weng ni sahihi ila angalia ambalo atleast una ka uzoefu ka hapa na pale usije ukadumbukza hiyo hela mahali huwez kupga mbizi bank wakala kichwa,kila la kheri
 
Back
Top Bottom