Mtaji siyo tatizo kwa walio wengi, tatizo ni sisi wenyewe kutojua jinsi ya kuanza.

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
2,973
Reaction score
3,904
Kuna watu wengi sana wanaolalamika kushindwa kuanza kufanya biashara kwa madai kwamba hawana mitaji. Ukweli ni kwamba kwa walio wengi madai ya kutokuwa na mtaji siyo ya kweli badala yake ukweli ni ukosefu wa elimu ya ujasiria mali.

Mfanya biashara Reginald Mengi aliwahi kusema, nami nakubaliana naye kwamba, kama mtu hawezi kufanya biashara kwa kutumia laki 1 na kufanikiwa hata akipwe mtaji wa Mil 100 hawezi kuibadilisha kuwa milion 150 - Haiwezekani kwa sababu Kanuni zinafanana.

Utakuta mtu ni mwl, anataka mtaji, wakati mtaji ni sebule ya nyumbani kwake na wanafunzi watatu hadi 5 wa kuanzia.
Niliwahi kumwuliza rafiki yangu hivi ukipata mtaji wo wote unaotaka wewe ungefanya nini? Akaniambia yafuatayo.
Nitanunua kiwanja kikubwa na kujenga shule kubwa ya sekondary yenye kila kitu - yaani madarasa, mabweni, walimu, maabara, vitabu vyote, viwanja nk - yaani kila kitu. Kisha nitatangaza kwa nguvu ktk vyombo vya habari.

Ukweli ni kwamba huyu rafiki yangu atafeli kwa uhakika kwa sababu, mimi siwezi kumpeleka mwanangu kwenye shule ambayo sijui historia yake hata kama ni kubwa namna gani - it is too risky. Lazima uanze chini kidogo kidogo ili ujenge jina zuri ( reputation). Huyu rafiki yangu, lazima angekwama kulipa mkopo. Kama atafanikiwa ni baada ya muda mrefu. Hapo lazima atakuwa ameshagombana na mwenye pesa - benki.

Shule nyingi ninazofahamu mimi hapa mjini zenye majina makubwa hakuna iliyoanza na wanafunzi 100 au zaidi kama alivyotaka rafiki yangu. Wengi wameanza na watoto chini 10 mfano Esacs, kamene nk.

Ndugu zangu, tujifunze kuanza chini na kupanda juu taratibu. Tusitake makubwa kuliko uwezo wetu. Biashara iko kichwani kwanza kabla haijwa halisi ktk hali halisi.

Biashara NI lazima ianze na kila unachokijua wewe ama una uzoefu nacho na kukipenda. Siyo kile ulichoambiwa kinalipa - hapana. kila Kitu kinalipa, hata kuimba au kuigiza kunalipa. Hoja ni kwamba je, unajua,unazoefu, unapenda na una uwezo kuimba au kuigiza? Na kwa kawaida ukishazingatia hilo, mtaji hauwi tatizo kama ilivyo tatizo kwa wengi sasa. Tatizo la wengi ni ufahamu.

Utakuta mwanasheria anatafuta mtaji wa kufungua ofisi ya huduma YA kisheria Ubungo Plaza - Haiwezekani. Ukimwuliza nani wateja wako wa kukuwezesha kulipa kodi na gharama zingine, Hana jibu. Kumbe alipaswa kuanza kutoa huduma hiyo kuanzia sebulen kwake then ofisi ndogo 80,000 mitaani, kabla ya ubungo Plaza.

Utakuta mtu anataka kwenda china kuchukua mzigo wa mil 50, kabla hajafanya biashara hiyo hiyo hapa bongo na kupata uzoefu kidogo kwa mtaji wa milioni moja au laki 1.

Hoja yangu si kwamba mtaji siyo tatizo la hasha, hoja yangu ni kwamba kwa walio wengi humu jf, tatizo ni ufahamu wa kutojua kitu cha kufanya kuliko tatizo la mtaji. Wapo wachache ambao kweli wana uzoefu na uwezo na wana matatizo la mtaji, lakini si wengi kama tunavyoona vilio vingi hapa JF- jukwaa la uchumi na kwinginepo mtaani. Tatizo la wengi ni ufahamu, agree or not.

