TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

Wana watoto watatu,mkubwa wa kiume yupo chuo kama si mwaka wa kwanza basi wa pili,wa pili sekondar, na wa tatu primary wakike hawa
Dah...sijui alijiwekea bima..dah... Kusaga inabidi alipe fadhila tu...hakuna namna...

Sent using Beretta ARX 160
 
Dah...Cha msingi ni kujipanga....yaani kutoacha pengo lisilozibika kwenye maisha yako binafsi...hasa kwenye majukumu...[emoji41]

Sent using Beretta ARX 160
 
Mwili wa aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde, umewasili wakati huu hapa nyumbani kwa wazazi wake, maeneo ya Mbezi Africana jijini Dar es Salaam.

Kibonde alifariki Machi 6, 2019 alipokuwa akiwahishwa Hospitali ya Bugando Mwanza baada ya hali yake kubadilika ghafla alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya Uhuru jijini Mwanza.

Baada ya taratibu zote za kuaga na ibada, msafara utaondoka hapa nyumbani milango ya saa 9 kwenda kumlaza kwenye nyumba yake ya milele, katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Kibonde alikuwa muongozaji wa shughuli (MC) kwenye msiba wa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba aliyezikwa Machi 4, 2019, alianza kujihisi vibaya mara baada ya maziko hayo yaliyofanyika Bukoba mkoani Kagera.
Hawawezi kuwa na Misa. Hao si mashahidi was yehova?
 
Mtoto wa pili wa mpendwa wetu Ephraim Kibonde akiwa kwenye hali ya huzuni kwani leo ndiyo siku ambayo anaenda kumpumzisha Baba yake kwenye makazi ya milele na kutomuona tena, Huzuni imetawala, mioyo inayovuja jasho la uchungu huku machozi yasiyokatika yakidondoka
 

Nami pia nakumbuka kile kijiwe chenye mabomba pale nyumba ya ile kona inayotazamana na Don Bosco!

Ephraim Kibonde ni mmoja watu ambao hawakati tamaa kutumia vipaji vyao na kuchakarika na alianza mapema sana.

Ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha kuondoka duniani tukiwa bado tunafaidi maisha yetu na kuacha familia changa lakini yote hayo ni mipango ya Mungu na kifo hakina appointment ni wakati wowote ule na mahali popote.

Namkumbuka Ephraim wakati kuna kipindi fulani tulipiga boksi pale UK (Royal Mail) na alikuwa so entertainer yaani ni mtu ambae utapenda kuwa nae karibu kwa vichekesho na mazumgumzo yake.

Hakika, kipindi cha Jahazi kitakosa mmoja wa wachangiaji mahiri sana.

Halikadhalika CMG imepoteza vipaji maalum vya Ruge Mutahaba na Ephraim Kibonde.

Pia wadau mbalimbali waloshiriki na Ephraim nao watamkosa mtu muhimu sana.

RIP Ephraim.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…