Transistor
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 1,061
- 1,637
Katika harakati za kijasiliamali mtambo huu unaweza kuwa tija kwa wajasiliamali.
Mtambo huu umeundwa maalumu kwa ajili ya kuendesha mashine ya kawaida ya kunyolea ambayo inatumika katika ofisi za kunyolea.
Mtambo huu una uwezo wa kubebeka na kusafirishika kirahisi kwasababu una uzito wa kawaida lakini pia unaweza kuficha panel zake za solar na kuzitoa.
Unaweza ukamyajiri kijana au ukakodisha mtambo huu kwasababu umefungwa kifaa kinachosoma matumizi (UNIT za umeme zinazo tumika).Hivyo ni rahisi kufanya makubaliano ya malipo na mtu uliye mwajili au kumkodisha.
Kinyozi anaweza kwenda maeneo ya vijijini na kufanya shughuri yake ya kunyoa katika maeneo yenye mikusanyiko mfano shule,munada,vilabu n.k
Pia mtambo huu unaweza ukatumika kama mbadala wa generator kipindi umeme umekatika uzuri ni kwamba hakuna gharama za ziada kwenye kuiendesha kama ilivyo kwa generator.