Hivi unajua kwanini benki zinawanyima baadhi ya watu fedha na kuwapa wengine. Wanataka kujua kama una uzoefu na kama umeanza chini kuja juu au laa. Wengi hatuwaelewi watu wa benki lakini ukweli ni kwamba benki wana nia njema na sisi. Hataki kutupa pesa nyingi kuliko uwezo na uzoefu wetu wa kulipa. Wanajua kuliko sisi. kutunyima sisi mitaji tunayotaka ni kutusaidia kwamba tukaanzie chini kwanza. Kumbuka benki wapo ili kukopesha. Wanaokopa ndo faida, wanaoweka tu fedha siyo deal kwao. Ukiona wanatunyima maana yake tunakosa uzoefu, tunaka kuanzia juu kama rafiki hapo juu. which is wrong.

Nahitimisha kwa kusema tuwe tayari kuanza chini kidogo kwa faida yetu kwa sababu kanuni ya kubadilisha au kufanya biashara kwa mtaji wa mil 100 kuwa mil 150 ni sawa na kanuni ya kuanzia na laki 1 na kuibadisha kuwa laki 2 kibiashara.
Nawasilisha.
 
dah ... umemaliza somo lote la ujasiriamali kwa post hii

big up mkuu Aweda .... natumain mabenki yanaweze kutumia mada kama hii kuelimisha uma ili mwisho wa siku waweze kupata wakopaji wengi zaidi
 
Huo ungekuwa utaratibu mzuri sana. Nadhani kuna benki ktk nchi zingine zinafanya hivyo. Nimesikia tu, sina hakika.
 
Full doze ya ujasiriamali!! Yuko clear,simple na analugha nzuri ya kumwelesha mtu! Jamaa ni kichwa! Big up mkuu tumekuelewa sana!!
 
asante sana kwa kututua moyo siye wenye vipato vidogo.
 
Mil 100 huanza na 1. Hatua 100 huanza na hatua 1. mbuyu huanza mche. Hata sisi tunazaliwa watoto wadogo then tunarefuka. In short Kila kitu kinaanza kidogo na kukua. Mimi nashanagaa kwenye biashara tunataka tuanzie juu - Ngumu.
 
Mikael P Aweda mi nakubaliana na wewe kwa 100%.

Mil 100 huanza na 1. Hatua 100 huanza na hatua 1. mbuyu huanza mche. Hata sisi tunazaliwa watoto wadogo then tunarefuka. In short Kila kitu kinaanza kidogo na kukua. Mimi nashanagaa kwenye biashara tunataka tuanzie juu - Ngumu.
 
Last edited by a moderator:
Kuna biashara ambazo huwezi kuanza 'kidogo-kidogo' kwa kuanzia na mtaji wa tsh. laki moja au laki mbili.....
Tuangalie mifano michache ifuatayo :-
  • Biashara ya dala dala. Lazima ununue basi moja ambalo utaanza nalo. Basi moja (Toyota coaster) ni tsh. millioni 20.
  • Biashara ya nyumba ya kupangisha. Huwezi kuanza 'kidogo-kidogo'. Lazima ujenge nyumba moja ya kuanzia. Kujenga nyumba moja ya 'kawaida' ni tsh. millioni 15 hadi 25 (kwa kutegemea eneo na bei ya kiwanja).
  • Biashara ya kuuza maji Dar es Salaam. Huwezi kuanza 'kidogo-kidogo'. Lazima uchimbe kisima kwa tsh. million 5, ununue pampu ya maji tsh. laki 5, ununue ma-tanki ya maji tsh. million 2, uweke mabomba ya kuuzia maji, n.k Jumla ya mtaji unaohitaji ni kama tsh. millioni 15.

Kwa maana hiyo, kwa kutegemea mtu anataka kuanzisha biashara gani, lazima awe na mtaji wa kutosha kuwezesha bishara husika kuweza kuanza.
Mtaji pungufu hautaweza kuanzisha biashara kama inavyotakiwa (kick-start the business). Mtaji pungufu ndio chanzo kikuu cha kuangusha mradi unaoanza.
Ni sawa na ndege (aeroplane) inayotaka kuruka, lazima ianze na nguvu kubwa ndio iweze kupata msukumo wa kuruka angani. Mradi ni hivyo hivyo, lazima uanze na mtaji unaotosheleza ndio mradi uweze kupata nguvu ya kusonga mbele.

Tusikatishe tamaa wajasiriamali wanaotaka kuanzisha miradi yao. Tuwape moyo, wanaweza.
 
