Mtangazaji Clouds TV afukuzwa kwa kutangaza habari za Tundu Lisu

Mtangazaji Clouds TV afukuzwa kwa kutangaza habari za Tundu Lisu

Huyo Mange wenu naye ni hopeless tu, anajazwaga kwenye kumi na nane naye anaingia tu fwaa.
 
Duuu kumbe Da Mange kasema basi ni marufuku kupinga .... sasa wote tuseme ni kweli kabisa Hassan kasimamishwa kazi....asitokee mtu wa kumpinga Da MANGE maana yeye ndio huongea ukweli kwa kila jambo.........
Leta kanusho kwakuleta udhibitisho unaoonyesha Hasan Ngoma bado anaendesha kipindi kama kawaida ili watu wawe upande wako wewe mpingaji.
 
Mlitaka vyombo vyake vya habari vifungiwe?? Heri mmoja kufukuzwa kuliko 10 kupoteza ajira

Nilijitahidi sana humu kumsema na kumkemea Hassan Ngoma hasa juu ya aina yake ya ' Utangazaji ' wa ' Kinafiki ' wa kuuma na kupuliza lakini kuna walioniona nilikuwa pengine nina chuki nae binafsi sasa yamemkuta. Pole yake kubwa sana na nimtakie tu maisha mema katika safari yake mpya ya maisha mapya. Sasa kwa Kipindi hiki Mwanadada Babie Kabae ( Brand Manager wa 360 Power Breakfast ) yupo Ziarani China Kipindi kitakuwa chini ya Ceaser, Masoud na Sam Nathaniel Sasali ila akirejea mwenye Kipindi chake Babie atabakia Masoud na Sam huku Ceaser akirejea zake katika Clouds fm Power breakfast. Kwa kukiwekea zaidi mvuto Kipindi hicho Masoud Kipanya sasa ataziba nafasi ya Hassan Ngoma kama vile ambavyo wengi wetu hapo nyuma baada ya Mtangazaji Hudson Kamoga kuondoka baada ya Kuteuliwa na JPM tulipenda na kushauri sana Ruge amuweke hapo Masoud Kipanya mara ghafla tukashangaa ametuletea Hassan Ngoma ambaye hata hivyo kwa wenye ' maono ' makali tulijua tu mapema kwamba kuna siku angeharibu na kweli imetokea.

Maelezo mengi ya kuhusu mabadiliko hayo ya Watangazaji sijayatoa akilini mwangu bali nimepata kutoka kwa Source wangu mkubwa aliyepo hapo hapo ' Mjengoni ' CMG na mwenye ' influence ' kubwa sana na ' Mabosi ' wakuu. Nimalizie tu kwa kusema tena kwamba pole sana Hassan Ngoma japo kwa mujibu wa huyu ' Source ' amesema kwamba tokea juzi, jana mpaka hivi leo Wafanyakazi wenzake akina Babie Kabae na Sam Sasali wanahangaika na kupambana kumuombea msamaha kwa Boss Ruge ili amsamehe kama ambavyo pia Watangazaji wa Kipindi cha Michezo akina Shaffih Dauda, Edgar Kibwana, Yahya Njenge na Issa Maeda walivyomuombea msamaha Mtangazaji mwenzao Alex Luambano na kweli Ruge akamsamehe japo alipewa onyo kali.

Hata hivyo kwa aina ya ' ushawishi ' mkubwa alionao Mtangazaji Babie Kabae kwa ' Mabosi ' zake kuna uwezekano Hassan Ngoma akasamehewa na kupewa ' onyo ' kali na tukaendelea kumuona wiki ijayo japo mpaka hivi sasa ratiba ya Kipindi cha Jumatatu ijayo tarehe 23 October 2017 inasema kwamba siku hiyo Kipindi kitaongozwa na Mtangazaji ' Deiwaka ' Ceaser. Moja ya sababu kubwa za wanaomtetea Hassan Ngoma wenzake akina Babie Kabae na Sam Sasali ni kwamba wanadai Hassan Ngoma ni Mchambuzi mzuri, ana exposure kubwa na pia ana uwezo mkubwa wa kushawishi na kwamba amewasaidia mno katika kukifanya Kipindi cha 360 Clouds tv kwa sasa kiwe juu, kikubalike na kiheshimike pia na Watazamaji.

Ni hayo tu kwa mchana huu ila nikipenyezewa zingine za ' moto moto ' juu ya suala hili la Hassan Ngoma na CMG nitawajuza bila hiyana wala uchoyo ila kwa sasa kwa mujibu wa ' source ' wangu hayo ndiyo aliyonidokezea. Kuna siku nilisema humu kwamba ukiona GENTAMYCINE anakusema sana jua una ' tatizo ' mahala hivyo jitathmini na jirekebishe upesi lakini pia ukiona ninakusifia kila mara jua ya kwamba kiukweli upo vizuri na endelea kufanya vyema hivyo hivyo.
 
Sio kweli hajafukuzwa ni uzushi tu samsasali anasema atakuwepo jumatatu na waziri wa viwanda

Katumia tu lugha ya Kidiplomasia kukuambia hivyo Mkuu. Ukiona amerudi hiyo Jumatatu kama ulivyoambiwa basi jua pengine ule msamaha alioombewa na Wenzake ( Sam Sasali) nae akiwemo basi umekubalika na Boss Ruge. Kitakachomsaidia tu Hassan Ngoma kurudi hapo ni kwasababu yupo karibu sana na Babie Kabae ambaye ndiyo Mtangazaji mwenye ' ushawishi ' mkubwa sana kwa Mabosi wote na Management nzima ya CMG kutokana tu na sababu moja ' Nyeti ' ambayo kwa sasa nisingependa kuiweka hadharani na naomba niishie tu hapa tafadhali.
 
Acha uzwazwa kapigwa stop tokea majuzi yamebumburuka sababu yakupigwa stop ni kudiscuss issue ya lisu while wamekatazwa watu wamemblast ruge na clouds ndo uyo Sam akajilete na iyo news kufunika what happened

Safi sana Mkuu kwani umemaliza kila kitu na kama ' Jamaa ' bado hajakuelewa basi ana matatizo. Umesema ukweli wote kama ulivyo. Heko mno!
 
Katumia tu lugha ya Kidiplomasia kukuambia hivyo Mkuu. Ukiona amerudi hiyo Jumatatu kama ulivyoambiwa basi jua pengine ule msamaha alioombewa na Wenzake ( Sam Sasali) nae akiwemo basi umekubalika na Boss Ruge. Kitakachomsaidia tu Hassan Ngoma kurudi hapo ni kwasababu yupo karibu sana na Babie Kabae ambaye ndiyo Mtangazaji mwenye ' ushawishi ' mkubwa sana kwa Mabosi wote na Management nzima ya CMG kutokana tu na sababu moja ' Nyeti ' ambayo kwa sasa nisingependa kuiweka hadharani na naomba niishie tu hapa tafadhali.
sababu ya kibaiolojia au sio
 
Back
Top Bottom