Mtangazaji wa redio hajui kazi ya Baraza la Mitihani la Taifa NECTA

Mtangazaji wa redio hajui kazi ya Baraza la Mitihani la Taifa NECTA

Kiukweli hana hanachojua huyu bwana kuhusu elimu, ni mfinishaji tu ndio hawa wanaoleta migogoro katika jamii yetu, kwanza sikuwa nimefurahia jinsi alivokuwa anamsakama Dr. Ndalichako as if anauomvi nae...

Hivi elimu yake ikoje...?
 
Adam Mchomvu a.k.a Balozi, PJ, Kibonde, wanajikomba kwa Magamba.Tena kuna Mdogo wangu Arnold Kayanda nilimwacha Form 1 pale Bugene Secondary na Matokeo yake ya Form Four aliibuka na Division zero leo nae ni Mtangazaji hapo Clouds FM na kuna siku huwa anatangaza Matukio ya Wiki pamoja na George Njogopa. Hii Redio ni ya Wajinga, Walevi na Wanzinzi like Diva and others.
 
Ndo matatizo ya watu kukurupuka pasipokujua kisa tu wana direct access kwenye media, mbaya zaidi unakuta analiongelea kiushabiki

Usipoteze muda wako bure kuwajadili watu ambao vichwa vyao vimejaa sifuri sifuri sifuri! GH hajui lolote anakurupuka tu! Unamkuta amekazania issue ambayo haielewi. Siku moja akiwa anatangaza alitafsiri shirika la OXFAM kama shamba la ng'ombe!
 
Adam Mchomvu a.k.a Balozi, PJ, Kibonde, wanajikomba kwa Magamba.Tena kuna Mdogo wangu Arnold Kayanda nilimwacha Form 1 pale Bugene Secondary na Matokeo yake ya Form Four aliibuka na Division zero leo nae ni Mtangazaji hapo Clouds FM na kuna siku huwa anatangaza Matukio ya Wiki pamoja na George Njogopa. Hii Redio ni ya Wajinga, Walevi na Wanzinzi like Diva and others.

Hapo mkuu naona wanajikomba kwa Waislam
 
Binafsi Gerald Hando huwa namkubali sana kama mtangazaji makini katika ile radio ukilinganisha na yule NANILIU mropokaji ropokaji...Ila kwa hili kateleza.....
 
Huyu sidhani kama alifaulu Form IV

IMG_0458.JPG
 
Necta hawawezi kuepuka hili kwani haya matokeo yanawalakini sababu hata wanafunzi ambao walikuwa na uwezo mzuri wamepigwa chini
Yes, mitihani ilikuwa inaibiwa, mwaka huu NECTA wamebana, ndio maana hakuna 1 ya 7 points
 
Hivi kama taifa tunayo sera ya habari na mawasiliano inayoeleweka? Kuna vigezo vyovyote vinasimamia uendeshaji wa vipindi kama hivi? Watoto wetu wanapofeli tunashangaa nini? Watapataje maarifa kama walimu wao,watangazaji wa redio/tv na waandishi wa habari wengi ni hawa waliofeli?!
 
Nimemsikiliza asubuhi hii mtangazaji wa kipindi cha power breakfast Gerald Hando kwenye jicho la ng'ombe anataka katibu mkuu wa baraza la mitihani aueleze umma wa watanzania kwa nini wanafunzi wamefeli. Nikajiuliza hivi anajua kazi ya hili baraza si kuwaandaa wanafunzi kwa mujibu wa mitahala hili wafanye mitihani yao na kufaulu bali ni kutunga mitihani, kusahihisha, kutoa majibu na kutoa vyeti.

Sasa katibu mkuu atajuaje kama wanafunzi wameandaliwa vizuri kwa kuwa hii ni kazi ya taasisi nyingine yaani shule ndizo zenye wajibu wa kazi ya kuwandaa wanafunzi. Shule nazo zina mambo mengi walimu vifaa, miundombinu maslahi ya walimu, maabara nk. Sasa mwenye jukumu la kuhakikisha haya yote yanapatikana ni serikali ili mwanafunzi pate maandalizi mazuri afaulu mtihani uliondaliwa na NECTA.

