Ulosema yote nakuelewa na nakubali nawe lakini kilichokosekana hapo nini? jina tu la Tanganyika ulopewa na mkoloni ndio unalilia. Sasa ndugu yangu wewe utakula jina? Kuwa na jina Tanganyika utafaidika na kipi au fahari ya macho! maana unapoomba kitu ujue faida na hasara zake.
Jina tu la Tanganyika kweli au kuna jingine? Kwani tukiitwa Tanzania Bara (Tanzania Mainland) kinapungua kitu gani? Acha wao wajiite Zanzibar sijui Wazanzibar ni fahari kwao lakini inawagharimu. Kwangu mimi hiyo ni Tanzania Visiwani, Zanzibar ni mji.
Kuwa na rais wanamlipa, baraza la Wawakilishi wanalipwa na kodi zao kifupi Serikali nzima inalipwa na wananchi wakati Ofisi moja ingeweza kuhudumia Bara na Visiwani. Mzee Karume akiwa Makamu wa rais alifanya mambo mengi makubwa kuliko hawa viongozi wote waliofuatia.
Cancer ya Mwafrika ni fikra za Ukabila na Udini tu. Unakuta tunapugania kwa nini Mawaziri wengi Wakristu! Je anapokuwa Muislaam anawasaidiaje Waislaam? Mimi sijaona iwe, Mwinyi Kikwete au Mama Samia na Mawaziri wote wanafanya kazi ya Chama na sii kabila wala dini.
Hata hivyo viti maalum kwa Wanawake ni Ujinga mtupu ikiwa wanawake hao hawahusiki na maswala ya Wanawake.
Kwangu mimi Tanganyika ni uzao wa MKOLONI yaani nchi ilogawanywa kwa mfumo wa divide and rule tukazipoteza Rwanda na Burundi. Leo hii tuna wakimbizi wengi kutoka Burundi na Rwanda raia wa Tanzania tofauti yetu ni mipaka tu.
Siku tutakuwa na Tanganyika, basi ujue hatutakuwa salama kesho. Mikoa ya kanda ya Ziwa Geita na Mara watajitoa kwa sababu dhahabu yao inachukuliwa kwa jina la Tanzania na Tanganyika.
Mtwara nao watadai Gas yao kwa sababu fikra ni zile Ile kugawana URITHI kwa kisingizio cha NCHI
Kumbuka tu kabla ya Mjarumani hatukuwa na Tanganyika. Bara iliongozwa na Machief wake ambao mpaka kesho wanataka watambuliwe. Libya leo hii Machief ndio viongozi mbali na Serikali ilosimikwa. Ugonvi hauishi kwa sababu ya Mafuta..
Tumepewe na wakoloni kivipi una maana wao ndio waanzilishi kabisa kabisa wa Jina Tanganyika? Ninachojua Mimi Walipotugawanya Afrika kwa % kubwa walikuta majina yapo.
Taabu au shida ilijitokeza kwa wazungu ilikuwa Ni kushindwa kutamka majina Kama walivyoambiwa na BABU ZETU:;
Mfano:-
Idodomia wao waksema Dodoma.
Masingida wao waksema Singida
Tararangir wao waksema Tarangire
Kilimanjaro,Arusha,Babati na mengine yalivyopatikana yametokea kwa kutofautiana matamshi.
Tuna mfano mwingine Jinsi Kijiji Cha KOLOMIJE mahali alipotokea MKUU wa Mkoa mstaafu - Makonda,Wasukuma walishindwa kutaja ipasavyo Jina la Mzungu aitwaye JONATHAN akawarahisishia kwa kuwaambia CALL ME J akijaribu kuwarahisishia namna ya kumwita bado wao ndio wakakorofa zaidi Badala ya kumwita J wakasema COLOMIJE [Call me J)
Utambulisho wetu Kama TAIFA HALISI na halali lililopata Uhuru mwaka Dec.9, 1961 Ni wa Jina lipi Sasa.
Kwanini utambulisho huo unatumika kwa TANZANIA ambayo imezaliwa kwa Muungano wa NCHI mbili - TANGANYIKA na ZANZIBAR 1964?
Kuna ujanja,Hila na upotoshaji wa namna tumeadhimisha Sherehe za Uhuru.Pia haijakaa sawa,Zanzibar wao wanasherehe yao ya Kupata Uhuru wao,AMRI JESHI MKUU anaufyata kwenye protocal hii Ni aibu haijakaa sawa kabisa.
Wengine tuliosoma Siasa while ya msingi tunaweza tusiwe na shida Sana lakini kizazi kisicho mjua NYERERE na KARUME.
Kizazi Cha instant coffee hawana subira,ninyi walafi madaraka na wapiga MADEAL kitawahukumu Asubuhi Kama so Mchana kweupe.
Msiliingize TAIFA kwenye majanga na uumwagaji wa damu usio wa Lazima.
Nini kinawashida kutengekeza HATA KATIBA MPYA ILI TUACHE WATOTO NA WATOTO WA WATOTO WETU KATIKA MIKONO SALAMA KWENYE KATIKA ISIYEMPENDELEA YEYOTE?
KATIBA iliopo inatoa mwanya wa kuiba chochote, iwe RASILIMALI, KURA NA MPAKA HATA MKE WA MTU na bado ukipita mtaani bado utaitwa mheshiwa.
Mnaipendea wapi TANZANIA?
Mpaka leo mikataba ya Hila Kama ya wakoloni wakizungu na waarabu walivyowafanyia BABU ZETU ndio bado IMESHAMIRI IKULU KWA SERIKALI YETU???
INAKERAAA SANAAAA!!??