Mtaji wa 46M faida 540,000, pia mtaji wa 45M faida 576,000

Kwaiyo mkuu tufanye biashara gani
Huwa mnalalamika situation ya biashara na hamtoi details hasa juu ya location. Unakuta mtu analalamika kitimoto hailipi unajikunja kumuelekeza kumbe jamaa yupo Unguja.

Nina kifremu naambiwa jirani kwenye godown hapa kabla sijapanga aliuza unga wa jumla alikuwa anauza sana watu wanapishana semi zinatoka Iringa uko zinajaza. Jamaa akafilisika eti watu wanajiuliza ilikuwaje, simply ni kwamba alikuwa anafanya biashara ya sifa kama wewe. Siku ukiagiza canter mvua imenyesha, likatumbukia mtoni likamwaga unga lazima uchanganyikiwe. Hasara moja inakula faida ya siku nyingi sana.

Yaani kwenye inventory ya milioni 40 unapata laki tano??? Biashara yangu ndogo sana ila nikitumia 5M huwa napata laki tano, yaani unafanya 10 times ya hela yangu na unateseka zaidi yangu ila faida tunalingana.

Nishawahi fanya research ya vyakula vya jumla kama mchele na unga, au mahindi. Kitu kikubwa kule ni uchawi, ila sio faida. Nimekaa sana Tandika nasoma wafanyabiashara na madalali nikajihakikishia ni biashara kichaa. Eti mtu ulete tani 20 za mchele upate faida milioni moja, si wehu huo. Halafu hasara ikija sasa, milioni tatu nne kawaida.

Unakuwa mfanyabiashara unaishi kwa hasira mtu akikukanyaga unampiga. Sura imekakamaa hela unazo ila hupendezi mawazo tu.
 
Mkuu Tandika sokoni kumbe pagumu
 
Mkuu tandika sokoni kumbe pagumu
Pale wamejaa roho ngumu kama Wapemba ndio wana faida hata ukienda Malinyi uko na Kahawa wanaagiza mizigo. Ukienda wewe ukoo wenu hakuna mgomvi wala hakuna mtu aliwahi miliki jini utakuwa unaambulia hela ya kula tu. Kuna figisu nyingi, usumbufu, uswahili almost 80% ya watu pale ni la saba B. Yani tafrani tu.

Halafu kuna mtu unakuta ana godown la tani 50 ila analifungua miezi mitatu tu kati ya mwaka, na maisha yanaenda.
 
Kaka nilikuwa nataka kulipia fremu kabisa.....pale karibu na daladala za Chamazi......UNANITISHA KAKA
 
Hapo kuna guarantee ya hio Faida? Huwezi kusema hio Faida ni ndogo sababu majority ya Biashara za kibongo pasua kichwa hapo unaweza ukakuta imekula kwako.... Actually ukiweka na muda wako na kwamba unajilipa mshahara ambao hapo haujilipi ni kwamba imekula kwako....

Biashara nyingi za kibongo pasua kichwa (not sustainable)
 
Mbona kama umeenda chaka, ni wapi amesema kuwa ana gari?!! Kipindi kile cha shule kwenye history umeshusha, weee, mwalimu anakuandikia out of point!!
 
Hiyo sio biashara mkuu!! Yaani 45m upate faida hiyo?!! Wakati kuna sehemu unaifanyia biashara, hiyo pesa kwa mwezi unapata si chini ya milioni 15?!!
 
Kwenye fremu ya biashara nyingine sijui, ila kwenye godown la nafaka. Ila kama sio game changer huendi kutoa changamoto kwa magangwe sidhani kama kuna shida.
Hata kwa biashara zingine bado ni changamoto tu, kwenye biashara za soko la pamoja kama Mbagala na Tandika, lazima uwe umeaga kwenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…