T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Huwa mnalalamika situation ya biashara na hamtoi details hasa juu ya location. Unakuta mtu analalamika kitimoto hailipi unajikunja kumuelekeza kumbe jamaa yupo Unguja.Kwaiyo mkuu tufanye biashara gani
Nina kifremu naambiwa jirani kwenye godown hapa kabla sijapanga aliuza unga wa jumla alikuwa anauza sana watu wanapishana semi zinatoka Iringa uko zinajaza. Jamaa akafilisika eti watu wanajiuliza ilikuwaje, simply ni kwamba alikuwa anafanya biashara ya sifa kama wewe. Siku ukiagiza canter mvua imenyesha, likatumbukia mtoni likamwaga unga lazima uchanganyikiwe. Hasara moja inakula faida ya siku nyingi sana.
Yaani kwenye inventory ya milioni 40 unapata laki tano??? Biashara yangu ndogo sana ila nikitumia 5M huwa napata laki tano, yaani unafanya 10 times ya hela yangu na unateseka zaidi yangu ila faida tunalingana.
Nishawahi fanya research ya vyakula vya jumla kama mchele na unga, au mahindi. Kitu kikubwa kule ni uchawi, ila sio faida. Nimekaa sana Tandika nasoma wafanyabiashara na madalali nikajihakikishia ni biashara kichaa. Eti mtu ulete tani 20 za mchele upate faida milioni moja, si wehu huo. Halafu hasara ikija sasa, milioni tatu nne kawaida.
Unakuwa mfanyabiashara unaishi kwa hasira mtu akikukanyaga unampiga. Sura imekakamaa hela unazo ila hupendezi mawazo tu.