Niwaambieni hivi. Juhudi za Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwepo toka kabla ya Nyerere wakati AA ikiendesha shughuli zake kote bara na Visiwani. Cecil Matola na Mzee Kreist Sykes wakiongoza makao Makuu Dar kwa sababu Mtawala wa kote alikuwa Muingereza. Sultan alikuwa kama King Charles wa Uingereza.
Kwa hiyo, hata zilipoanza harakati za Uhuru AA ya Zanzibar walishirikisha watu kutoka bara kutaka kuunda Chama chao, jina sikumbuki lakini Mzee Sapi alitakiwa kuwa nwenyeji hakuweza kufika maana alikuwa kenda Uingereza.
Kulikuwepo mshirikiano mkubwa baina ya bara na Visiwani kichama asiwadanganye mtu isipokuwa walilazimika kufanya hivyo kwa sababu tayari Muingereza alishamtambua Sultan na kumpa ulinzi wakati Bara amekabidhiwa na UN.
Sidhani kama Seyyid Said aliwahi kutawala pwani yote ya Bara. Alikuwa na makubaliano na baadhi ya city states kama Kilwa, Malindi, Mikindani n.k. Hakuna chief yeyote wa makabila ya pwani aliyemhesabu Sultan kama mtawala wake na hivyo kumpelekea mapato. Kuheshimiwa kwa hao mawalii hakukuwa na maana ya kuwa alikuwa anawatawala. Mawalii walikuwa wawakilishi wake. Ndio maana ilikuwa hata wakitaka kupitisha bidhaa zao (ikiwa pamoja na watumwa) katika sehemu nyingi walikuwa wanatozwa ushuru. Tanganyika wangedaije Zanzibar wakati haikuwa kuwa sehemu yake? Kale kakanda ambacho Sultan alidai kuwa ni chake (kuzunguka Dar es Salaam) kilipeewa wajerumani 1890 kwenye mkataba wa Heligoland-Zanzibar.
African Association hakikuanzishwa kwa ajili ya siasa. Kilikuwa ni chama cha burdani na kijamii. Kwa sababu hiyo sio ajabu kuwa na matawi Zanzibar ambako kulikuwepo wengi wenye asili ya Tanganyika.
Hauwezi kufananisha miji na nchi. Mimi sijawahi kukutana na raia wa Marekani ambae alijitambulisha kama New Yorker, au hata Texan. Wote nje ya mipaka yao wanajitambulisha kama wamarekani. Hii ni tofauti na wazanzibari ambao wako wanaojitambulisha kama wazanzibari na sio watanzania. Hatuwezi kulazimisha identity.Watanganyika tukiwa kwetu tunajitambulisha kama wakerewe, wachaga, watanganyikan.k. lakini nje ya mipaka yetu bado tunajitambulisha kama watanzania. Hamna ubaya katika hili.
Amandla...
Mkuu umasema kitu gani hapa. Seyyid Said alitawala pwani yote ya Bara kumbuka kwamba Sayyid alikuja kabla ya Mjarumani na Muingereza. Yaani toka pwani Mogadishu hadi mpaka wa Msumbiji baada ya kumondoa Mreno.
Na Mreno pia aliuondoa utawala wa Shiraz ambao alitawala eneo hilo hilo na Msimbiji likiitwa AZANIA. Naomba google ama isome historia yetu kwa watangulizi wetu kwa sababu hata Tippu Tip alikuwa Sultan kule DRC.
Sii kweli kwamba AA kilikuwa chama cha Starehe maana Waanzilishi wake walikuwa Wafanyakazi Bandarini, Mabaharia, Watumishi wa Serikali ya Mkoloni.
AA kilichokuwa chama labda niseme UNION kutetea haki za Wafanyakazi. Lakini watu hao hao (baadhi) baadae ndio walokuja kubadilisha mwelekeo wa chama kuwa chama cha Siasa.
Watu wengi wanasema kuwa kilikuwa kijiwe cha starehe kwa sababu kina Sykes walikuwa Wanamuziki na hivyo kuchukulia kwamba AA na TAA vilikuwa vyama vya starehe laa hasha. Toka AA kwenda TAA hadi TANU ilikuwa tu kubadilisha jina kulingana na malengo. Hata AA kuwa ASP ilikuwa na malengo yake. Leo tuna CCM kwa sababu zake. Naweza sema CCM haikupigania Uhuru, kweli kabisa lakini mwenye kuelewa anajua tunazungumzia TANU na ASP.
Hoja ya Wazanzibar, hii imekuja kutokana na muundo wa Serikali tu lakini haipunguzi kitu kwetu. Tena naweza sema Zanzibar wana haki ya kulalamika maana mzigo wote wanaubeba wao kwa kuitaka Zanzibar. Sisi Bara, Bunge Moja la JMT linaendesha ya Mambo ya Muungano na 99% mambo ya Bara. Tumeua ndege wawili kwa jiwe moja wakati Zanzibar inawa cost big time kulipa viongozi wote ambao ni kama wajumbe wa nyumba 10 kwa eneo la mraba.
Tulitakiwa kuwa na nchi MOJA tu. Hapi tunepunguza mabaraza yote ya Zanzibar wakashiriki mabaraza ya JMT kuondosha gharama za ma VX, mafuta, posho. Viongozi wa Zanzibar wanaitaka Tanganyika ili nasi tusikie machungu yao. Na pengine sababu isije tokea tukaunda Tanzania MOJA wakakosa nafasi hizi za ULAJI..