TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

Kibonde alikuwa anaipa radha Jahazi kwa kuropoka kwake sijui nani ataifit style ile!!..
 
Aliwaponda sana kina Dr Ulimboka na walichokuwa wanakipigania enzi zile 2012, sasa yale yale waliyokuwa wanalalamika ndio hayo hayo yamemkuta. Nenda tu kaka panapokustahili
 
Pole sana familia kwa kumpoteza baba na mama. Nawaonea huruma sana watoto wa marehemu kwa kuwapoteza wazazi wao wote. Nina imani Mungu atawalea kwani yeye ndiye muweza wa kila jambo.

Pole aside, kifo cha kibonde kiwe fundisho kwa watangazaji wengine wanaotumia sauti zao kukandamiza haki za wengine au kupindisha ukweli. Tumejifunza kitu kufuatia kifo cha Ruge kutoka kwa watu mbalimbali kama Konki na Jide. Hili ni fundisho kuwa unapokuwa hai, jitahidi kuwatendea haki kila mtu bila kujali nafasi yake ktk jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu kwa uchungu unaopitia, ila kuhusu binadamu kufa hiyo ni nature tu, mzungu/mwarabu alijaribu kutuhadaa kuwa kuna maisha baada ya kifo, its just fiction...
Mkuu hata bila mzungu mbona imani zetu za jadi pia zimetufundisha hivyo. Hujasikia habari za mizimu,mahoka na matambiko mbali mbali kwa hiyo mizimu?

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…