Mtaji wa 46M faida 540,000, pia mtaji wa 45M faida 576,000

Mtaji wa 46M faida 540,000, pia mtaji wa 45M faida 576,000

Tafuta leseni ya Microfinance mkuu.

Kausha Damu ina Hela sana.

Ukifanikiwa kuzungusha milioni 30 tu unapata Faida Ghafi Milioni 6 kwa mwezi ( ambayo ni riba 20% )
 
Hiyo sio biashara mkuu!! Yaani 45m upate faida hiyo?!! Wakati kuna sehemu unaifanyia biashara, hiyo pesa kwa mwezi unapata si chini ya milioni 15?!!
Wapi huko, niweke million 45 nikapate million 15 kwa mwez. Means ndani y miez 3 hela imerud

Acha uongo, ona aibu
 
Habari wakuu mnaionaje hizi baishara ni za kuendelea kufanya kweli tandam ya gari ya sukari inabeba mifuko 600 ya sukari unaiuza kwa miezi 2 na faida yake ni 540,000 wakati huo gharama za manunuzi 46m faida kwa Kila mfuko jumla jumla ni tsh 900.

Wakati huo huo mtaji wa gari ya ngano 45m hapo gari ya ton 32 sawa na mifuko 1280 kwa Kila mfuko ukiuza jumla faida ni tsh 450 sawa jumla ya 576,000 kwa mifuko yote ambayo unaiuza kwa miezi 2.

Je, wakuu hii biashara inanichanganya sana mtaji mkuwa faida kidogo, tupeane fursa za hela ili tubadilishe biashara tupate faida anagalau inayoendana na mtaji.
"consistency".

Wenzako hiyo wanauza kabla haijateremshwa kwenye gari.

Usiwe na shaka, ukikuwa utazowea.
 
Mbona kama risk sana , au mtaji wako uko covered na bima ,
46m kwa profit ya lak 5 . Kwa miez miwili hapn bora uweke Fixed account

Kwa million 20, wenzako wanaingiza 300k had 500,k per day,

Pia x 10000000 ujenge lodge
 
Back
Top Bottom