TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

Dah, inatisha na kuumiza. Sijui ndugu zetu wa Clouds wanahali gani. Israel alikuwa anatafuta mmoja tangu jana walipopata ajali bahati nzuri hawakupata majeraha makubwa! Leo kaamua kutumia njia tofauti kuondoka na Kibonde. Dah
Nimekumbuka wimbo wao: Mbinguni hakuna bia.... Dah Kibonde leo ni zamu yako kunywa zako bia! Ama kweli maisha haya ni ubatili mtupu!
 
Uhai ni zawadi, kifo ni lazima. Pumzika kwa amani Kibonde[emoji120][emoji120]
 
Hii poem inasikitisha [emoji22][emoji22][emoji22]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
How do you know that I am happy?Are you pastor Lukau younger brother?
Huyu atakuwa mwagito mpaka anaweza kusoma hisia zako
Ni kutokana na jinsi unavyiandika maneno mtu anaweza kusoma hisia zako, umeandika kana kwamba ni habari ya kufurahisha, jifunze namna ya kuleta habari za misiba, Nimeumizwa na msiba, Pumzika kwa amani Ephraim, umetimiza wajibu wako duniani uliobaki ni wetu, Tangulia.. tunakuja.
 
Clouds inaweza kupitia kipindi kigumu. Hali inayoonekana au inayotokea kwasasa ni hali ya matukio, ambayo inaweza kupelekea Clouds kupita katika kipindi kigumu, kwa kampuni na wafanyakazi wake.

Ifahamike kuwa, Ruge alikuwa kiongozi mkubwa, na alifahamika kama Boss Ruge. Ieleweke vizuri kuwa, hakuna mfanyakazi aliyeko kazini hasiyempenda boss wake. Kila mfanyakazi huwa na tumaini/hisia/mapenzi ya dhati na boss wake, hata kama hawaongei mara kwa mara. Utendaji wa Boss Ruge, ulimgusa kila mfanyakazi wa Clouds, kwa namna moja ama nyingine. Kama watanzania wameguswa kiasi cha juu, inakuwaje kwa wafanyakazi wa clouds?

Ushauri ni huu: Wapate muda wa kupumzika. Katika kipindi hiki cha mapumziko, wapate mtaalamu wa masuala ya Psychology kutokea nje ya kampuni yao ili kuja kuongea na wafanyakazi. Najua kuwa, clouds ina wafanyakazi wenye talent kubwa ya utangazaji, na zaidi wenye uelewa mkubwa sana wa masuala ya kijamii. Ila kwa kipindi hiki, wanahitaji mtu wa nje yao, kuja kuongea nao. Hii itasaidia kuwaongezea kitu kipya ambacho kitawasaidia kuwawezesha kuzidi kuwa na uthubutu wa akili, na uwezo wa mwili kuhimili mikiki ya kazi, hasa kipindi hiki kikiisha. Pia, kuhimili hisia na furaha, hasa kuhamisha mawazo yao kutoka kwa mpendwa wao Ruge, na kujenga upya hisia/furaha zao kwenye maisha yao.

Ruge ameshatangulia mbele za haki, na ameishaimaliza kazi yake hapa duniani.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Clouds. Amen!..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ujumbe uwafikie wakolomije wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…