Mkereketwa_Huyu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 9,836
- 7,231
Wanamwita manju wa muziki. Huyu ni mtangazaji mkongwe na nguli wa maswala ya muziki na wanamziki, kupitia TBC.
Ukimsikiliza Masoud, utaelewa umuhimu wa specialization katika utangazaji, uandaaji vipindi na uandishi habari kwa ujumla.
Masoud anaelewa ni nini anachofanya na kwa muktadha muafaka.
Ukifuatia simulizi zake kimuziki sio tu zina mizania ya kimantiki bali pia zina mtiririko kama movie fulani hivi inayokushawishi kuendelea kuitazama uone mwisho wake.
Hongera Manju,
MASOUD MASOUD !
Jamaa ni manju wa muziki lakini aliniacha hoi pale alipochemsha simulizi za marehemu Papa Wemba. Yaani sijuwi alidanganywa na nani maana alikosea wasifu wa Papa Wemba vibaya sana. Mwingine ambaye alikuwa mtaalam wa muziki ni marehemu Maestro Freddy Mosha. Jamaa alikuwa noma sana, Mungu ailaze roho yake peponi.