TANZIA Mtanzania Abraham Mgowano aliyeajiriwa na Google afariki dunia kwa kuanguka kwenye Boti na kuzama

TANZIA Mtanzania Abraham Mgowano aliyeajiriwa na Google afariki dunia kwa kuanguka kwenye Boti na kuzama

View attachment 2918748
View attachment 2918751
MAREKANI: Mwili wa Mtanzania Abraham Mgowano aliyekuwa akiishi na kufanya kazi katika Kampuni ya Google kama Mhandisi wa Programu Endeshi (Software Engineer) umepatikana ukielea katika Mto Miami jijini Florida baada ya kuanguka kwenye 'Boti'.
View attachment 2918766
Abraham aliripotiwa kupata ajali Februari 24, 2024 akiwa na wenzake 12 pamoja na Kapteni wa Boti hiyo. Polisi walianza kumtafuta kwa kutumia Boti nyingine na Helikopta bila mafanikio hadi walipopata taarifa za kupatikana kwa mwili huo ukielea Februari 27, 2024.

Kwa mujibu wa taarifa, Abraham alikuwa Mfanyakazi wa Google kwa miaka 9 baada ya kuwa mmoja wa Wanafunzi bora kutoka Chuo Kikuu cha Stanford. Baadaye aliajiriwa kama Mshauri wa Masuala ya Kompyuta chuoni hapo kwa mwaka mmoja.

Aidha, Mtanzania huyo alikuwa kati ya Wanafunzi Bora 12 waliofaulu vizuri Mtihani wa Kidato cha 4 mwaka 2007 ambapo walipata nafasi ya kukutana na kupongezwa na Rais Jakaya Kikwete.

========

The body of a California man who fell from a chartered yacht making its way up the Miami River over the weekend was found floating in the water Tuesday, according to police.

Abraham Mgowano, 35, had been missing since falling from the 44-foot Sea Ray cabin cruiser around 2:30 p.m. Saturday as it headed westbound on the river near Lummus Park.

While confirming the Berkeley, California native’s body had been found, police with the Florida Fish and Wildlife Conservation, the lead agency investigating the case, did not release details about where Mgowano’s corpse was discovered nor who found him.

The 12 other people on the boat told investigators they saw him go overboard and never resurface, according to the initial incident report released by the FWC.

The report states the boat operator, Eddy Espinosa Hernandez, 39, was a captain hired by the passengers. He could not be reached for comment. Police noted in their report that he “showed no signs of impairment.”

The Coast Guard suspended its search for Mgowano around 8:15 p.m. Saturday after finding no signs of him.

The hunt on the river spanned from the Flagler Street and 7th Avenue bridges, as well as the nearby coastline, said Petty Officer 2nd Class Diana Sherbs, a Coast Guard spokeswoman.

Fish and Wildlife officers and officers with the city of Miami and Miami-Dade County continued their search this week.

“Our thoughts are with Mr. Mgowano’s friends and family during this difficult time,” the FWC said in a statement. “This is an active investigation.”

CBS NEWS
...[emoji26]...Hakuna Mchezo mchafu kweli Hapo ? Watu 12 Wakishinda kumuokoa mwenzao mmoja ?....[emoji848]
 
Stori yake ni sawa na ile ya mwanariadha wa Kenya Kelvin Kiptum Cheruiyot aliyefariki kwenye ajali ya gari, Very young kabla hajafaidi matunda ya kazi yake...

Graveyard is full of unaccomplished dreams...
Hii habari imenisikitisha sana sana😭😭
 
