Kwa hiyo, kwa uelewa wako, Chato ndio mfano halisi wa kuilinganisha na Mwanza! Mbona unajivisha ujuha waziwazi hivi?
"Watalii wa Zanzibar" wakiondokea Dar es Salaam hawafiki ulaya? Wanaotua Nairobi na kwenda mahala kwingine hawatoki na kufika Ulaya?
Umekwisha ambiwa mara kadhaa humu, kwamba viwanja vya ndege havipo kwa ajili ya utalii pekee, lakini wewe hilo ndilo jambo pekee unalolishikilia, kwa sababu hujui mengine yote.
Nilikupa mfano mmoja wa kule Marekani, uwanja wenye wasafiri wengi zaidi duniani, uliopo Atlanta, Georgia, Hartfield-Jackson, Georgia kuna utalii gani huko, unajua?
Ukweli ni kwamba huna unalojuwa katika maswala haya ya usafiri wa ndege, kinachokuumiza tu roho ni kudhani kwamba uwepo wa Mwanza utaiondolea au ipunguzia sifa Arusha. Lakini ukweli ni kwamba, wewe, pamoja na wengine wote waliokuwa na mategemeo ya kuifanya Mwanza kutotumia nafasi yake kikamilifu, matumaini yenu hayo hayaendi popote. Mwanza itashamiri na itachukuwa nafasi yake katika miji mashuhuri, siyo hapa Tanzania pekee, bali duniani kote.
Hili halizuiliki kwa hila zozote.