Mu israeli,
Hapa changamoto mbili ntakupa.
Kwanza ni karibu umetoka nje ya mada.
Mimi niko wa wajasiria mali wa chini kabisa. Mimi nataka kuwapa mbinu hawa wajasiria mali wadogo sana ambao mil moja tu anaisikia kwenye redio. Wengine mshahara ni laki moja. Jana niliongea na mtu aliyefanya kazi ya kuuuza duka la mtu miaka 9. Hajui kitu cha ufanya. Huyu ndo namwambia aanze chini kwenda juu. Hao wenye mil 20 kwenda juu ni sio wajasiriamali wadogo. Mtu ambaye benk inaweza kumpa kiasi hicho lazima ana dhamana kubwa - Amesha toka.

Pili, Huwezi u kutoka unakojua ukatafuta mil 20 ukaanza biashara ya dala dala au ukaanza kujenga nyumba za kupanga nk. Mimi nilifanya kosa hilo ktk biashara fulani likanigharimu sana.( Kumbuka natumia ID halisi,ukitaka unaweza kujua kunitembelea). Lazima ujue kwanza in and out ya biashara yo yote unayotaka kufanya. Mwekezaji tu ndo anaweza kufanya hivyo kwa sababu yeye ni pesa ndo inamfanyia kazi. Hahitaji uzoefu.
 
Mkuu Aweda ni Kweli kabisa, Na Mitaji imekuwa ikitumika kama Ngao ya mtu kuhararisha kuto fanya biashara, yaani mtu ili usiendelee kumuliza story za kujiajiri atakuambia sina Mtaji,

Ila ukweli ni kwamba Mtaji si ishu ishu ni mbinu na mikakati, Na nikweli kabisa kwamba kanui za biashara ni hizo hizo uwe na mataji wa Bilioni moja na mwingine mtaji wa elfu kumi mbinu ni hizo hizo,

Kuna mdau kasema kuna baadhi ya Biashara lazima uanze na mitaji mikubwa, Mimi nataka kumuhakikishia kwamba Biashara zote unazo ziona hapa DUNIANI hakuna iliyo anzia juu, Makampuni kama Cocacola, Peps, Microsoft na kazalika zote zilianza with Nothing, walianza na zero, Wakina HONDA walianza kwa kutengeneza Baiskeli za Watu,

Kule china kuna watu wanaanza Transportation Business na mkokoteni wa kusukuma lakini kwa sababu ana determination, mwisho wa siku huja kumiliki Magari ya mizigo,

Biashara ya Kubeba abilia wapo waliaonza kwa kubeba watu mgongoni na baadae Baiskeli na baadae, Pikipiki mpaka kuja kumiliki mabasi,

Biashara zote zinakubalika kuanzia chini, Tatizo la watanzania ni kutafuta utajiri na kutaka Kusifiwa na Ndugu, Jamaa na marafiki kwamba ana Biashara kubwa,

Na Mara nyingi ukiwa na Spirit ya Ujasirimali ni lazima utafanikiwa tu lakini kama una spirt ya kufanya biashara haya utayaona ni kama ndoto,

Kule Kenya Marehemu MUGUKU aliacha kazi ya kufundisha na kuanza na kufuga kuku wasio zidi Kumi tena kwa pesa ya kusaidiwa na Baba yake, lakini kwa sababu alisha jitolea, mwisho wa siku alikuja kuibuka kuwa kati ya Matajiri watano nchini Kenya na Mtu pekee single aliye kuwa na Share Nyingi kwenye Benki ya Equity,

Na alipo hojiwa alisema kama angeendelea kubakia na kazi ya Kuajiriwa asingekuwa hapo alipo na huenda angekufa masiikini

UJASIRIMALI SIKU ZOTE NI MUGUMU SANA NA KINACHO TAKIWA NI UVUMILIVU WA HALI YA JUU KABISA, NA MARA NYINGI MATUNDA YA UJASIRIMALI HUONEKANA BAADA YA MUDA MREFU INGAWA HUWA NI MATUNDA YASIYO ISHA KWA URAHISI, TOFAUTI NA MATUNDA YA KUFANYA BIASHARA AMBAYO NI SAWA NA MAUA,
 
Kweli kabisa kwa wengi tatizo sio mtaji.Wengine tatizo ni kuto jitambua kwamba vile alivyo ni mtaji tosha.Na wengine tunafikiri kwamba Dsm ni kila kitu na hivyo tunaua mitaji yetu.Hakuna mtaji mkubwa wala mdogo, suala ni kujipanga vizuri na kuwa na mikakati iliyosimama.
 
