Mtani wetu Simba, hii Derby haina kipengele labda ukilete wewe. Kuna Azam walikijua mapema

Powder

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2016
Posts
4,977
Reaction score
6,635
Jana wote tumeshuhudia Ma bus makubwa 2 yakitaka kuingia Uwanja wa Mkapa usiku.

Moja likiwa Bus la Simba, lingine likiwa Limejaa Wazee sijui walitoka wapi...! Makomando wa Yanga hawakuwa na tatizo na Bus la Simba, walitaka kujua lile Bus jingine la BM limewabeba kina nani..!? Walipolisogelea lile Bus wakaanza kusikia sauti za Mbuzi na Kondoo ndani ya Bus.... Mgogoro ukaanzia hapo.

Simba Ina Majeruhi 2 wa Wachezaji wa Kikosi Cha kwanza, Camara na Arteba, Wazee wakawaambia Mechi ya Leo tutafungwa lah twende tukaicheze Ile Mechi uwanjani, ikaonekana ni jambo gumu coz Watu wangeona kama wangeenda kufanya Mazoezi mida ya saa 10 jioni.

Wakapata wazo kwamba wataenda kufanya Mazoezi usiku, ili wakati wao wanazuga na Mazoezi, Wazee waendee kuicheza Mechi ya Leo wakiwa pale pale uwanjani.

Kwa vile Simba ni watu sana wanaamini Ushirikina (Rejea tu tukio la Simba kuwasha moto Mechi na Kaizer chief) na Huwa hawana aibu kufanya mambo ya Kishirikina.
Makomando wa Yanga wakakataa kuwaruhusu Simba kuingia Taifa, wakawaambia kama mnataka ingizeni Bus Moja tu lenye Wachezaji, Simba wakakataa wakisema lazima waingize na Bus la Wazee wao wakiwataja kama Mashabiki wao, Makomando wa Yanga wakasema basi Leo hamuingii humu ndani, Simba wakaamua kuondoka.

Wakaenda kufanya Kikao na Wazee wao, Wazee wakawaambia kama kesho mkipeleka Team Kwa maana ya Leo, mnaenda kufa Goli 7, na Kwa vile imeshindikana kwenda kuicheza Mechi sisi wenyewe Taifa, kesho Msipeleke Team uwanjani.

Andikeni malalamiko ili Mechi isogezwe mbele, Majeruhi wetu watakua wamepona, pia matokeo yatabadirika kutegemea na tarehe husika na siku husika...!

Wameandika Barua Bodi ya ligi, mwanzo Bodi ya ligi ilitoa msimamo kwamba Mechi lazima ichezwe, kama Kuna uvunjifu wa kanuni, Team itaadhibiwa Kwa mujibu wa kanuni, lakini Kwa vile Bodi ya ligi inaendeshwa na viongozi wengi wa Simba, wakaamua kukwepesha Kanuni.

Sasa hivi Yanga ipo Taifa inamsubiri Simba, Simba wasipokuja Yanga wanataka point zao 3 na magoli 3.... Wameshasema kama SI Leo hawatacheza Mechi na Simba kwenye Mechi zilizobaki.

Ugomvi ambao Bodi ya ligi wameuanzisha Kwa kukwepesha Kanuni na kusogeza Mechi mbele, hawana uwezo wa kuumaliza Wala TFF haiwezi zaidi ya kupiga Yanga point 3, lah..... Ugomvi utaenda kumalizwa CAF ama FIFA.

Azam inabidi watueleze na kibwagizo Chao Cha matangazo ya Derby....kwamba...

"Hii Derby Haina Kipengele Mtani, Kipengele labda ukilete wewe.....!
Kususia Mechi ya hii kulipagwa zamani.
 
Ila hapa naona kama hiyo bodi ya ligi ndio imejaa wapumbavu.
Huwezi ghairi mechi kipumbavu namna hiyo tena masaa machache kabla ya mechi.
Ushauri wangu kwa Yanga ni kwamba kama wasipocheza mechi leo, wagome wasicheze tena. Sijaona sababu zenye mashiko zimetolewa
 
Huwezi ghairi mechi kipumbavu namna hiyo tena masaa machache kablabya mechi.
Ushauri wangu kwa Yanga ni kwamba kama wasipocheza mechi leo, wafome wasicheze tena. Sijaona sababu zemye mashiko zimetolewa
Sahihi kabisa, na kanunuzi zipo Wazi... Bodi ya ligi Kuna watu Huwa hawatumii Akili zao.... Ni Wapuuzi sana.
 
