Mtanzania aingiza kitabu chake soko la WALMART Marekani

Mtanzania aingiza kitabu chake soko la WALMART Marekani

SANGAPIPI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
206
Reaction score
301
Kutoka kwa Yericko

Habari njema kwangu na kwa Watanzania nikuwa Kitabu chetu pendwa cha Ujasusi baada ya kuingia makubaliano na kampuni ya Kindle Publishers ili wauze kitabu kupitia amazon.com miaka mitano iliyopita,

Sasa kimekubalika na kuingizwa kwenye soko la makampuni makubwa sita ya uuzaji wa vitabu duniani ambayo ni WALMART kupitia link hii hapa Verify your identity

Kampuni ya tatu nyingine iliyoruhusu Kitabu cha Ujasusi kuingizwa na kuuzwa katika soko lake ni BARNES AND NOBLE kupitia link hii hapa Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi|Paperback

Kampuni ya nne nyingine iliyoruhusu Kitabu cha Ujasusi kuuzwa katika soko lake la kimataifa baada ya kujiridhisha ubora na upekee wa kitabu hiki ni THRIFT BOOKS kupitia link hii hapa chini Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi (Afrikaans... book

Kampuni ya tano nyingine iliyoruhusu Kitabu cha Ujasusi kuuzwa katika soko lake la kimataifa baada ya kujiridhisha ubora na upekee wa kitabu hiki ni BOL kupitia link hii hapa chini bol.com | Ujasusi Wa Kidola Na Kiuchumi, Yericko Nyerere | 9789976993608 | Boeken

Kampuni ya sita nyingine iliyoruhusu Kitabu cha Ujasusi kuuzwa katika soko lake la kimataifa baada ya kujiridhisha ubora na upekee wa kitabu hiki ni TANUM kupitia link hii hapa chini Ujasusi Wa Kidola Na Kiuchumi

Kampuni nyingine ya saba ambayo nayo imeruhusu Kitabu cha Ujasusi kuuzwa katika soko lake la kimataifa baada ya kujiridhisha ubora na upekee wa kitabu hiki ni EBAY kupitia link hii hapa chini

Kwa wale msiojua kitabu cha mtu ili kiuzwe na kampuni kama Walmart ni mziki mrefu kinatakiwa kitabu hicho kiwe katika ubora wa kimataifa na mwandishi awe alitulizana wakati wa kuandika. Vitabu vinavyouzwa katika masoko hayo hupitia hatua nyingi ndipo viruhusiwe.

Haya yanaweza kuonekana ni mafanikio yangu binafsi, lakini katika tafsiri haya ni mafanikio ya Taifa la Tanzania, ni mafanikio ya Afrika, ni Mafaniko ya Lugha ya Kiswahili. Ni mafaniko dhidi ya ujasuri na uthubutu.

Asanteni sana wadau wote mlioshiriki kwa namna yoyote ili kunifikisha hapa. Miaka mitano ya kukisafirisha kitabu hiki hadi soko la kimataifa ilikuwa migumu na yenye vikwazo vingi sana.

WAHI OFA MAALUMU.

1. Kitabu: Mtu baada ya Mtu, OFA ni 20,000 badala ya 80,000/=

2. Kitabu: Ujasusi, OFA ni 20,000 badala ya 80,000/=

Nunua kwa:

TigoPesa 0715865544
M-Pesa 0755865544
Airtel Money 0788887887
HaloPesa 0624452045
(Yericko Nyerere)

Tuma majina yako na ulipo

(Dar ni free delivery)

Nje ya Dar nauli 8,000/=

Instagram Follow @yerickonyerere
 
Kutoka kwa Yericko

Habari njema kwangu na kwa Watanzania nikuwa Kitabu chetu pendwa cha Ujasusi baada ya kuingia makubaliano na kampuni ya Kindle Publishers ili wauze kitabu kupitia amazon.com miaka mitano iliyopita...
Safi sana. Tumechoka vile vitabu ...... maisha yangu....
Uzinduzi ni mpaka derby iahirishwe!
 
