Mwanza haina abiria wengi wanaoweza kusababisha kujengwa international airport. Hakuna shughuli za kimataifa kama Arusha, Dar, Dodoma. Mnataka international airport ya nini?
Kwa maoni yako haya ni kwamba Mwanza hata kama haina vitu hivyo leo, itakuwa hainavyo miaka yote?
Angalia uwingi wa watu. Hao unaowaona leo hawawezi kupanda ndege, ni hao hao miaka kumi ijayo watakuwa wanapigana vibega kutumia usafiri huo.
Palipo na uwingi wa watu, shughuli zote hizo ulizotaja wewe ni lazima ziwepo
Kwanza kimandhari tu, huwezi kulinganisha Arusha kwa njia yoyote na Mwanza.
Pengine kwa vile huna 'exposure' na miji mingi duniani, ndiyo maana unashindwa kujuwa maana ya uwanja wa kimataifa ni nini.
Chukulia uwanja wa Kimataifa wa Hartfield-Jackson, kwa mfano uliopo Atlanta Georgia; uwanja ambao ni wa pili (nadhani) duniani kwa wingi wa wasafiri kwa ndege duniani. Hapo Atlanta hakuna vivutio vya utalii unavyodai wewe; lakini mahali ulipo uwanja huo ni sehemu muhimu inayounganisha wasafiri toka maeneo mbalimbali duniani.
Kwa mahali ilipo Mwanza katika bara la Afrika, hata hiyo Hartfield-Jackson haiwezi kuwa na 'potential' iliyonayo Mwanza.
Kwani shughuli za Kimataifa ni nini? Si ni kuwa na kumbi tu za kutosha na hotel nzuri? Unategemea hayo yote yawepo hata bila kuwepo kwa uwanja kwanza?
Kigali kuna nini, mbona mikutano ya kimataifa mingi tu inafanyika huko?
Ni hivi, unayo hofu kubwa sana juu ya 'potential' iliyo nayo Mwanza, kiasi kwamba hofu yako inakupofusha na kudhani kukua kwa Mwanza kutaiua Arusha. Na bila shaka, hata huko kwenye wafanya maamuzi serikalini hofu hii ndiyo inayofanya pawepo na mizengwe mingi juu ya mji huu wa Mwanza. Mizengwe hii haiwezi kuizuia Mwanza kuchukua hadhi yake katika majiji bora kabisa duniani.