Usitujumuishe na wengine kwenye ujinga wako.

Huo ushuhuda umeushuhudia wewe na hao mabaunsa wenu.
Sasa Kama unaishi Mpwapwike na kisimu Cha Tochi na mbs za kuunga sio tatizo langu, Mimi nimetizama live video Jana ya tukio Zima.
 
Mimi sio shabiki kindaki ndaki wa mpira lakini kwenye hili suala mashabiki inabidi na wao waoneshe msimamo wao. Wanachotakiwa kufanya ni kutokuingia uwanjani siku mpya ya mechi (itakayopangwa na bodi).

Naamini kuna viongozi wa mashabiki wa hivi vilabu viwili, watoe msimamo wao kuwa pesa walizolipia kwenye mchezo huu zitumike kwenye michezo mingine ila sio mchezo mpya wa Yanga na Simba.

Wacheze wenyewe uwanjani bila mashabiki na mapato ya uwanjani ili liwe funzo waache kucheza na akili na pesa za mashabiki. Tofauti na hivyo hivi vilabu na hao TFF/Bodi hawataacha huu ujinga kamwe!
 
Jana wote tumeshuhudia Ma bus makubwa 2 yakitaka kuingia Uwanja wa Mkapa usiku.

Moja likiwa Bus la Simba, lingine likiwa Limejaa Wazee sijui walitoka wapi...! Makomando wa Yanga hawakuwa na tatizo na Bus la Simba, walitaka kujua lile Bus jingine la BM limewabeba kina nani..!? Walipolisogelea lile Bus wakaanza kusikia sauti za Mbuzi na Kondoo ndani ya Bus.... Mgogoro ukaanzia hapo.

Simba Ina Majeruhi 2 wa Wachezaji wa Kikosi Cha kwanza, Camara na Arteba, Wazee wakawaambia Mechi ya Leo tutafungwa lah twende tukaicheze Ile Mechi uwanjani, ikaonekana ni jambo gumu coz Watu wangeona kama wangeenda kufanya Mazoezi mida ya saa 10 jioni.

Wakapata wazo kwamba wataenda kufanya Mazoezi usiku, ili wakati wao wanazuga na Mazoezi, Wazee waendee kuicheza Mechi ya Leo wakiwa pale pale uwanjani.

Kwa vile Simba ni watu sana wanaamini Ushirikina (Rejea tu tukio la Simba kuwasha moto Mechi na Kaizer chief) na Huwa hawana aibu kufanya mambo ya Kishirikina.
Makomando wa Yanga wakakataa kuwaruhusu Simba kuingia Taifa, wakawaambia kama mnataka ingizeni Bus Moja tu lenye Wachezaji, Simba wakakataa wakisema lazima waingize na Bus la Wazee wao wakiwataja kama Mashabiki wao, Makomando wa Yanga wakasema basi Leo hamuingii humu ndani, Simba wakaamua kuondoka.

Wakaenda kufanya Kikao na Wazee wao, Wazee wakawaambia kama kesho mkipeleka Team Kwa maana ya Leo, mnaenda kufa Goli 7, na Kwa vile imeshindikana kwenda kuicheza Mechi sisi wenyewe Taifa, kesho Msipeleke Team uwanjani.

Andikeni malalamiko ili Mechi isogezwe mbele, Majeruhi wetu watakua wamepona, pia matokeo yatabadirika kutegemea na tarehe husika na siku husika...!

Wameandika Barua Bodi ya ligi, mwanzo Bodi ya ligi ilitoa msimamo kwamba Mechi lazima ichezwe, kama Kuna uvunjifu wa kanuni, Team itaadhibiwa Kwa mujibu wa kanuni, lakini Kwa vile Bodi ya ligi inaendeshwa na viongozi wengi wa Simba, wakaamua kukwepesha Kanuni.

Sasa hivi Yanga ipo Taifa inamsubiri Simba, Simba wasipokuja Yanga wanataka point zao 3 na magoli 3.... Wameshasema kama SI Leo hawatacheza Mechi na Simba kwenye Mechi zilizobaki.

Ugomvi ambao Bodi ya ligi wameuanzisha Kwa kukwepesha Kanuni na kusogeza Mechi mbele, hawana uwezo wa kuumaliza Wala TFF haiwezi zaidi ya kupiga Yanga point 3, lah..... Ugomvi utaenda kumalizwa CAF ama FIFA.

