Kama niliweza hata hivyo visentensi vichache, shida iko wapi? Kwani kiswahli ulikuwa unapata mia? Mimi ni mkatoliki, sala zote ya kikatoliki niliweza kwa kiswahili nikiwa primary. Nilikuwa nahudhuria ibada za kiingereza hapa Nairobi na Arusha. Ni juhudi binafsi zitakusaidia. Halafu wewe huwezi kuwa mwalimu, kama utamdharau mwanafunzi wako na kumwambia vijisentensi. Kuomba maji kwa kiingereza ukiwa primary ni mtihani tosha. Hebu pitia mada yako na uweze kuitathmini kama mchangiaji alivyotaka iwe kwa mfumo mwingine.