CONTROLA
JF-Expert Member
- Sep 15, 2019
- 7,001
- 23,449
Katika Vitu vinapoteza watu wengi kwenye biashara ni MTAJI WA KUTOSHA.
kuna watu nawambia wana mitaji mikubwa sana ya kufungua biashara yoyote na popote pale lakini hawaangaliii wala kuwaza yatakayojiri kwenye hizo biashara mambo yakigeuka.
Kuna
Uwezo kipesa na
Kuna Ujuzi Wa kitu
Katika biashara zinazokufa sio wote zinakufa sababu mitaji imeyumba
Hujawahi kuona mtu biashara imekufa lakini anaendelea kula maisha vizuri tu,bata always,matanuzi kama kawaida ila Frem imemshinda kaiachia...
Sasa hao ndio ninao waongelea hapa, Hawa ni wale watu wenye pesa wao nawaonaga kama sio wafanyabiashara...
Maana mfanyabiashara lazima ujue kuangalia na kutathmini biashara yako miaka miwili mbele,3,nk
hawa watu wao hilo hawana, maana wana upofu wa PESA.
MFANO :
Usifungue Biashara ya Kutoa Huduma kama wewe binafsi Huwezi chochote katika huduma zitolewazo ofisini kwako...
Biashara za kutoa Huduma ni kama
USAFI
UFUAJI
UPIKAJI
SALOON (KIKE/KIUME)
USAFIRISHAJI,nk
Zipo Nyingi sana
Sasa kuna Mtu ana pesa/mtaji anataka fungua Moja wapo ya hizo Biashara..
Tuchukulie Mfano SALUNI YA KIKE
mtu kafungua Saluni ya kike, Yeye hajui chochote kwenye saluni hajui kusuka,kufanya chochote kile hajui
Anawategemea wafanyakazi (pesa anayo ya kuajiri yeyote)
Hii ni HATARI SANA na katika watu 100 wanaofanikiwa ni watu 10 tu kuendeleza hizi biashara za hivi.
Na hawa wanaofanikiwa ni wale wana mifereji mingine mingi ya kupatia pesa...
Mfanyakazi ni mzuri sana Mwanzoni maana hamjuani anataka kazi Na wewe unataka ofisi ifunguliwe
ila amini nakwambia mfanyakazi huyu hatokua mzuri kwako milele
itafika mahali atataka kuacha kazi,atataka kufanya mambo yake
Je utafanyaje?
Umeshawahi kujua nini chakufanya ikitokea wafanyakazi wako wote wamekugomea kufanya kazi/kuja kazini?
Atleast hata ungekua unajua huduma unazotoa ingekua rahisi kwako kuendelea pale wanapoachia wafanyakazi wako huku ukiendelea Tafuta wengine.
Hii maswala ya Kusimamisha huduma kisa wafanyakazi ya kuiangalia sana unapotaka kuwekeza hela yako sehemu flani
Unapokua na hela yako usifate sana wale wanaokwambia Fungua kitu unachokipenda..
Wakati mwingine unaweza penda kitu usichokua na ujuzi nacho, sio sawa.
Heri ujifunze kwanza kuhusu hicho kitu ajiriwa (maana kuajiriwa sio dhambi) pata uzoefu ukishajua kinafanywa vipi FUNGUA HUDUMA.
Kuwa.mmoja wa team yako ya kazi, Epuka Kuwa BOSS wakati ndio ofisi yako ya kwanza.
Ukiona umefungua ofisi na hufanyi kitu kwenye ofisi kila kitu wanafanya wafanyakazi jiangalie sana hautodumu na hiyo biashara kuna muda itakataaa Tu.
na Ubaya wa hizi biashara za kutoa Huduma Wateja hujenga mazoea na watoa huduma (ambao ni wafanyakazi wako) na wateja hao hao wanaweza kukuchukulia wafanyakazi wako Je umeshawaza Ikitokea siku Mfanyakazi wako BORA akakuacha OFISI itaendelea au itakufa? (Jibu unalo)
Mtaji una mahala pake lakini Biashara zote zinazohitaji Uzoefu/Skills hakikisha Unajua kwanza wewe BOSS ndipo unaajiri.
Kama usafirishaji Anza kwanza mwenyewe kushika usukani
Kama Mama Ntilie Anza kwanza mwenyewe kupika vyakula vitamu
Kama ni Usafi Majumbani Anza mwenyewe kwenda kwa wateja kusafisha maeneo yao
Wewe kwanza kisha ndio Wafanyakazi...
Wewe ndio Ulieshikilia Biashara yako,
Wewe ndio MTAJI wa kwanza kisha Pesa inafata.