Ila mimi napingana na Mtoa maada hapo kwenye Elimu ya Ujasirimali, Tatizo la watu wengi si Elimu bali ni Sprit ya Ujasirimali ndo watu hawana, kama huna Spirt hata Ukiwa na Phd Ya Ujasirimali ni kazi Bure, na hata hivyo Kwa Duniani hakuna Chuo kinacho weza kumfanya mtu akawa Mjasiromali bali kuna Vuo vya Kufundisha Business skills kama Marketing, Business palning, Customer care na kazalika,

Hakuna Chuo cha Kufundisham Commitment, Inovation, Risk taking, Uvumilivu, na zinginezo, that is wahy ni vigumu kufundisha mtu Ujasirimali, unaweza mfundisha kufanya biashara lakini si Entrprenership.

Na pamoja na kwamba kuna Born and Made Entrpreners, Lakini hata Made Entrepreners lazima anakuwa na spriti ya Entrprenership, watu kama wakina Dell, Thomas Edson, Honda na wengineo ni BORN kwa sababu hawa kujifunza popote pale,

Tanzania inatakiwa elimu ya Biashara itolewe kwa Rough Diomond, kuna watu ambao ukiwaona ni sawa na Alumasi ambayo haijasafishwa na ukiisafisha tu inakuwa rear Diaomond, na kosa linalo fanyika ni kwenda kutoa elimu ya Biashara bila kujalisha huyu ana muelekeao wa ujasirimali au la,

So ni lazima Tujue kwamba Ujasirimali ni zaidi ya Elimu, Huhitaji elimu ya aina yoyote ile wewe kuwa mjasirimali,ila unahitaji elimu ya biashara ili ufanye biashara, Ila kuwa mjasirimali huhitaji chochote kile,

Hakuna kitu ambacho mtu nahitaji ili awe mjasirimali, si pesa wala si nini, na wala huhitaji program za Serikali ili uwe Entrepreners, Unahitaji tum kuwa na Spirit ya Ujasirimali basi na si kingine kile

Nazani wakuu mtakua mmenipata vyema
 
Mkuu una akili sana. Mimi nilitumia m10 kufungua stationery, lakini pamoja ni mipesa yote ikafa. Jamaa wakaniambia nilitakiwa nifuate zindiko la biashara sumbawanga (sasa nimeelewa kumbe zindiko = principles za ujasiriliamali).

Ndo problem ilipo, ni kweli Watu wengi hutumia mitaji mikubwa sana na mwisho wa siku huishia kupata hasara kubwa sana, na that is wahy unaambiwa ni lazima kwenda step by step huku ukisoma mazingira na wewe ukijifunza taratibu,

Ila kufeli ni kujifunza mkuu na utakapo anza tena nina uhakika hutafeli
 
Kuna watu wengi sana wanaolalamika kushindwa kuanza kufanya biashara kwa madai kwamba hawana mitaji. Ukweli ni kwamba kwa walio wengi madai ya kutokuwa na mtaji siyo ya kweli badala yake ukweli ni ukosefu wa elimu ya ujasiria mali.

Mfanya biashara Reginald Mengi aliwahi kusema, nami nakubaliana naye kwamba, kama mtu hawezi kufanya biashara kwa kutumia laki 1 na kufanikiwa hata akipwe mtaji wa Mil 100 hawezi kuibadilisha kuwa milion 150 - Haiwezekani kwa sababu Kanuni zinafanana.

Utakuta mtu ni mwl, anataka mtaji, wakati mtaji ni sebule ya nyumbani kwake na wanafunzi watatu hadi 5 wa kuanzia.
Niliwahi kumwuliza rafiki yangu hivi ukipata mtaji wo wote unaotaka wewe ungefanya nini? Akaniambia yafuatayo.
Nitanunua kiwanja kikubwa na kujenga shule kubwa ya sekondary yenye kila kitu - yaani madarasa, mabweni, walimu, maabara, vitabu vyote, viwanja nk - yaani kila kitu. Kisha nitatangaza kwa nguvu ktk vyombo vya habari.

Ukweli ni kwamba huyu rafiki yangu atafeli kwa uhakika kwa sababu, mimi siwezi kumpeleka mwanangu kwenye shule ambayo sijui historia yake hata kama ni kubwa namna gani - it is too risky. Lazima uanze chini kidogo kidogo ili ujenge jina zuri ( reputation). Huyu rafiki yangu, lazima angekwama kulipa mkopo. Kama atafanikiwa ni baada ya muda mrefu. Hapo lazima atakuwa ameshagombana na mwenye pesa - benki.

