Mtangazaji Masoud Masoud wa TBC

Mtangazaji Masoud Masoud wa TBC

Huyu Mzee anajua sana. Anaonesha ukongwe wake katika utangazaji. Kuna mwingine mtangazaji wa zamani alikuwa anaitwa Mikidadi Mahmoud sijui yupo wapi siku hizi.!
Kuna kipindi alikuwa mkurugezi wa Radio Uhuru.
 
Nampenda sana huyu kijana wa zamani,
Anajiamini, anajielewa anachofanya na anashikilia msimamo wake thabiti,
Alinifurahisha sana kwenye kipindi cha Mkasi, alifunguka vizuri bila kusita sita.
 
Masoud hata sauti yake ni murua kuisikiliza, kwa hakika ni mtangazaji mahiri na anafuata aina ya maisha ya wazee wa zamani kama alivyo, huwezi kumuona anahamahama vituo vya radio.
Acha Urongo huyu Alikuwepo Radio One na Sasa yupo TBC nini unazungumza wewe au ndio zile zilizoimbwa sifa za kijinga
 
Napenda sana country na blues music. Huyu nae yuko so much interested na the same music. Anaweza kutunga simulizi hapa kwa kuunganisha nyimbo mbali mbali na hadithi ikawa super. Zamani nilikuwa nasikiliza kipindi chake RTD alikuwa anakiita "Simulizi ya mwana Kisiwa" (sikumbuki vizuri ). Ilikuwa ikifika saa nne usiku Jumapili lazima nisikilize hicho kipindi ndipo nilale.
 
Wanamwita manju wa muziki. Huyu ni mtangazaji mkongwe na nguli wa maswala ya muziki na wanamziki, kupitia TBC.

Ukimsikiliza Masoud, utaelewa umuhimu wa specialization katika utangazaji, uandaaji vipindi na uandishi habari kwa ujumla.

Masoud anaelewa ni nini anachofanya na kwa muktadha muafaka.

Ukifuatia simulizi zake kimuziki sio tu zina mizania ya kimantiki bali pia zina mtiririko kama movie fulani hivi inayokushawishi kuendelea kuitazama uone mwisho wake.

Hongera Manju,
MASOUD MASOUD !

I like the way anavyo manage kipindi chake, huyu ni mtangazaji bora niliyewahi kumshuhudia, big up masoud masoud! Lakini mbona masoud sikupati kwenye kipindi chako cha tbc radio cha miziki ya zamani ambapo hujitaja wewe ndo manju wa muziki, ni cha jumamosi saa 5 usiku, na unakirudia jumapili saa 5 asubuhi? Wakurudishie kipindi chako, tunakitaka!!!!
 
Huyu jamaa aliwahi kweli kuwa D.j pale YMCA na marehemu KaliKali akijulikana kama Nigger J ni mtangazaji mahiri unapo msikia kwa ufasaha wa lugha na anajua anacho kifanya awapo hewani hasa inapokuwa ni kwenye nyimbo za zamani,alipata kuwa Uhuru FM kabla ya TBC,ila itoshe tu kumsikia hewani.
 
Wanamwita manju wa muziki. Huyu ni mtangazaji mkongwe na nguli wa maswala ya muziki na wanamziki, kupitia TBC.

Ukimsikiliza Masoud, utaelewa umuhimu wa specialization katika utangazaji, uandaaji vipindi na uandishi habari kwa ujumla.

Masoud anaelewa ni nini anachofanya na kwa muktadha muafaka.

Ukifuatia simulizi zake kimuziki sio tu zina mizania ya kimantiki bali pia zina mtiririko kama movie fulani hivi inayokushawishi kuendelea kuitazama uone mwisho wake.

Hongera Manju,
MASOUD MASOUD !
Ndo nani hiyu? weka picha.
 
Ama hakika hili ni gulu la habari za mziki na wanamziki.
Anaujua mziki hasa wa enzi zile sio hawa vijana wa kileo na kelele kelele za bangi.
Kutangaza hawajui ujuaji mwingi, matusi na maisha yao yamegubikwa makandokando mengi.
Cc Adam Mchomvu&B12
Halafu wanashindwa kutenganisha kazi na maisha binafsi
 
Ama hakika hili ni gulu la habari za mziki na wanamziki.
Anaujua mziki hasa wa enzi zile sio hawa vijana wa kileo na kelele kelele za bangi.
Kutangaza hawajui ujuaji mwingi, matusi na maisha yao yamegubikwa makandokando mengi.
Cc Adam Mchomvu&B12

Pia ni mabingwa wa kukojolesha wenzao
 
Ni mchambuzi wa muziki mbobezi...ila kuna yule Zomboko wa Redio one ndiye anajiita Raisi wa Wachambuzi wa muziki Tanzania.....sijui Masoud ana maoni gani kwa hilo?

Zomboko mtu wa kujikomba sana..afu yeye anajua mziki wa bendi za Daresalama tu na ubabaishaji mwingiii
 
Back
Top Bottom