Kutoka kwa Yericko

Habari njema kwangu na kwa Watanzania nikuwa Kitabu chetu pendwa cha Ujasusi baada ya kuingia makubaliano na kampuni ya Kindle Publishers ili wauze kitabu kupitia amazon.com miaka mitano iliyopita...
Makulilo miaka zaidi ya kumi marekani bado kiingereza cha kuungaunga, buku, about, this hahahaha
 
Kwanza hongera kwa Yericko Nyerere kuweza kufika ngazi hivyo ya soko.

Je kinapatikana ktk lugha ya Kiingereza ili wigo wa wasomaji uongezeke? Kama sivyo fanya hima kipatikane ktk chapisho sanifu cha hiyo lugha nyingine ya kimataifa ya English.
 
Mbona vimo vingi vya watanzania wengine? Hata hivyo, kuingiza kitabu walmart hakumnufaishi mtungaji kama mnavyodhani. Hawa ni matapeli wa kawaida sawa na wengine wengi wanaouuza vitabu online.

Namfahamu mwandishi maarufu ambaye vitabu vyake vijaa online lakini analalamika hawamlipi chochote. Nadhani mleta uzi hajui biashara ya vitabu.

Ni mawazo yatokanayo na uzoefu tu. Hebu fuatilia link hii hapa Verify your identity
 
Kutoka kwa Yericko

Habari njema kwangu na kwa Watanzania nikuwa Kitabu chetu pendwa cha Ujasusi baada ya kuingia makubaliano na kampuni ya Kindle Publishers ili wauze kitabu kupitia amazon.com miaka mitano iliyopita,
Ni kitabu cha kiswahili lakini bei ya yake ni mara kumi ya vitabu maarufu kama vifuatavyo:

1623026979748.png

1623027123486.png

1623027187810.png

1623027259207.png

1623027415027.png

1623027536848.png

1623027625406.png
 
Ni kwamba asiwe na tamaa ya kuweka bei kubwa wakati wasomaji wake ni hawa hawa wabeba boksi na walala hoi kama mimi iwapo wenye vitabu vinavyosomwa na wenye uwezo hawachaji bei kubwa hivyo.
Kwa taarifa yako, mtunzi hapangi bei bali wachapishaji na washitiri wao kama vile Walmart.
 
Kwa taarifa yako, mtunzi hapangi bei bali wachapishaji na washitiri wao kama vile Walmart.

Inawezekana wewe hujawahi kuingia kwenye hiyo industry ya kpublish vitabu kwa hiyo unadhani bei inapangwa na walmart au publisher. Kuna vitabu vinachukua rasmilali nyingi sana za mtunzi wake na huwezi kuvipata kwa bei ya chini; mtunzi anakusanya data kwa kusafiri sehemu mbalimbali ili kukamilisha kitabu hicho.

Kitabu cha namna hiyo siyo sawa na kitabu ambacho mtu anakaa na kuweka mawazo yake pamoja kama kitabu. Kabla wale jamaa hawajapanga bei zao hutaka kujua kuwa mtunzi anasema nini; na mara zote bei zao ni kama 10-15% tu ya bei ya mtunzi, plus tax na gharama za shipping and handling!!
 
Hongera sana kwa watanzania wachache wanaofanya vitu duniani kama mimi na wengine.
Mitano tena ingekuwepo Hapa kazi tu ingeendelea na kazi iendelee
Nnje ya mada kidogo



1623041904276.png



Nakukumbusha tu

1. "Pema usijapo pema, ukipema si pema tena"

2. "Mwenda juu kipungu, hafikilii mbinguni"

3. "Mwenda tezi na omo marejeo ngamani"
 
Huyu itakuwa ni Mtanzania wa pili baada ya Gwajima na kitabu chake cha Kijapani!!
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Back
Top Bottom