Mtangazaji wa kituo cha Citizen TV, Swaleh Mdoe ametangaza kuuza figo ili aweze kulipa madeni yanayomkabili

Mtangazaji wa kituo cha Citizen TV, Swaleh Mdoe ametangaza kuuza figo ili aweze kulipa madeni yanayomkabili

Mjue mwanahabari na muandishi wa vitabu kadhaa: Salehi Mdoe: toka kuwa mwandishi wa gazeti la chama tawala KANU la Kenya times, pia gazeti la the standard, kisha kujiunga na BBC African service London, kurejea tv ya ntv nation ....mpaka mhariri mkuu, makala zake ktk gazeti la Express Tanzania, citizen tv Kenya ....nchini Kenya watu hawapendi kujisomea vitabu, wanapenda habari za udaku. ..

 
Umeona eeh? Wanajuana kwa vilemba, wazee wa kuchuna ngozi! Dah, ni siku nyingi, enzi zile nikiwa shule msingi, yaani mtoto mdogo tu, hayo mambo yalikuwa yanatutisha si haba. Walikuwa wanadakana na yale matrela ya Tz yakielekea Namanga. Yalikuwa yakisimama tu barabarani hapo singonji kuona yatakayojiri! Nduki! Niliziogopaga zaidi ya vibwengo! 😀
Unamaanisha mliambiwa trela za Tz zinawasomba mkachunwe ngozi, issue za uchunaji ngozi mlizisikia?
Ilikuwa balaaa mbaba.
 
Unamaanisha mliambiwa trela za Tz zinawasomba mkachunwe ngozi, issue za uchunaji ngozi mlizisikia?
Ilikuwa balaaa mbaba.
Kweli jombaa, hiyo ndo ilikuwa 'monkey under the bed' kwangu nikiwa darasa la kwanza na shule ya chekechea. Ilinitisha si mchezo! Yaani kuvuka barabara wakati naenda au kutoka shuleni ilikuwa ni kama movie ya horror. Trela ikisimama karibu na anga zangu, nduki, hata sikujali kama natoroka nikielekea shuleni, wakati wa kurudi nyumbani, au ndo nelekea home wakati ni asubuhi tu! Tulikuwa tunaambiwa hao jamaa wa trela wakikudaka tu, wewe kwishney! Unajipata Tz bila ngozi. 😀😀 Hayo mambo yalitufikia sisi ambao tulikuwa tunaishi karibu na mpaka wa Tz. Hehehe, 😀😀😀 dah, miaka inasonga kwa kasi sana!
 
Ukiwa hauna pesa unaweza ukajiona wewe ndiye mtu mwenye matatizo pengine kuliko watu maarufu unaowaona kila siku kwenye runinga au kuwasikiliza redioni, lakini ukweli ni kwamba maisha hayapo hivyo kila mtu anachangamoto zake. Hii imedhihirishwa na mtangazaji nguli wa kituo cha Citizen TV, Swaleh Mdoe ambaye ametangaza kuuza figo yake moja ili aweze kulipa madeni yanayomkabili.

Swaleh Mdoe ambaye amejipatia umaarufu nchini Kenya kupitia kipindi cha ‘Tafakari na Babu’ cha Citizen TV kinachoruka kwa lugha ya kiswahili amesema anauza figo yake kwa shilingi milioni 1 za Kenya ambayo sawa na milioni 23 za kitanzania.

Msomaji huyo nguli wa taarifa ya habari ya Citizen TV leo Ijumaa Februari 16, 2018 akifanya mahojiano na kituo cha Radio cha Ghetto FM cha Jijini Nairobi nchini Kenya, amesema kuwa kwa sasa yupo katika mtikisiko wa kiuchumi kwani anadaiwa fedha nyingi ndiyo maana amechukua maamuzi hayo.

Nimejitafakari kwa kina mimi na daktari wangu hadi kuchukua maamuzi ya kutangaza kuuza figo yangu moja, Kuna mambo hayapo sawa kiuchumi kwa upande wangu nataka niyamalize mwenyewe hivyo natangaza kuuza figo yangu kwa yeyote anayehitaji asisite kunitafuta kupitia 0722-733130. Nataka nifanye hili haraka na nitatoa matangazo mengine kwenye magazeti,“amesema Swaleh Mdoe.

Hata hivyo, amesema ingawaje ni mtu maarufu nchini Kenya hataki kutangaza michango watu wamchangie kwani anaona atawabunguzi watu ambao hawahusiki na madeni hayo.

Sitaki kuwabughuzi watu wengine kwa sababu ya umaarufu wangu, nadhani figo moja inatosha kulipa madeni yangu yote na mwili wangu utakuwa na afya kama nilivyo sasa,“amesema Mdoe na kuwataka Wakenya wenye matatizo ya uhitaji wa figo wamtafute.


Bongo 5
Aisee ni hatari sana.Kuna haja ya wadau kudonate chochote kabla Bw.Mdoe hajafikia maamuzi hayo.
 
Tusisikitike maana figo anayo toa inakwenda kuokoa maisha ya MTU fulani
 
Back
Top Bottom