Mtandao wa Halotel wameniibia

Mtandao wa Halotel wameniibia

Wernery G Kapinga

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2012
Posts
376
Reaction score
127
Bila shaka mpo vizuri

Tarehe 15 nililipia king'amuzi kupitia mtandao wa Halotel. Cha ajabu sikurudishiwa ujumbe na pesa kwenye account imeondolewa.

Nikapiga simu huduma kwa wateja. Wa kwanza akaniambia system iko chini kwa hiyo itakuwa accessed baada ya muda wa dk 20 mpaka 30. Siku ikapita holaa.

Nikapiga simu siku ya pili asubui, akaniambia pesa iko pending na Kama huduma haitapatikana ndani ya masaa 24, basi pesa itarudishwa kwenye account. Masaaa husika yakapita hola.

Nikapiga simu baada ya masaa 24, mhudumu akaniambia atatuma taarifa makao makuu kwa ajili ya kurudisha muamala. Akaniambia nisubiri masaa 6-12. Mpaka Sasa hola. Nimepiga tena simu saizi wananiambia inatakiwa nisubiri masaa 72. NIMECHOKA.

HALOTEL wameshanitapeli. Nafikiria kwenda kuwashtaki. Jaman msaada wenu wa pakuanzia. Je, niende kwanza polisi ama? Kuna namna nyingine ya kufungua kesi dhidi ya makampuni ya simu?

Naomba kuwasilisha.
 
Hali kama hii Iliwahi kunitokea, Nimelipa Azam Kifurushi Cha 13000 Nashangaa Channel Azioneshi, Niliwapigia Simu Tigo Walinikoma Wenyewe Walirudisha Hela Baada ya Siku.
 
Nilinunua kifurushi cha 5000 Airtel M, wakaniambia sijui nn. Jaribu baadae.

Nmekaa nusu saa, nikajaribu tena. Ikakubali

Mara paaa meseji mbili zote za kununua vifurushi kwa 5000 yaan jumla 10000

Kuchek salio, kweli bana wamekata 10000

Nikawapandia hewan, Jamaa yule akaanza maneno maneno

Nilimtapikiaa matusii, akaniuliza, una shida nyingine tukusaidie?? Nikatapika matusi

Nilipokata simu, muamla mmoja wa 5000 ,ukarudishwa .
 
Wafate ofisi yao kuu ya HaloPesa,, watakushughulikia chap
ila wana tatizo la kimfumo nimefuatilia hela yangu miezi minne ukipiga wanakuambia itarejea baada ya saa72 na zikiisha wanaongeza tena 72 sijui wana tatizo gani
 
ila wana tatizo la kimfumo nimefuatilia hela yangu miezi minne ukipiga wanakuambia itarejea baada ya saa72 na zikiisha wanaongeza tena 72 sijui wana tatizo gani
Ukipiga simu ndo wanakuzungusha.... Wafuate ofisini kwao kule bamaga watakushughulikia..

Ninaongea kwa uzoefu... Pesa yangu walikaa nayo siku nyingi tu wananizungusha... Nilipoenda ofisini kwao, pesa ilirudi ndani ya dakika 10 tu.
 
Mimi Nisha wahi kuibiwa Hela ya Luku na nilipiga simu haikupokelewa kabisa halotel ni wezi wazuri tu
 
Back
Top Bottom