Namashaka na wewe. Wewe sio mfanya biashara. Utakuwa umesikia story vijiweni. Biashara unayozungumzia hapo ni biashara ya jumla. (Whole sale) na biashara ya jumla huwezi kuuza mifuko 600 kwa miezi miwili. Huo ni uongo kabisa.
Biashara yoyote ya jumla ina faida ndogo ila ni pesa nyingi. Dukani kunakuwa ma bidha kama hizi kwa mfano.
1. Sukari kg 50 na kg 25
2. Ngano kg 50 na kg 25
3. Mafuta ya kula lita 20 na lita 10
4. Sabuni za unga packege za ujazo tofauti
5. Sabuni za miche makampuni tofauti
6. Dawa za meno. Colgate, whitedent mls tofauti tofauti
7. Bidhaa nyingine zote zinazopatikana kwenye maduka ya rejareja almaarufu maduka ya mangi.
Sasa huyu wa duka la jumla anauza bidhaa hizi kwa wateja wa duka la reja reja. Mteja akija kwa mfano ataandiksha vitu vifuatavyo.
1. Sukari kg 50 pc 1
2. Mafuta ya kula lt 20 pc 1
3. ngano kg 50 pc 1
4. Colgate gm 250 dozan 2
5. Majani ya chai gm 125 dozani 3
6. Omo sabuni za unga catton 2
7. Sigara bomba 1 sawa packet 10 moja
8. Pipi, big G, juice, pc 10 kila moja
9. Nk.
Huyu mteja mmoja akija hapa lazima amwachie huyu jamaa wa duka la jumla wastani wa tshs 10-15k kama faida. Akiwauzia wateja 25 tu kwa siku anapata wastani wa tshs 300k +. Unasemaje hapo hakuna faida?
Wewe mleta mada hujui chochote kuhusu biashara. Biashara kwa taarifa yako ina faida ndogo lakini pesa ni nyingi.
Ukija kwa hawa wa maduka ya rejareja. Akiwa na duka la kuuza wastani wa shilingi 300k wa siku, huyu jamaa kama atakuwa msimamizi mzuri baada ya miaka miwili, my friend humgusi.
Naandika kama mzoefu kwenye hili eneo. Nimewahi kuwa na duka la rejareja na ni mzoefu kwenda kununua kwenye haya maduka ya jumla.