TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

GARDNER: TULIPOKWENDA HOSPITAL YA RUFAA MKOANI KAGERA DAWA ALIZOTAKIWA KUMEZA KIBONDE ZILIKOSEKANA "GARDNER

Gardner G habash ameyasema hayo alipohojiwa na kituo cha ITV kua hali ya rafiki yake na mtangazaji mwenzake ephraim kibonde ilibadilika na kuanza kujisikia vibaya walipokua kwenye msiba wa boss wao ruge mkoani kagera.

baada ya kumkimbiza katika hospital ya rufaa wilayani bukoba mkoani hapo dawa alizotakiwa kumeza ili kupata nafuu zilikosekana hospitalini hapo, walizitafuta katika maduka ya dawa bila mafanikio kwani maduka mengi ya dawa mmda huo yalikua yamefungwa..

Ndipo hali yake ikazidi kuwa mbaya wakampeleka mwanza had umauti ulivyomkuta

CHANZO: ITV HABARI 20:00 EAT
Sisi ni dona kantiri halafu mkoa mzima dawa hamna?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Habari za hivi punde ni kuwa mtangazaji maarufu wa Clouds FM, Ndugu Ephraim Kibonde amefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 7 Machi 2019.

Kibonde alianza kusumbuliwa na presha akiwa katika msiba wa marehebu Ruge Mutahaba huko Bukoba mkoani Kagera na kuhamishiwa hospitali ya Bugando jijini Mwanza ambapo mauti yamemkuta.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa

Mwaka jana Ephraim Kibonde alimpoteza mkewe mama Sara Kibonde. Zaidi soma >TANZIA: Ephraim Kibonde afiwa na Mke wake Sara Kibonde - JamiiForums

View attachment 1039958
Ephraim Kibonde akiwa na mkewe enzi za uhai wao​
R.I.P EK.
Lipo la kujifunza kila kifo cha mwanadamu kinapotokea.
 
Hongera wewe ambaye huna miwaya, so una guarantee ya kuishi milele.


Semeni nyie..leo humu nimestaajabu mno mno!hvy kwa maisha hayya kuna mtu hajaathirika kwa namna 1 au nyingine na hili gonjwa?kwahyo sasa kila mtu ameungua..aise inakera sana..sijui wanaougua huu ugonjwa wakiona vitu km hv wanJiskiaje..!semen nyie
 
Rafiki yangu Ephrahim, Tulicheza Basketball, Football, Keram, Table Tenis pamoja wote Don Bosco Upanga, Tulikuwa hatukosi kila siku Don Bosco baada ya shule, baada ya ukubwa vijana wote kila mtu aliaanza maisha yake, Tulikuwa tunakoona enzi hizo CTN TV yaani we acha tu
Ulikuwa MC kwenye Harusi yangu mpaka leo nina kumbukumbu hiyo saa hiyo mwenzangu ulishaanza maisha ya majukumu long time Brother
Mungu akulaze mahala pema peponi Amin
Pole kwa Familia, Mungu awatunze watoto wako Inshaalah Amin
 
Semeni nyie..leo humu nimestaajabu mno mno!hvy kwa maisha hayya kuna mtu hajaathirika kwa namna 1 au nyingine na hili gonjwa?kwahyo sasa kila mtu ameungua..aise inakera sana..sijui wanaougua huu ugonjwa wakiona vitu km hv wanJiskiaje..!semen nyie
Ni upungufu tu wa akili wa watu wachache wenye mawazo ugando kuzani kwamba ukimwi ndio gonjwa kubwa sana linalo ua kwa haraka wakisau kwamba kuna kansa na mwngine mengi tu yanayoua haraka tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HIli ni pigo kubwa kwangu binafsi, machozi hayajakauka kutokana na misiba mingine. Gen X, hakika, ina uchungu na Ma komrade waliotangulia, na hakika hatuta wasahau.
Nenda kwa Amani Kaka wangu.
 
Mbinguni hakunaaa biaaaaaaa, tupo hapa tunakunywa biaaaaaa....Haka kawimbo Gadner na Kibonde alikaimba sana wanapomaliza Jahazi na wakitoka hapo wanaingia kitaa kunywa zao biaaaaaa.....

Dah haya banah!
I hope they were not serious. Maana kufa kama umepatwa na kimeta, bia zinasaidiaje kwa mfano?
 
Tulikosea wapi wanadamu mpk Mungu ukaamua kutuletea KIFO? Eeh baba Sijui hii niite Adhabu au niite nini lakini BABA najua unatusikia TUSAMEHE tubadilishie hii adhabu tunajaribu kuizoea lakini haizoeleki BABA,natamani miaka irudi nyuma tuweze kuongea nawewe uso kwa uso kama kina MUSA na manabii wengine ulivyokua ukiongea nao Hakika Ningesimama chini yako na kuomba ufute hiki kitu.

Mungu huna makosa kazi yako sikuzote hakuna wakuipinga lkn KIFO ni zaidi ya Adhabu baba,tuepushie tupe mbadala au maandalizi ya kukipokea lakini BABA unatushtukiza TU hutuambiii why lord? Tuonee huruma Tunaumia mioyo yetu angalia tunaishi kwa kutojiamini Maisha yanapoteza ladha, tusaidie baba Tukiwa bado hata hatujapona kidonda kingine tayari unakuja na lingine eeh BABA tufanye nini sisi?

Tupe hata ishara ya kitu unachotaka kifanyike tukifanye tu ili utuondolee hiki kitu KIFO tuonyeshe hata ishara baba tufanye nini ili tukusahaulishe maumivu tuliyokusababishia huko nyuma kiasi cha kutuacha na adhabu kali na kubwa isiyozoeleka kama hiii,bado ni mtihani mzito mbele yetu BABA .

DEAR GOD,hear my PRAYERS.
Pole sana mkuu kwa uchungu unaopitia, ila kuhusu binadamu kufa hiyo ni nature tu, mzungu/mwarabu alijaribu kutuhadaa kuwa kuna maisha baada ya kifo, its just fiction...
 
Pole sana mkuu kwa uchungu unaopitia, ila kuhusu binadamu kufa hiyo ni nature tu, mzungu/mwarabu alijaribu kutuhadaa kuwa kuna maisha baada ya kifo, its just fiction...
Acha kudhihirisha ujinga wako ww, kwani maisha baada ya kifo hayapo?
Yapo sana ila inaegemea kama utaenda kwa shetani au kwa Mungu
 
Mtoto mkubwa wa kibonde jana usiku alipokua anaupokea mwili wa baba yake airport dar
52736515_2058671544214938_6615203461086068734_n.jpg
52813662_617945511980148_7014411571712664566_n.jpg
 
Back
Top Bottom