Unakaa kwenye redio untaka mwenye jukumu la kutunga aeleze matatizo ya maandalizi ya wanafunzi kufanya mitihani. Nina wasiwasi na uwezo na uelewa na pia elimu ya huyu jamaa anaropoka bila kufikiri

Siyi hando tu. Mnae pasco humu ndani nae hajui baraza la mitihani linafanya kaz gani. Ni wiki mbili tu zimepita mbatia alipiga kelele juu ya mitaala, si clouds si pasco walisema chochote na hawakutaka kufahamu mitaala ni nini na inaathiri vipi mwenendo mzima wa utoaji wa elimu. Leo wanalaumu baraza la mitihani, wana hakika kama walichokuwa wanafundishwa wanafunzi kwa miaka 4 kinafanana kwa shule zote nchi nzima nahata kile walichopewa baraza na wizara? .kwangu mimi kukosekana kwa mtaala ni kama kukosekana kwa mungu miongoni mwa wajenzi wa mnara wa babeli
 
Hili ndio tatizo la msingi kwa nchi yetu, badala ya kushughulikia TUNAPOJIKWAA sisi tunashughulikia TULIPOANGUKIA.
 
Binafsi Gerald Hando huwa namkubali sana kama mtangazaji makini katika ile radio ukilinganisha na yule NANILIU mropokaji ropokaji...Ila kwa hili kateleza.....
Binadamu hatujakamilika asilimia mia, hata mie wakati fulani humkubali mno. Tumsamehe na wakati mwingine anatupiwa haya majamboz.
 
Binadamu hatujakamilika asilimia mia, hata mie wakati fulani humkubali mno. Tumsamehe na wakati mwingine anatupiwa haya majamboz.
Ni kweli mkuu tatizo la kulaumu katika kila jambo ni hulka ya watanzania wengi...kosa moja hufuta mazuri 99
Anyway ukitafuta kuwa perfect sana kwenye hii dunia ni kujiongezea utumwa tuu...
 
Wao na bosi wao ndio wanahamasisha watoto kwenda kujirusha, mara ooh after school bash mara sijui fiester na makolokolo kibao
 
Necta hawawezi kuepuka hili kwani haya matokeo yanawalakini sababu hata wanafunzi ambao walikuwa na uwezo mzuri wamepigwa chini

walikuwa na uwezo mkubwa ukiwalinganisha na kina nani?? Maana isije kuwa alikuwa ni kilaza aliyekuwa na unafuu mbele ya vilaza wenzie na sasa Dr. Ndalichako ndio kawaonesha their real personalities. Maana hawa watoto wa sikiu hizi starehe mbele na elimu ipo back seat.
 
nilimsikiliza huyo kaka nikatamani nimpigie simu nikakosa namba yake. alimsema sana mama ndalichako kana kwamba yeye ndiye aliyehusika kufelisha wanafunzi. ohoo mara hujitetea kwa kutuambia vina na mashairi ya bongo falva waliyoandika wanafunzi na kadhalika. Nijuavyo mimi Necta hawahusiki kufundisha wanafunzi na hata maswali ya mitihani hutungwa na waalimu wao ambao huyachuja na kubakisha ya mtihani wa taifa.
 
Hii redio ina hazina kubwa sana ya vilaza, mbaya zaidi wanajifanya wanajua kila ki2. Huyu Kibonde hakuna asichokijua, ikitokea ya madaktari anajua kila kitu, ya wanajeshi usiseme,walimu, wanasheria, hata ile breaking news ya papa alitumia saa nzima kuizungumzia as if ndo alikuwa ametua kutoka Vatican that moment..
 
Back
Top Bottom