Azam inabidi watueleze na kibwagizo Chao Cha matangazo ya Derby....kwamba...

"Hii Derby Haina Kipengele Mtani, Kipengele labda ukilete wewe.....!
Kususia Mechi ya hii kulipagwa zamani.
Screenshot_20250308-173528.jpg
 
Sasa Kama unaishi Mpwapwike na kisimu Cha Tochi na mbs za kuunga sio tatizo langu, Mimi nimetizama live video Jana ya tukio Zima.
Sasa kama umetizima ukiwa umepiga miwa na vijiti unafikiri kuna namna ungeweza kuona tofauti ya hicho ulichokiona?
 
Ila hapa naona kama hiyo bodi ya ligi ndio imejaa wapumbavu.
Huwezi ghairi mechi kipumbavu namna hiyo tena masaa machache kabla ya mechi.
Ushauri wangu kwa Yanga ni kwamba kama wasipocheza mechi leo, wagome wasicheze tena. Sijaona sababu zenye mashiko zimetolewa
Kunywa kinywaji chochote Fanton Mahal msimamo ndiyo huo, wanaahirishaje mechi masaa machache hivi, kabla ya muda wa mechi? Tena hakuna tukio kubwa la kitaifa kusema lipishe. Tutawatagisha hawa, hiyo tarehe wanayopanga wao hatutacheza. walipolalia ndipo tulipoamkia.
 
Wabongo bhana 😂
Kususa asuse simba afu kosa lionekane la Azam 😂
 
Kunywa kinywaji chochote Fanton Mahal msimamo ndiyo huo, wanaahirishaje mechi masaa machache hivi, kabla ya muda wa mechi? Tena hakuna tukio kubwa la kitaifa kusema lipishe. Tutawatagisha hawa, hiyo tarehe wanayopanga wao hatutacheza. walipolalia ndipo tulipoamkia.
Kosa Mimi naona lipo kwa Yanga wanewaruhusu simba waingie tu uwanjani na wazee wao maana hizo ndo tamaduni zetu za kiafrika
 
CCM Ndio inapenda vijana Wa Tanganyika waweke nguvu zao huko kwenye simba Na YANGA".

Great Thinker
.

Leo Tutaona Nyuzi za Simba na Yanga zaidi ya elfu 60 humu jukwaani.

TUKIWAAMBIA KUSHABIKIA SANA SIMBA NA YANGA UNAANZA KUWA MPUMBAVU HAMUELEWI.
 
Kunywa kinywaji chochote Fanton Mahal msimamo ndiyo huo, wanaahirishaje mechi masaa machache hivi, kabla ya muda wa mechi? Tena hakuna tukio kubwa la kitaifa kusema lipishe. Tutawatagisha hawa, hiyo tarehe wanayopanga wao hatutacheza. walipolalia ndipo tulipoamkia.
Na mbaa zaidi taarifa zinatolewa kwenye social media jaman, kwan hakuna utaratibu formal kutekeleza hili?
 
Kosa Mimi naona lipo kwa Yanga wanewaruhusu simba waingie tu uwanjani na wazee wao maana hizo ndo tamaduni zetu za kiafrika
Hapana kosa si la Yanga, sisi ndiyo wenyeji uwanjani ni kucheza. Tamaduni zao, wangezifanyia makao makuu yao siyo uwanjani. Hatujui na wanyama wanaenda fanya nini uwanja ambao leo tungecheza nao. Ndiyo maana walipigwa fine kwa kuwasha moto uwanjani. Wana mambo yasiyo ya kimchezo kabisa.
 
Kwahiyo mnaogopa uchawi na ushirikina .

Kama mnakikosi kizuri , mmejiandaa vizuri Ila bado mnaogopa mila na tamaduni za simba basi na nyietakuwa ndo wale wale
 
Hakuna mtu anaogopa, kwani walipopigwa faini CAF waliogopa nini? Matukio yasiyo ya kimchezo, tusiyatukuze na kuona ni ya kawaida. Hayo mambo kama timu imebobea wafanye wenyewe kwa siri huko. Ndiyo maana soka limebaki kwa timu, 2 kama si 3 tu. Kimataifa ndiyo tia maji. Tushabikie zaidi mchezo wenyewe, kuliko hayo makandokando. Tukomeshe hadharani.
 
Bantu Lady yanga ndiyo walioleta kipengele cha kuvunja kanuni kwa kuwahujumu Simba sc wasifanye mazoezi.
 
Back
Top Bottom