Kila Nafsi Itaonja Mauti Na Hakuna Atakayebakia Isipokuwa Allaah ุณุจุญุงูู ูุชุนุงูู
Kila Nafsi Itaonja Mauti Na Hakuna Atakayebakia Isipokuwa Allaah ุณุจุญุงูู ูุชุนุงูู
Iymaan-Taqwa
Anasema Allaah ุณุจุญุงูู ูุชุนุงูู:
ููููู ููููุณู ุฐูุขุฆูููุฉู ุงููู
ูููุชู ููุฅููููู
ูุง ุชูููููููููู ุฃูุฌููุฑูููู
ู ููููู
ู ุงููููููุงู
ูุฉู ููู
ูู ุฒูุญูุฒูุญู ุนููู ุงููููุงุฑู ููุฃูุฏูุฎููู ุงููุฌููููุฉู ููููุฏู ููุงุฒู ููู
ุง ุงููุญูููุงุฉู ุงูุฏููููููุง ุฅููุงูู ู
ูุชูุงุนู ุงููุบูุฑููุฑ
((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu)) [Al-'Imraan: 185]
Tokea kuumbwa kwa Nabii Aadam ุนููู ุงูุณูุงู
hadi leo na mpaka siku ya Qiyaamah hakuna kiumbe kitakachobakia isipokuwa Mwenyewe Mola Mtukufu kama Anavyosema:
ููููู ุดูููุกู ููุงูููู ุฅููููุง ููุฌููููู
((Kila kitu kitaangamia isipokuwa Yeye)) [Al-Qaswas: 88]
Vile vile Anasema Allaah ุณุจุญุงูู ูุชุนุงูู :
((ููููู ู
ููู ุนูููููููุง ููุงูู))
((ููููุจูููู ููุฌููู ุฑูุจูููู ุฐูู ุงููุฌูููุงูู ููุงููุฅูููุฑูุงู
))
((Kila kilioko juu Yake kitatoweka))
((Na Atabakia Mwenyewe Mola wako Mwenye utukufu na ukarimu)) [Ar-Rahmaan: 26-27]
Baada ya kupulizwa Swuur (baragumu) siku ya Qiyaamah viumbe vyote vitakufa kwa mpangilio Anaoutaka Mwenyewe Allaah ุณุจุญุงูู ูุชุนุงูู. Kisha mwisho atabakia Malakul Mawt (Malaika mtoaji roho) na Allaah ุณุจุญุงูู ูุชุนุงูู. Kisha Allaah ุณุจุญุงูู ูุชุนุงูู Atamuamrisha Malakul Mawt ajitoe roho yake mwenyewe. Atakapokufa Malakul Mawt Atabakia Allaah ุณุจุญุงูู ูุชุนุงูู Pekee wa Mwanzo na wa Mwisho, Al-Hayyul-Qayyuum (Mwenye uhai wa maisha, Msimamia kila jambo). Allaah ุณุจุญุงูู ูุชุนุงูู Siku hiyo Atazikusanya ardhi na mbingu katika Mikono Yake,
((ููุงููุฃูุฑูุถู ุฌูู
ููุนูุง ููุจูุถูุชููู ููููู
ู ุงููููููุงู
ูุฉู ููุงูุณููู
ุงููุงุชู ู
ูุทููููููุงุชู ุจูููู
ูููููู))
((Na Siku ya Qiyaamah ardhi yote itakuwa mkononi Mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume)) [Az-Zumar: 67]
Na Hadiyth kutoka kwa Ibn 'Umar ุฑุถู ุงููู ุนูู kwamba:
((ูุทูู ุงูุณู
ูุงุช ูุงูุฃุฑุถ ุจูุฏูุ ุซู
ูููู: ุฃูุง ุงูู
ููุ ุฃูุง ุงูุฌุจุงุฑุ ุฃูุง ุงูู
ุชูุจุฑุ ุฃูู ู
ููู ุงูุฃุฑุถุ ุฃูู ุงูุฌุจุงุฑููุ ุฃูู ุงูู
ุชูุจุฑููุ)) ู
ุณูู
((Allaah Atazikunja mbingu kwa Mikono Yake, kisha Atasema, Mimi ni Mfalme, Mimi ni Al-Jabbaar (Mwenye Kushurutisha), wako wapi wafalme wa dunia? Wako wapi majabbaar (wanaolazimisha), wako wapi wanaotakabari?))[Muslim]
Hapo tena Atauliza mara tatu:
((ูููู
ููู ุงููู
ููููู ุงููููููู
ู))
((Ufalme ni wa nani leo?)) [Ghaafir:16]
Hakutakuwa na mtu wa kujibu, basi Atajibu Mwenyewe,
((ููููููู ุงููููุงุญูุฏู ุงูููููููุงุฑ))
((Ni wa Allaah Mmoja Mtenda Nguvu)) [Ghaafir 16]
Na hapo tena ndipo kila mtu atakuta hesabu yake ya matendo aliyoyatenda duniani ikiwa ni mema au mabaya, hakuna atakayedhulumiwa hata chembe, kwani Allaah ุณุจุญุงูู ูุชุนุงูู Atahukumu kwa uadilifu baina ya viumbe Vyake. Kila jema Atalilipa kwa mara kumi na kila ovu atahesabiwa mja kwa ovu moja.
((ุงููููููู
ู ุชูุฌูุฒูู ููููู ููููุณู ุจูู
ูุง ููุณูุจูุชู ููุง ุธูููู
ู ุงููููููู
ู ุฅูููู ุงูููููู ุณูุฑููุนู ุงููุญูุณูุงุจู))
((Leo kila nafsi italipwa kwa iliyochuma. Hapana dhulma leo. Allaah ni Mwepesi wa kuhisabu)) [Ghaafir: 17]