TANZIA Mtangazaji Mukhsin Mambo alias MC Hammer afariki dunia nyumbani kwake Marekani

TANZIA Mtangazaji Mukhsin Mambo alias MC Hammer afariki dunia nyumbani kwake Marekani

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Aliyekuwa mtangazaji wa StarTv, Muhsin Mambo Alias MC Hammer afariki dunia siku ya leo tarehe 8 Februari nyumbani kwake nchini Marekani.

Pia soma > Muhsin Mambo yuko wapi?

Hammer.jpg

Mwanahabari Mukhsin Mambo, wakati wa uhai wake​

--
Mwandishi wa habari Mukhsin Mambo, amefariki dunia hii leo Februari 8, 2021, akiwa nyumbani kwake nchini Marekani. Mambo, amewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital hii leo Februari 8, 2021, Bernard James, ambaye ni mmoja wa watu aliowahi kufanyanao kazi amesema kuwa taratibu za msiba zinafanyika jijini Mwanza maeneo ya Capripoint kwa Dada yake.

Aidha James ameongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa za awali zinadai Mambo, alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa kipindi cha muda mfupi na kwamba mpaka mauti yanamfika alikuwa anajisikia vibaya kabla ya kukimbizwa hospitali.

Mukhsin Mambo amewahi kufanya kazi katika kituo cha Radio Free Africa (RFA) Mwanza na TV1.
 
Rip
Kuliko?
Au changamoto ya upumuaji?
 
Dah huyu jamaa nakumbuka Kwenye wimbo wa Hussein Machozi "Kwa ajili yako " ndo alifanya jingo Pia katika Bonga na star ukiachana na Sauda Mwilima huyu pia alikua akiwa interview wasanii ..May his soul rest in peace ,amin [emoji120]
 
Pole sana kwa familia yake pia kwa wafanyakazi wa startv kwa kupoteza hazina.
kifo ni somo tosha kwa sisi tulio baki hai, usiringe ukadhani utaishi Milele hapa duniani, usijeone mzima wa afya ukajifanya wewe ni mwamba na utaishi sana miaka 150!! unakosea,
tuishi maisha ya kumpendeza Mungu wakati wowote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom