Elvis Legacy
JF-Expert Member
- Aug 10, 2017
- 3,984
- 5,820
Apumzike kwa amani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Poleni sana. Ukweli hayo majina yamenikumbusha mbili sana likiwemo la David Wakati. Nakumbuka kusikia uteuzi wake wa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa RTD nilipokuwa nasikiliza taarifa ya habari ambapo Raisi Mwinyi ndio alimteua David Wakati kuwa Mkurugenzi Mkuu.asante kwa taarifa hii
Moja ya simulizi za maisha yetu na Sued Mwinyi.
Tukiwa ndiyo mwanzo mwanzo tumejiunga na rtd mimi, Sued Mwinyi na Pascal Mayala baada ya kumaliza mafunzo yetu ya utangazaji pale mjengoni tukapelekwa idhaa ya biashara, mkuu wa idhaa akiwa Mikidadi Mahamoud na wasaidizi wake Sekione Kitojo, Salama Mfamao(Rip)na Siwatu Luanda(Rip).
Pascal akapewa kipindi cha Karibu Vijana kinatoka saa 10.45-11.00 jioni. Sued akapewa Salam Mkulima na mimi nikapewa kipindi cha Pole kwa Kazi(11.05-12.00 jioni).
Wakati ule vipindi hivyo vyote ni recorded yaani vinatayarishwa mapema na kuja kurushwa baadaye.
Sued alikuwa shabiki mkubwa wa muziki wa Reggae, Pascal yeye ngoma za kizungu za kuruka majoka na mimi nikihusudu sana mabolingo.
Basi katika vipindi vile vyetu ambavyo nilikuwa vya salaam, Sued akawapigia wakulima Reggae tupu, Pascal yeye kwa vijana alibakia Marekani na mimi katika pole kwa kazi nikawapa pole wafanyakazi kwa mabolingo mtindo mmoja.
Vipindi vilivyomalizika kwenda hewani siku ya pili yake wakuu katika kikao chao chini Mkurugenzi David Wakati(Rip) wakatufanyia tathmini na kuona kuwa tulikuwa hatuna utaifa na uzalendo kwa utamaduni wetu.
Basi tukahamishwa haraka sana.Mimi nikapelekwa idhaa ya taifa chini ya Fauziyat Ismail Aboud, Sued nadhani akarudishwa External Service( sote watatu tulianzia huko) na Pascal akapelekwa kitendo cha ngoma zetu akapewa kipindi cha tuimbe sote na ngoma zetu bosi wake akiwa Khalid Ponera na Msaidizi wake Michael Katembo.
Hapo kwangu ndiyo ukawa mwanzo wa kuzijua na kuzipenda nyimbo za bendi zetu kwa sababu nilipewa kuandaa kipindi cha mchana mwema, Jambo na jioni njema.
Pascal Mayala mpaka leo anazijua sana ngoma za makabila yetu pamoja na kwaya za shule ya msingi ya Khana Tanga.
KWAHERI SUED MWINYI
C&P
Abubakar Liongo
Ni ngumu sana kusimulia maisha ya mwenziyo mliyoanza pamoja maisha na sasa ametangulia mbele ya haki.
Sued Ramadhan Mwinyi tuliajiriwa siku moja pale RTD June 1989. Mwengine ni Pascal Mayalla. Baadaye tukaanza kozi ya utangazaji hapo hapo RTD tukijumuika na Bakari Msulwa, Eshe Muhiddin,Nyambona Masamba, Shida Wazir,Kassim Mikongolo(rip) kwa uchache niliyowakumbuka.
Lakini ilitokea sisi watatu, Sued,Pascal na mimi tukawa maswahiba sana. Kuna mengi sana ya kusimulia kuhusu ndugu yangu huyu. Nakumbuka siku ya harusi yangu 1996 Sued alivaa suti akisema ni mara yake ya kwanza kuvaa suti pale Pool Side Kilimanjaro Hotel(now Kempiski).
Nyambona Massamba kwa niaba ya mwenzangu Pascal Mayalla tunakupa asante na hongera sana kwa kusimamia matibabu ya mwenzetu(utatu wetu) hadi umauti ulipomfika.
Sued umetangulia sehemu ambako swahiba wetu aliyetupokea External Service Mohamed Dahman atakupokea tena japo mara hii ukiwa peke yako bila ya Pascal Mayalla na Aboubakary Liongo.
Utapokelewa pia na Nadhir Mayoka, Salama Mfamao, Siwatu Luanda, Sara Dumba,Kassim Mikongolo,Hassan Mkumba, Hendrik Libuda, Ahmed Jongo,Khalid Ponera, Tumbo Risasi, Julius Nyaisanga na wengine.
Mwenyezimungu akuondolee adhabu ya kabri, akusamehe makosa yako.
IKO SIKU ISIYO NA JINA TUTAONANA HUKO ULIKOTANGULIA
C&P About
Abubakar Liongo
Pole sana Chief @Abou Liongo , na asante sana kwa kumbukumbu hii ya enzi zetu. Batch yetu ya Watangazaji 10, wanaume 5 na wanawake watano. Swedy Mwinyi, Abubakar Liongo, Bakari Msulwa, Kassim Mikongolo na mimi Pascal Mayalla. Wanawake ni Eshe Muhidin, Shida Waziri, Nyambona Masamba, Jane Rutaserwa na Rose Japhet. Batch yetu ndio iliyokuwa batch ya mwisho ya watangazaji kuajiriwa enzi za Mkurugenzi David Wakati. Abou Liongo na Swedy Mwinyi ndio watangazaji wa kwanza wa umri mdogo kusoma habari RTD. Ikatoea Mimi, Swedy na Abou, kuwa marafiki wa karibu na kuanza kutembeleana home. Swedy alipofiwa na mama yake, tulisindikiza Morogoro kuzika, Swedy alipofiwa na baba yake, tulishiriki bega kwa bega kuzika, sasa leo tunakutana tena kumsindikiza mwenzetu tuliyeanza naye kazi siku moja. Ni huzuni kubwa!. Innalillah wa inna illah Raajiun!.
Pascal Mayalla
Unakumbuka kilichomkuta wakati wa uchaguzi mkuu 2015 ?Inasemekena alikuwa kwenye bodi ya TBC iliyotunga neno kabambe la TUNATEKELEZA ili kumsifia Jiwe
SikumbukiUnakumbuka kilichomkuta wakati wa uchaguzi mkuu 2015 ?
Tuko pamoja nduguOK mkuu nimekuelewa haina shida .
I remember this day...Dominic Chilambo.
Alifariki akiwa anatangaza mpira kati ya Tukuyu Star vs Yanga/Simba.
Kipindi cha michezo saa moja na nusu RTD Halima Mchuka akatangaza kifo chake kwa masikitiko makubwa sana akiwa ameweka wimbo flani hivi na kisha kuweka sauti ya mwisho ya Chilambo akiwa anatangaza hiyo match.
asante kwa taarifa hii
Moja ya simulizi za maisha yetu na Sued Mwinyi.
Tukiwa ndiyo mwanzo mwanzo tumejiunga na rtd mimi, Sued Mwinyi na Pascal Mayala baada ya kumaliza mafunzo yetu ya utangazaji pale mjengoni tukapelekwa idhaa ya biashara, mkuu wa idhaa akiwa Mikidadi Mahamoud na wasaidizi wake Sekione Kitojo, Salama Mfamao(Rip)na Siwatu Luanda(Rip).
Pascal akapewa kipindi cha Karibu Vijana kinatoka saa 10.45-11.00 jioni. Sued akapewa Salam Mkulima na mimi nikapewa kipindi cha Pole kwa Kazi(11.05-12.00 jioni).
Wakati ule vipindi hivyo vyote ni recorded yaani vinatayarishwa mapema na kuja kurushwa baadaye.
Sued alikuwa shabiki mkubwa wa muziki wa Reggae, Pascal yeye ngoma za kizungu za kuruka majoka na mimi nikihusudu sana mabolingo.
Basi katika vipindi vile vyetu ambavyo nilikuwa vya salaam, Sued akawapigia wakulima Reggae tupu, Pascal yeye kwa vijana alibakia Marekani na mimi katika pole kwa kazi nikawapa pole wafanyakazi kwa mabolingo mtindo mmoja.
Vipindi vilivyomalizika kwenda hewani siku ya pili yake wakuu katika kikao chao chini Mkurugenzi David Wakati(Rip) wakatufanyia tathmini na kuona kuwa tulikuwa hatuna utaifa na uzalendo kwa utamaduni wetu.
Basi tukahamishwa haraka sana.Mimi nikapelekwa idhaa ya taifa chini ya Fauziyat Ismail Aboud, Sued nadhani akarudishwa External Service( sote watatu tulianzia huko) na Pascal akapelekwa kitendo cha ngoma zetu akapewa kipindi cha tuimbe sote na ngoma zetu bosi wake akiwa Khalid Ponera na Msaidizi wake Michael Katembo.
Hapo kwangu ndiyo ukawa mwanzo wa kuzijua na kuzipenda nyimbo za bendi zetu kwa sababu nilipewa kuandaa kipindi cha mchana mwema, Jambo na jioni njema.
Pascal Mayala mpaka leo anazijua sana ngoma za makabila yetu pamoja na kwaya za shule ya msingi ya Khana Tanga.
KWAHERI SUED MWINYI
C&P
Abubakar Liongo
Ni ngumu sana kusimulia maisha ya mwenziyo mliyoanza pamoja maisha na sasa ametangulia mbele ya haki.
Sued Ramadhan Mwinyi tuliajiriwa siku moja pale RTD June 1989. Mwengine ni Pascal Mayalla. Baadaye tukaanza kozi ya utangazaji hapo hapo RTD tukijumuika na Bakari Msulwa, Eshe Muhiddin,Nyambona Masamba, Shida Wazir,Kassim Mikongolo(rip) kwa uchache niliyowakumbuka.
Lakini ilitokea sisi watatu, Sued,Pascal na mimi tukawa maswahiba sana. Kuna mengi sana ya kusimulia kuhusu ndugu yangu huyu. Nakumbuka siku ya harusi yangu 1996 Sued alivaa suti akisema ni mara yake ya kwanza kuvaa suti pale Pool Side Kilimanjaro Hotel(now Kempiski).
Nyambona Massamba kwa niaba ya mwenzangu Pascal Mayalla tunakupa asante na hongera sana kwa kusimamia matibabu ya mwenzetu(utatu wetu) hadi umauti ulipomfika.
Sued umetangulia sehemu ambako swahiba wetu aliyetupokea External Service Mohamed Dahman atakupokea tena japo mara hii ukiwa peke yako bila ya Pascal Mayalla na Aboubakary Liongo.
Utapokelewa pia na Nadhir Mayoka, Salama Mfamao, Siwatu Luanda, Sara Dumba,Kassim Mikongolo,Hassan Mkumba, Hendrik Libuda, Ahmed Jongo,Khalid Ponera, Tumbo Risasi, Julius Nyaisanga na wengine.
Mwenyezimungu akuondolee adhabu ya kabri, akusamehe makosa yako.
IKO SIKU ISIYO NA JINA TUTAONANA HUKO ULIKOTANGULIA
C&P About
Abubakar Liongo
Pole sana Chief @Abou Liongo , na asante sana kwa kumbukumbu hii ya enzi zetu. Batch yetu ya Watangazaji 10, wanaume 5 na wanawake watano. Swedy Mwinyi, Abubakar Liongo, Bakari Msulwa, Kassim Mikongolo na mimi Pascal Mayalla. Wanawake ni Eshe Muhidin, Shida Waziri, Nyambona Masamba, Jane Rutaserwa na Rose Japhet. Batch yetu ndio iliyokuwa batch ya mwisho ya watangazaji kuajiriwa enzi za Mkurugenzi David Wakati. Abou Liongo na Swedy Mwinyi ndio watangazaji wa kwanza wa umri mdogo kusoma habari RTD. Ikatoea Mimi, Swedy na Abou, kuwa marafiki wa karibu na kuanza kutembeleana home. Swedy alipofiwa na mama yake, tulisindikiza Morogoro kuzika, Swedy alipofiwa na baba yake, tulishiriki bega kwa bega kuzika, sasa leo tunakutana tena kumsindikiza mwenzetu tuliyeanza naye kazi siku moja. Ni huzuni kubwa!. Innalillah wa inna illah Raajiun!.
Pascal Mayalla
Ahmed Jongo kumbe alishafariki. Omary Jongo bado yupo?Ahmed Jongo
Ezekiel Malongo
Halima Mchuka
Sued Mwinyi
Mlifanya matangazo ya mpira na kioinfi cha michezo RTD kuwa moto sana!!
Nazeeka sasa
Pumzikeni kwa amani Ma-Legend
We mahondaw hiyo picha ya kwenye avatar niwewe.Apumzike kwa amani
Alikua ana tangaza mpira vizur sana siyo Watangazaji wa sasa hawajui chochote zaidi ya kelele na wasifiwa wanajua.Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un
Jamii ya wanamchezo watamkumbuka sana kwa sauti yake iliyokuwa ikituhabarisha michezo hususani mpira wa miguu.
Chilambo DominicPana Mtangazaji mmoja alikuwa anatangaza Mwanza nae alifariki Mbeya simbubuki jina alikuwa anaweza kutangaza kikosi cha Tipso wa lindanda akiwa anawaona wanatroti tu wenyewe walikua wanasema naona Wachezaji wanapasha misuri joto pale au wanapiga njalamba pale...
Alikua anatangaza kikosi cha Pamba ya Mwanza kwa kuwaangalia wakiwa wanachukua mazoezi ya viungo bila hata kupewa karatasi na ikija karatasi kikosi ni kile kile kile wana Tispo lindanda...Chilambo Dominic