Pole kw Tz yetu ila Ukweli ni kwamba hiyo Ndio michongo ya wazungu wanapenda killing za ndani ya maji, eneo la maji.maana uchunguzi unakuwa mgum kinoma hivyo ndio njian rahisi kwao ukienda ulaya au kwa wanzungu epuka kwenda nao kwenye mito au baharini kama huna blacks wezako na watu unao waamini sana.
Na usipokee ushauri unao letwa Twende tukatalii sehemu flan amua kwa utashi wako. Ustoe Ratiba zako za matembezi , wazungu wana hila kinoma ila wanatumia Akili nyingi ..ogopa mtu anakuchekea kila siku ila ana lake analokupangia kwa siri ila ana subiri tu uingie kwenye kupatwa kwa mwezi.yani mkakati ulenge kwenye eneo huska.
La sivyo kuzamishwa ni Dakika chache tu na hakuna Cha finger print wala nn....Hapo
Mwamba walimlia rada siku nyingi hata hiyo safari Huenda walileta wazo naye akakubali kwenda kutalii bila kujua.
Na pia Lazma wakuleweshe kwanza kabla ya tukio.
..Hizo ngozi nyeupe nazijua wana wivu ila hawalogi😄..unaliwa Timing kuliko Paka anavyo Fanya kwa panya ....Paka Anaweza kukeshasha juu ya shimo la panya au njia anayopita panya.. akifanya kutoka tu au kupitia Hilo eneo Anao..imeisha hiyo. Ndivyo na hao Racist walivyo.

Miafrika bana. Akili zimekabaa backwards tu. Sababu za kijinga jinga kama hizi ndo serikali zenu zinatoa kuwachota akili badala ya uwajibikaji.
 
Mliokuwa mnauliza tanzania one wako wapi? Majibu yanakuja polepole
80% ya waalimu vyuo vikuu, taasisi za serikali, mashirika ya kimataifa na makampuni binafsi hasa hasa zile idara zinazohitaji vichwa vilivyotulia kama utafiti mara nyingi sana huwa utawakuta wanafunzi waliofanya vizuri sana kitaifa.

Nakumbuka pale benki kuu (BoT) kurugenzi ya uchumi na utafiti iliwahi kuwa na wachumi pamoja na wataalamu wa fedha zaidi ya 30
ambao miaka yao walipokuwa wanamaliza f6 walikuwa wanafunzi bora kitaifa kuanzia mwaka 1989 (John Mtui) mpaka 2006 (Mosses Mwizarubi).
 
Naona player haters washaanza kuwasigolea [emoji1]

Ova
Ndio hivyo mkuu, wabongo wengi wao wana roho za husda, na wanajua kubeba box basi ni hizo kazi tu na kusikia huyo alikua Google basi wanaona ndio alikua top of all the people in USA. Hawajui kua kuna watu wanafanya kazi kwenye mashirika makubwa hata huko africa hawayajui na wanalipwa mpunga wa kutosha. Na wamekazana ooh rudi bongo, ukiwauliza bongo kuna nini ?? hamna kitu hawajui wengine tuliondoka kuja kuishi ughaibuni.Kuendesha magari na nyumba tumejenga kitambo sana na pesa za Long room.
RIP Mgowano.
 
Nikawaida na desturi ya sisi waTanzania kutoa mkono wa pole mkuu, kama huko kwenu Canada hamna utaratibu huo basi nisawa.
Nashukuru kunitabiria U Canada ingawa siutaki uraia wa Canada. Bado sijatoka nje ya bara la Afrika mkuu, ila naamini "one day yes". Canada lazima nifike.

Weka namba yako ya simu "watakaoguswa" wakarushie chochote. Watakaoguswa tu lakini. Mimi niondoe kwenye listi ya "watakaoguswa"
 
Walikua watundu na walikua na ushirikiano sana

Kwa jinsi wasivyopenda makuu wale wazazi wao nadhani bado watakua wanakaa pale pale kimara kwa bondeni,japo wana nyumba kadhaa

Ila wale watoto wana maisha yao mazuri na majumba yao na wote ni computer engineers,jamaa wa Google ndio hela ilikua ishaanza kumiminika bahati mbaya ndio hivyo tena

Kwa huu msiba I really feel sorry for them

I remember genius Abraham kamaliza Stanford familia nzima ikaja America kumsapoti mtoto wao na leo ndio kawatoka tena

I wonder kama mtu alikua na beef na marehemu itakua ni maajabu maana jamaa alikua mkimya sana na very respectiful...cha ajabu hii dunia wenye akili na maana ndio wanakufaga tunabaki sisi wasumbufu
Kimara sehemu gani Mkuu??
 
Back
Top Bottom