Shule nyingi ninazofahamu mimi hapa mjini zenye majina makubwa hakuna iliyoanza na wanafunzi 100 au zaidi kama alivyotaka rafiki yangu. Wengi wameanza na watoto chini 10 mfano Esacs, kamene nk.

Ndugu zangu, tujifunze kuanza chini na kupanda juu taratibu. Tusitake makubwa kuliko uwezo wetu. Biashara iko kichwani kwanza kabla haijwa halisi ktk hali halisi.

Biashara NI lazima ianze na kila unachokijua wewe ama una uzoefu nacho na kukipenda. Siyo kile ulichoambiwa kinalipa - hapana. kila Kitu kinalipa, hata kuimba au kuigiza kunalipa. Hoja ni kwamba je, unajua,unazoefu, unapenda na una uwezo kuimba au kuigiza? Na kwa kawaida ukishazingatia hilo, mtaji hauwi tatizo kama ilivyo tatizo kwa wengi sasa. Tatizo la wengi ni ufahamu.

Utakuta mwanasheria anatafuta mtaji wa kufungua ofisi ya huduma YA kisheria Ubungo Plaza - Haiwezekani. Ukimwuliza nani wateja wako wa kukuwezesha kulipa kodi na gharama zingine, Hana jibu. Kumbe alipaswa kuanza kutoa huduma hiyo kuanzia sebulen kwake then ofisi ndogo 80,000 mitaani, kabla ya ubungo Plaza.

Utakuta mtu anataka kwenda china kuchukua mzigo wa mil 50, kabla hajafanya biashara hiyo hiyo hapa bongo na kupata uzoefu kidogo kwa mtaji wa milioni moja au laki 1.

Hoja yangu si kwamba mtaji siyo tatizo la hasha, hoja yangu ni kwamba kwa walio wengi humu jf, tatizo ni ufahamu wa kutojua kitu cha kufanya kuliko tatizo la mtaji. Wapo wachache ambao kweli wana uzoefu na uwezo na wana matatizo la mtaji, lakini si wengi kama tunavyoona vilio vingi hapa JF- jukwaa la uchumi na kwinginepo mtaani. Tatizo la wengi ni ufahamu, agree or not.

Hivi unajua kwanini benki zinawanyima baadhi ya watu fedha na kuwapa wengine. Wanataka kujua kama una uzoefu na kama umeanza chini kuja juu au laa. Wengi hatuwaelewi watu wa benki lakini ukweli ni kwamba benki wana nia njema na sisi. Hataki kutupa pesa nyingi kuliko uwezo na uzoefu wetu wa kulipa. Wanajua kuliko sisi. kutunyima sisi mitaji tunayotaka ni kutusaidia kwamba tukaanzie chini kwanza. Kumbuka benki wapo ili kukopesha. Wanaokopa ndo faida, wanaoweka tu fedha siyo deal kwao. Ukiona wanatunyima maana yake tunakosa uzoefu, tunaka kuanzia juu kama rafiki hapo juu. which is wrong.

Nahitimisha kwa kusema tuwe tayari kuanza chini kidogo kwa faida yetu kwa sababu kanuni ya kubadilisha au kufanya biashara kwa mtaji wa mil 100 kuwa mil 150 ni sawa na kanuni ya kuanzia na laki 1 na kuibadisha kuwa laki 2 kibiashara.
Nawasilisha.

Mkuu naomba nikutafute nahisi tunaweza kuwa na mengi ya kuzungumza...nimechukua namba yako yangu ninaku PM
 
Mkuu Aweda ni Kweli kabisa, Na Mitaji imekuwa ikitumika kama Ngao ya mtu kuhararisha kuto fanya biashara, yaani mtu ili usiendelee kumuliza story za kujiajiri atakuambia sina Mtaji,

Ila ukweli ni kwamba Mtaji si ishu ishu ni mbinu na mikakati, Na nikweli kabisa kwamba kanui za biashara ni hizo hizo uwe na mataji wa Bilioni moja na mwingine mtaji wa elfu kumi mbinu ni hizo hizo,

Kuna mdau kasema kuna baadhi ya Biashara lazima uanze na mitaji mikubwa, Mimi nataka kumuhakikishia kwamba Biashara zote unazo ziona hapa DUNIANI hakuna iliyo anzia juu, Makampuni kama Cocacola, Peps, Microsoft na kazalika zote zilianza with Nothing, walianza na zero, Wakina HONDA walianza kwa kutengeneza Baiskeli za Watu,

