TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

RIP Bro!
Mungu akupokee huko upande wa pili
Nenda salama ndugu yetu
Salamu kwa ndugu yako Kaka yako mfanyakazi mwenzako Ruge
** Hakuna aijuaye kesho. Mungu tufundishe kuomba na kujiandaa
 
daah iam speechless kwa kweli
 
So sad,kifo ni fumbo kubwa sana,pole sana ndugu,jamaa na marafiki pia familia nzima ya Clouds media group na wanafamilia wote,Pumzikiza kwa amani kaka yangu Kibonde.
 
Umeandika ujumbe mzito sana ndugu,binadamu wote inabidi tuishi kwa kulitambua hilo,dunia ni mapito tuishi kwa upendo.R.I.P kaka kibonde.
 
Tulikosea wapi wanadamu mpk Mungu ukaamua kutuletea KIFO? Eeh baba Sijui hii niite Adhabu au niite nini lakini BABA najua unatusikia TUSAMEHE tubadilishie hii adhabu tunajaribu kuizoea lakini haizoeleki BABA,natamani miaka irudi nyuma tuweze kuongea nawewe uso kwa uso kama kina MUSA na manabii wengine ulivyokua ukiongea nao Hakika Ningesimama chini yako na kuomba ufute hiki kitu.

Mungu huna makosa kazi yako sikuzote hakuna wakuipinga lkn KIFO ni zaidi ya Adhabu baba,tuepushie tupe mbadala au maandalizi ya kukipokea lakini BABA unatushtukiza TU hutuambiii why lord? Tuonee huruma Tunaumia mioyo yetu angalia tunaishi kwa kutojiamini Maisha yanapoteza ladha, tusaidie baba Tukiwa bado hata hatujapona kidonda kingine tayari unakuja na lingine eeh BABA tufanye nini sisi?

Tupe hata ishara ya kitu unachotaka kifanyike tukifanye tu ili utuondolee hiki kitu KIFO tuonyeshe hata ishara baba tufanye nini ili tukusahaulishe maumivu tuliyokusababishia huko nyuma kiasi cha kutuacha na adhabu kali na kubwa isiyozoeleka kama hiii,bado ni mtihani mzito mbele yetu BABA .

DEAR GOD,hear my PRAYERS.
 
Pole sana watoto na familia na pole sana CMG kwa kuondokewa na watu muhimu sana katika muda mfupi
 
https://www.facebook.com/
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…