TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

Sijui walikuwa na watoto? Balaa gani hili kwao!

Habari za hivi punde ni kuwa mtangazaji maarufu wa Clouds FM, Ndugu Ephraim Kibonde amefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 7 Machi 2019.

Kibonde alianza kusumbuliwa na presha akiwa katika msiba wa marehebu Ruge Mutahaba huko Bukoba mkoani Kagera na kuhamishiwa hospitali ya Bugando jijini Mwanza ambapo mauti yamemkuta.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa

Mwaka jana Ephraim Kibonde alimpoteza mkewe mama Sara Kibonde. Zaidi soma >TANZIA: Ephraim Kibonde afiwa na Mke wake Sara Kibonde - JamiiForums

View attachment 1039958
Ephraim Kibonde akiwa na mkewe enzi za uhai wao​

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Du!,jamani[emoji26]
RIP Brother.

Sent from Nokia 7 Plus
 
Hata sisi kwetu haturuhusiwi kuchimba kaburi lilale bila kuzika, labda wazee wa maeneo husika wasiwepo, lakini hata kama wazee hawapo haijawahi tokea hivo, watu wanazikwa hata kama kuna mvua ya namna gani, nakumbuka kuna mtu walimzika huku mvua kubwa inanyesha, kazi ilikua ni kutoa maji yaliyokua yanaingia kaburini.

Nimeanza kuamini.
 
Kila Nafsi Itaonja Mauti Na Hakuna Atakayebakia Isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى
Kila Nafsi Itaonja Mauti Na Hakuna Atakayebakia Isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى
Iymaan-Taqwa
Anasema Allaah سبحانه وتعالى:

كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَما الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ مَتَاعُ الْغُرُور
((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu)) [Al-'Imraan: 185]

Tokea kuumbwa kwa Nabii Aadam عليه السلام hadi leo na mpaka siku ya Qiyaamah hakuna kiumbe kitakachobakia isipokuwa Mwenyewe Mola Mtukufu kama Anavyosema:
كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ
((Kila kitu kitaangamia isipokuwa Yeye)) [Al-Qaswas: 88]

Vile vile Anasema Allaah سبحانه وتعالى :

((كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ))
((وَيَبْقَى وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَام))

((Kila kilioko juu Yake kitatoweka))
((Na Atabakia Mwenyewe Mola wako Mwenye utukufu na ukarimu)) [Ar-Rahmaan: 26-27]

Baada ya kupulizwa Swuur (baragumu) siku ya Qiyaamah viumbe vyote vitakufa kwa mpangilio Anaoutaka Mwenyewe Allaah سبحانه وتعالى. Kisha mwisho atabakia Malakul Mawt (Malaika mtoaji roho) na Allaah سبحانه وتعالى. Kisha Allaah سبحانه وتعالى Atamuamrisha Malakul Mawt ajitoe roho yake mwenyewe. Atakapokufa Malakul Mawt Atabakia Allaah سبحانه وتعالى Pekee wa Mwanzo na wa Mwisho, Al-Hayyul-Qayyuum (Mwenye uhai wa maisha, Msimamia kila jambo). Allaah سبحانه وتعالى Siku hiyo Atazikusanya ardhi na mbingu katika Mikono Yake,

((وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّماوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ))

((Na Siku ya Qiyaamah ardhi yote itakuwa mkononi Mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume)) [Az-Zumar: 67]

Na Hadiyth kutoka kwa Ibn 'Umar رضي الله عنه kwamba:

((يطوي السموات والأرض بيده، ثم يقول: أنا الملك، أنا الجبار، أنا المتكبر، أين ملوك الأرض؟ أين الجبارون؟ أين المتكبرون؟)) مسلم

((Allaah Atazikunja mbingu kwa Mikono Yake, kisha Atasema, Mimi ni Mfalme, Mimi ni Al-Jabbaar (Mwenye Kushurutisha), wako wapi wafalme wa dunia? Wako wapi majabbaar (wanaolazimisha), wako wapi wanaotakabari?))[Muslim]

Hapo tena Atauliza mara tatu:
((لِّمَنِ الْمُلْكُ الْيَوْمَ))
((Ufalme ni wa nani leo?)) [Ghaafir:16]

Hakutakuwa na mtu wa kujibu, basi Atajibu Mwenyewe,
((لِلَّهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّار))

((Ni wa Allaah Mmoja Mtenda Nguvu)) [Ghaafir 16]

Na hapo tena ndipo kila mtu atakuta hesabu yake ya matendo aliyoyatenda duniani ikiwa ni mema au mabaya, hakuna atakayedhulumiwa hata chembe, kwani Allaah سبحانه وتعالى Atahukumu kwa uadilifu baina ya viumbe Vyake. Kila jema Atalilipa kwa mara kumi na kila ovu atahesabiwa mja kwa ovu moja.

((الْيَوْمَ تُجْزَى كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ))

((Leo kila nafsi italipwa kwa iliyochuma. Hapana dhulma leo. Allaah ni Mwepesi wa kuhisabu)) [Ghaafir: 17]
 
Bob Marley alikufa na miaka 36, akiwa bado kijana mbichi kabisa.

Malcom X alikufa na miaka 39 akiwa na mipango mingi tu ya kuleta mabadiliko ya kisiasa kwa wamarekani weusi.

Martin Luther King alikufa na miaka 39 akiamini kwamba yupo tayari kuelekea mbinguni.

John Lennon alikufa na miaka 40, mmoja wa mashabiki wake alimpiga risasi.

Mwanamuziki Gerard Levert mzee wa Cassanova alikufa na miaka 40 baada ya kunywa dawa aina mbili tofauti zilizotengeneza sumu mwilini mwake.

Rajiv Gandhi alikufa na miaka 46, akiwa bado kijana mng'avu na mwenye matumaini mengi tu.

John F Kennedy alikufa na miaka 46, akiamini kuwa uchaguzi wa mwaka 1964 angeweza kushinda na kuiongoza Marekani kwa mihula miwili.

Edward Moringe Sokoine alikufa na miaka 46, akiwa katikati ya vita dhidi ya wahujumu uchumi.

Mjasiriamali Ruge Mutahaba kaondoka duniani na miaka 48 akiwa na mipango mingi mikubwa.

Nahisi Marehemu Ephraim Kibonde ni wa umri huo huo wa Ruge, nae kaondoka na uchangamfu wake maskini!.

Maishani unaweza usifikishe hata miaka 50 kwa mipango ya Mungu, unaweza ukawa na miaka 45 au chini ya hapo lakini kumbe wewe ni "mzee" tayari.

Ujumbe wa hao wote niliowataja na ambao waliaga dunia wakiwa hata hawajaishi nusu karne ni kwamba muda wetu ni mfupi.

Uhairishaji wa mambo (procrastination) wakati hujui kama wewe tayari ni "mzee" kwa mipango ya muumba wetu sio jambo jema.

Kesho hatuijui, kwanini tunapoteza muda kwenye kuendekeza siasa za makundi na upambe na uhasama wakati muda wetu hatujui utaisha lini?.

Vipaji vyetu na tuvitumie kwa ajili ya kuinua maisha yetu binafsi na kuuinua mustakabali mwema wa Tanzania.

Tunajua tumekuja lini duniani lakini hatujui hii sinema yenye mengi iitwayo maisha, itamalizika lini na sehemu gani.

RIP Kaka Kibonde, RIP Kaka Ruge. Siku zetu chini ya jua sio nyingi kama tunavyozipanga katika mipango yetu, dakika ya kufanya masuala ya muhimu ndio hii ya sasa.
 
Back
Top Bottom