Mtaji wa 46M faida 540,000, pia mtaji wa 45M faida 576,000

Nipo Kanda ya ziwa,kg 50 ya nje yenyewe last week tuliipata pale Kwa mo Kwa 140000 tumeiuza Kwa 160000,Kagera sugar wameanza kutoa sukari kg 25 inapatikana Kwa 71000 jumla tunaiuza 76000-78000,ndugu yangu Kwa mauzo hayo haufanyi biashara ya jumla,ukichukua mifuko 600 lazima uwauzie wanaoenda nao kuuza juma na sio mfuko mmoja mmoja.Ushauri wangu you are in a wrong place if it real your doing such business.
Inawezekana kwa eneo uliopo ww uko mnatengeneza hiyo faida ila Kuna maeneo niliopo mim uku nzega nishindani Kila mtu anataka auze so faida Iko hivo ukiweka Bei kubwa huuzi
 
Nipo Kanda ya ziwa,kg 50 ya nje yenyewe last week tuliipata pale Kwa mo Kwa 140000 tumeiuza Kwa 160000,Kagera sugar wameanza kutoa sukari kg 25 inapatikana Kwa 71000 jumla tunaiuza 76000-78000,ndugu yangu Kwa mauzo hayo haufanyi biashara ya jumla,ukichukua mifuko 600 lazima uwauzie wanaoenda nao kuuza juma na sio mfuko mmoja mmoja.Ushauri wangu you are in a wrong place if it real you are doing such business.
Mkuu hapo awali miaka nyuma kidogo ndo ilikua faida kwa mfuko 35000 baada ya supply kuwa wengi ikaingia tabia ya ushindani Kila mtu kutaka kuuza kufikia Sasa kushusha Bei masupply wapya wanashusha Bei ili wauze sana mnajikuta mnakimbizana nao Bei hiyo hiyo ya faida 900
 
Ndugu acha izo bhana na hilo jina.

BTT. Kilimo nilicho na experience nacho ni mpunga bwashee, kwa mtaji huo mi nitaishi vizuri bila karaha na kila mwaka ninaweza kulima kwa kuongeza mtaji. Naweza ongeza na kilimo cha kitunguu na nyanya kwa kuanza na ekari moja moja.
Kilimo we kione tu kwenye vipeperushi. Kilimo ni zaidi ya jeshi.
 
Umeweka UTT hiyo Mil 46 kwa mwezi utapata around 400,000.. miezi miwili utapata zaidi ya 800,000
Yaani milioni 46 halafu nitafute faida ya laki 4 kila mwezi? Kama kama biashara kichaa hiyo.
 
Sasa mkuu UTT kwa mwaka unapewa 11% Sasa kwa m100 ni sawa na 11m unapewa. Sasa mkuu hakuna biashara ya kuzunguusha hiyo m100 ikazaa zaid ya 11m nnayopewa na UTT.
Ndio maana kampuni za kubet zinafanikiwa sana hapa bongo.
 
Nashauri chukua hiyo pesa kaweke UTT, utapata faida kiliko hicho unafanya.
Suppose akichukua hiyo hela, akichukua aka-beti kwa timu tofauti tofauti anaweza kupata zaidi uliko hiyo ya sukari.

Ijumaa hii Yanga anatolewa, simba anatolwa, akiweka milioni moja milioni anapa zaidi ya 20m .

#Akiliwa asilaumu.
 
Huwa mnalalamika situation ya biashara na hamtoi details hasa juu ya location. Unakuta mtu analalamika kitimoto hailipi unajikunja kumuelekeza kumbe jamaa yupo Unguja.

Nina kifremu naambiwa jirani kwenye godown hapa kabla sijapanga aliuza unga wa jumla alikuwa anauza sana watu wanapishana semi zinatoka Iringa uko zinajaza. Jamaa akafilisika eti watu wanajiuliza ilikuwaje, simply ni kwamba alikuwa anafanya biashara ya sifa kama wewe. Siku ukiagiza canter mvua imenyesha, likatumbukia mtoni likamwaga unga lazima uchanganyikiwe. Hasara moja inakula faida ya siku nyingi sana.

Yaani kwenye inventory ya milioni 40 unapata laki tano??? Biashara yangu ndogo sana ila nikitumia 5M huwa napata laki tano, yaani unafanya 10 times ya hela yangu na unateseka zaidi yangu ila faida tunalingana.

Nishawahi fanya research ya vyakula vya jumla kama mchele na unga, au mahindi. Kitu kikubwa kule ni uchawi, ila sio faida. Nimekaa sana Tandika nasoma wafanyabiashara na madalali nikajihakikishia ni biashara kichaa. Eti mtu ulete tani 20 za mchele upate faida milioni moja, si wehu huo. Halafu hasara ikija sasa, milioni tatu nne kawaida.

Unakuwa mfanyabiashara unaishi kwa hasira mtu akikukanyaga unampiga. Sura imekakamaa hela unazo ila hupendezi mawazo tu.
Huo mchele wenzetu mnanunua wapi.
 
