Wakaguongo
Member
- Sep 23, 2026
- 95
- 38
Mtangazaji wa Milele FM, Wilbroda, amemkosoa Rais William Ruto kuhusu namna anavyowasilisha hotuba zake, akimtaka kuacha kuwakumbusha watu mara kwa mara kuwa yeye ndiye Rais na Amiri Jeshi Mkuu.
Katika kauli iliyomlenga Ruto, ambaye pia humtaja kama Baba Charlene, Wilbroda amehoji kwa nini Rais hutumia mara kwa mara kauli ya “Mimi kama Rais, mimi kama Commander-in-Chief” katika hotuba zake, huku akishangaa pia kwa nini hotuba hizo zimejaa maswali mengi.
Kauli hiyo imeibua mjadala kuhusu mtindo wa mawasiliano wa Rais na matarajio ya wananchi wanaposikiliza hotuba kutoka kwa kiongozi mkuu wa nchi.
Je, unadhani viongozi wanapaswa kubadili namna wanavyowasiliana na wananchi, au matumizi ya maswali katika hotuba za Ruto ni sehemu tu ya mtindo wake wa kuwasilisha ujumbe?