Mtaji wa milioni moja, naomba wazo la biashara

Mtaji wa milioni moja, naomba wazo la biashara

Daniel Adrian

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Posts
311
Reaction score
326
Habari zenu jamani.

Kwanza nikiri kwamba naandika post hii huku kichwa kinaniuma. Toka nimepata hii pesa (600k nimeuza mali, 400k nimekopa) nimeumiza sana kichwa biashara gani ntafanya ili niendeshe maisha?

Kiukweli sitafuti faida ya haraka haraka, nataka tu nipate chochote ili nilipe kodi na kum-support mzazi mwenzangu maana nimesota sana baada ya kupoteza kazi.

Niliwaza biashara hizi (zifuatazo) lakini nikaacha hayo mawazo kwa sababu zifuatazo.
Saloon - flemu, vifaa, furniture. Nikaona pesa haitoshi.
Mobile money - flemu, leseni, float. Pesa haitoshi.
Mgahawa - flemu, (viti na meza), vyombo. Na nikizangatia hakuna biashara inayolipa ndani ya siku chache za mwanzo nikaona pesa haitoshi. Nitakula msingi.


Biashara ambayo naiwaza sasa hivi ni kunnua simu, hata nikianza na tatu kisha niziuze tu mtaani. Kama kuna mtu ashawai fanya hivi naomba mawazo yenu. Na risk zake ni zipi ?

Lakini kama idea yangu si nzuri, naombeni mnishauri idea nzuri maana kichwa kinauma sana.
 
Kwa simu itakuuwa na mawazo tena kama upo Dar. Then kwa biashara ya simu sijui utauza bei kwani upate faida wakati mtu akishakuona na simu mkononi anajuwa used bei inashuka.

Nakupa wazo mkuu, fungua biashara ya vipodozi uswahilini, chukua frame lipa miezi 4 lakini 2 chukua laki 4 ingia kariakoo chukuwa zaga kama zote njoo weka.

Kama utakuta frame ina shelf itakuwa poa sana ila kama hamna tumia laki mbili ya matengenezo then laki moja fanya nauli na chai ukisikilizia mchongo mwaisa.

Pia ukikaa vizuri m1 kwa vipodozi ni mtaji mkubwa sana aisee. Achana na mambo ya leseni ,TRA sijui nini fanya kigumu usifate protocol sana.

Hii biashara ina faida sana hela ya mtaji kwa kipodozi unaweza ukaingiza faida kama ulowekeza.

Ngoja niishie hapa
 
Kwa simu itakuuwa na mawazo tena kama upo Dar. Then kwa biashara ya simu sijui utauza bei kwani upate faida wakati mtu akishakuona na simu mkononi anajuwa ised bei inashuka.

Nakupa wazo mkuu, fungua niashara ya vipodozi uswahilini, chukua frame lipa miezi 4 lakini 2 chukua laki 4 ingia kariakoo chukuwa zaga kama zote njoo weka.

Kama utakuta frame ina shelf itakuwa poa sana ila kama hamna tumia laki mbili ya matengenezo then laki moja fanya nauli na chai ukisikilizia mchongo mwaisa.

Pia ukikaa vizuri m1 kwa vipodozi ni mtaji mkubwa san aisee. Achana na mambo ya leseni ,TRA sijui nini fanya kigumu usifate protocol sana.

Hii biasharaina faida sana hela ya mtaji kwa kipofozi unaweza ukaingiza faida kama ulowekeza.

Ngoja niishie hapa
Kaka nakushukuru sana kwa kunipa hili wazo.
 
Kila kitu mkuu hata ukipata gari fresh tu maana ake mchanganyiko, radio, tv, pasi, meza, vitanda etc
 
Back
Top Bottom