Mkuu hapo awali miaka nyuma kidogo ndo ilikua faida kwa mfuko 35000 baada ya supply kuwa wengi ikaingia tabia ya ushindani Kila mtu kutaka kuuza kufikia Sasa kushusha Bei masupply wapya wanashusha Bei ili wauze sana mnajikuta mnakimbizana nao Bei hiyo hiyo ya faida 900
Chief kwa hapo nzega inaonekana utachelewa ungejaribu kuhamia sehemu yenye mzunguko zaidi kama mwanza au kahama unaweza kupiga hatua zaidi.
 
Habari wakuu mnaionaje hizi baishara ni za kuendelea kufanya kweli tandam ya gari ya sukari inabeba mifuko 600 ya sukari unaiuza kwa miezi 2 na faida yake ni 540,000 wakati huo gharama za manunuzi 46m faida kwa Kila mfuko jumla jumla ni tsh 900.

Wakati huo huo mtaji wa gari ya ngano 45m hapo gari ya ton 32 sawa na mifuko 1280 kwa Kila mfuko ukiuza jumla faida ni tsh 450 sawa jumla ya 576,000 kwa mifuko yote ambayo unaiuza kwa miezi 2.

Je, wakuu hii biashara inanichanganya sana mtaji mkuwa faida kidogo, tupeane fursa za hela ili tubadilishe biashara tupate faida anagalau inayoendana na mtaji.
Nitafute 0688954729 Njoo Mtwara wilaya ya Nanyumbu tununue ufuta na kuuza ghalani faida ya 30% mpaka 40% kwa kilo , au karanga tutanunua mashineni kuuza mwanza au dar kwenye maghala ya wachina au wahindi
 
Huwa mnalalamika situation ya biashara na hamtoi details hasa juu ya location. Unakuta mtu analalamika kitimoto hailipi unajikunja kumuelekeza kumbe jamaa yupo Unguja.

Nina kifremu naambiwa jirani kwenye godown hapa kabla sijapanga aliuza unga wa jumla alikuwa anauza sana watu wanapishana semi zinatoka Iringa uko zinajaza. Jamaa akafilisika eti watu wanajiuliza ilikuwaje, simply ni kwamba alikuwa anafanya biashara ya sifa kama wewe. Siku ukiagiza canter mvua imenyesha, likatumbukia mtoni likamwaga unga lazima uchanganyikiwe. Hasara moja inakula faida ya siku nyingi sana.

Yaani kwenye inventory ya milioni 40 unapata laki tano??? Biashara yangu ndogo sana ila nikitumia 5M huwa napata laki tano, yaani unafanya 10 times ya hela yangu na unateseka zaidi yangu ila faida tunalingana.

Nishawahi fanya research ya vyakula vya jumla kama mchele na unga, au mahindi. Kitu kikubwa kule ni uchawi, ila sio faida. Nimekaa sana Tandika nasoma wafanyabiashara na madalali nikajihakikishia ni biashara kichaa. Eti mtu ulete tani 20 za mchele upate faida milioni moja, si wehu huo. Halafu hasara ikija sasa, milioni tatu nne kawaida.

Unakuwa mfanyabiashara unaishi kwa hasira mtu akikukanyaga unampiga. Sura imekakamaa hela unazo ila hupendezi mawazo tu.
😄😄😄😄😄😄😄😄
 
Habari wakuu mnaionaje hizi baishara ni za kuendelea kufanya kweli tandam ya gari ya sukari inabeba mifuko 600 ya sukari unaiuza kwa miezi 2 na faida yake ni 540,000 wakati huo gharama za manunuzi 46m faida kwa Kila mfuko jumla jumla ni tsh 900.

Wakati huo huo mtaji wa gari ya ngano 45m hapo gari ya ton 32 sawa na mifuko 1280 kwa Kila mfuko ukiuza jumla faida ni tsh 450 sawa jumla ya 576,000 kwa mifuko yote ambayo unaiuza kwa miezi 2.

Je, wakuu hii biashara inanichanganya sana mtaji mkuwa faida kidogo, tupeane fursa za hela ili tubadilishe biashara tupate faida anagalau inayoendana na mtaji.
Ingia kwenye mazao nunua kwa mkulima uza kwa wahindi.

Utazungusha hela yako na kuoata faidi kwa muda mfupi
 
Habari wakuu mnaionaje hizi baishara ni za kuendelea kufanya kweli tandam ya gari ya sukari inabeba mifuko 600 ya sukari unaiuza kwa miezi 2 na faida yake ni 540,000 wakati huo gharama za manunuzi 46m faida kwa Kila mfuko jumla jumla ni tsh 900.

Wakati huo huo mtaji wa gari ya ngano 45m hapo gari ya ton 32 sawa na mifuko 1280 kwa Kila mfuko ukiuza jumla faida ni tsh 450 sawa jumla ya 576,000 kwa mifuko yote ambayo unaiuza kwa miezi 2.

Je, wakuu hii biashara inanichanganya sana mtaji mkuwa faida kidogo, tupeane fursa za hela ili tubadilishe biashara tupate faida anagalau inayoendana na mtaji.
Kweli penye miti hapana wajenzi

All the best mkuu
 
Back
Top Bottom