Mtalaka wa Sugu azuiwa kuingia ofisi za RITA

Mtalaka wa Sugu azuiwa kuingia ofisi za RITA

View attachment 668359 Mtalaka wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi "Sugu", Faiza Ally alijikuta akizuiwa kuingia katika ofisi za RITA jijini Dar es Salaam kutokana na kuvaa mavazi yasiyo na staha.

Askari waliokuwepo ofisi za RITA walimtaka Faiza Ally akabadili vazi na kuvaa linalostahili kuvaliwa katika ofisi ya umma. Baada ya mvutano, alijitokeza msamaria aliyemuazima mtandio ambao alivaa na ndipo aliporuhusiwa kuingia ofisini ili kutimiziwa shida iliyompeleka.
Leo namtetea jaman sasa hapo ubaya wa hilo gauni ni nini mbona kavaa vizur kabisa tena la kwendea ukwen
 
Sketi gani sasa hapo? Faiza hajavaa sketi. Mwenyesketi iliyobinuka na kuacha magoti nje ni yule polisi. Shria ya ofisi za uma kwa wafanyakazi wa uma, na si wageni!
Kwenye ofisi za Umma haijalishi we ni mfanyakazi au lah lakini wanataka nguo ivuke magoti.Pia Huwa wanataka mikono iwe imesitiriwa.Ukivaa zile zenye vikamba vya kuning'iniza hupiti getini.
 
Mmmh leo wamemuonea mbona gauni halina shida hilo,nahisi ni kwa vile wamezoea kumwona na vivazi vya nusu uchi
 
Hivi Hawa Askari wetu wanapewa muda wa mazoezi ya ukakamavu kweli, maana mama kaenea skirt iko chini ya kitomvu.
 
Huyo mwenye tumbo.
Huyo askari yuko vzr sana ipo sehemu faiza alikosea sio nguo tu,hasingeweza kumzuia maana hata utawara waliwakataza kuwapangia wateja nguo za kuvaa labda uwe mtumishi mle ndani ndio utarudishwa ukabadili.wateja wengi wanaingia na nguo za ajabu ajabu na hawajawai kuzuiliwa hata siku moja IPO tu walipokwazana akaona amkomalie kwenye nguo.
 
Back
Top Bottom