Kule china kuna watu wanaanza Transportation Business na mkokoteni wa kusukuma lakini kwa sababu ana determination, mwisho wa siku huja kumiliki Magari ya mizigo,

Biashara ya Kubeba abilia wapo waliaonza kwa kubeba watu mgongoni na baadae Baiskeli na baadae, Pikipiki mpaka kuja kumiliki mabasi,

Biashara zote zinakubalika kuanzia chini, Tatizo la watanzania ni kutafuta utajiri na kutaka Kusifiwa na Ndugu, Jamaa na marafiki kwamba ana Biashara kubwa,

Na Mara nyingi ukiwa na Spirit ya Ujasirimali ni lazima utafanikiwa tu lakini kama una spirt ya kufanya biashara haya utayaona ni kama ndoto,

Kule Kenya Marehemu MUGUKU aliacha kazi ya kufundisha na kuanza na kufuga kuku wasio zidi Kumi tena kwa pesa ya kusaidiwa na Baba yake, lakini kwa sababu alisha jitolea, mwisho wa siku alikuja kuibuka kuwa kati ya Matajiri watano nchini Kenya na Mtu pekee single aliye kuwa na Share Nyingi kwenye Benki ya Equity,

Na alipo hojiwa alisema kama angeendelea kubakia na kazi ya Kuajiriwa asingekuwa hapo alipo na huenda angekufa masiikini

UJASIRIMALI SIKU ZOTE NI MUGUMU SANA NA KINACHO TAKIWA NI UVUMILIVU WA HALI YA JUU KABISA, NA MARA NYINGI MATUNDA YA UJASIRIMALI HUONEKANA BAADA YA MUDA MREFU INGAWA HUWA NI MATUNDA YASIYO ISHA KWA URAHISI, TOFAUTI NA MATUNDA YA KUFANYA BIASHARA AMBAYO NI SAWA NA MAUA,

Well described mkuu. Congratulation. Tuko pamoja.
 
Ila mimi napingana na Mtoa maada hapo kwenye Elimu ya Ujasirimali, Tatizo la watu wengi si Elimu bali ni Sprit ya Ujasirimali ndo watu hawana, kama huna Spirt hata Ukiwa na Phd Ya Ujasirimali ni kazi Bure, na hata hivyo Kwa Duniani hakuna Chuo kinacho weza kumfanya mtu akawa Mjasiromali bali kuna Vuo vya Kufundisha Business skills kama Marketing, Business palning, Customer care na kazalika,

Hakuna Chuo cha Kufundisham Commitment, Inovation, Risk taking, Uvumilivu, na zinginezo, that is wahy ni vigumu kufundisha mtu Ujasirimali, unaweza mfundisha kufanya biashara lakini si Entrprenership.

Na pamoja na kwamba kuna Born and Made Entrpreners, Lakini hata Made Entrepreners lazima anakuwa na spriti ya Entrprenership, watu kama wakina Dell, Thomas Edson, Honda na wengineo ni BORN kwa sababu hawa kujifunza popote pale,

Tanzania inatakiwa elimu ya Biashara itolewe kwa Rough Diomond, kuna watu ambao ukiwaona ni sawa na Alumasi ambayo haijasafishwa na ukiisafisha tu inakuwa rear Diaomond, na kosa linalo fanyika ni kwenda kutoa elimu ya Biashara bila kujalisha huyu ana muelekeao wa ujasirimali au la,

So ni lazima Tujue kwamba Ujasirimali ni zaidi ya Elimu, Huhitaji elimu ya aina yoyote ile wewe kuwa mjasirimali,ila unahitaji elimu ya biashara ili ufanye biashara, Ila kuwa mjasirimali huhitaji chochote kile,

Hakuna kitu ambacho mtu nahitaji ili awe mjasirimali, si pesa wala si nini, na wala huhitaji program za Serikali ili uwe Entrepreners, Unahitaji tum kuwa na Spirit ya Ujasirimali basi na si kingine kile

Nazani wakuu mtakua mmenipata vyema

Mkuu leo nakubaliana na wewe mia kwa mia. Katika mmoja ya post zako za huko nyuma sikukuelewa naona leo tuko pamoja kabisa. Thx a lot for good contiribution.
 
Back
Top Bottom