Mtanzania aingiza kitabu chake soko la WALMART Marekani

Mtanzania aingiza kitabu chake soko la WALMART Marekani

Tapeli mwenye macho makavu. Sijui ni ujasiri wa bange au vipi🤣
 
Kwanza hongera kwa Yericko Nyerere kuweza kufika ngazi hivyo ya soko.

Je kinapatikana ktk lugha ya Kiingereza ili wigo wa wasomaji uongezeke? Kama sivyo fanya hima kipatikane ktk chapisho sanifu cha hiyo lugha nyingine ya kimataifa ya English.
Asante sana mkuu nitafanyia kazi jambo hili mapema
 
Huyu itakuwa ni Mtanzania wa pili baada ya Gwajima na kitabu chake cha Kijapani!!
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji125][emoji125][emoji125]
Hahahaa daaah
 
Nnje ya mada kidogo



View attachment 1810949


Nakukumbusha tu

1. "Pema usijapo pema, ukipema si pema tena"

2. "Mwenda juu kipungu, hafikilii mbinguni"

3. "Mwenda tezi na omo marejeo ngamani"
Dah!!! Umekuja kunisaka na huku mkuu
Kwa nini yasiishie kule?
 
Hongera sana kwa kuweza kuandika kitabu...hongereni pia na walioweza kusoma..hongera sana...mimi nitavinunua naimani pengine wanangu watapewa kipaji cha kusoma...
 
Kutoka kwa Yericko

Habari njema kwangu na kwa Watanzania nikuwa Kitabu chetu pendwa cha Ujasusi baada ya kuingia makubaliano na kampuni ya Kindle Publishers ili wauze kitabu kupitia amazon.com miaka mitano iliyopita,

Sasa kimekubalika na kuingizwa kwenye soko la makampuni makubwa sita ya uuzaji wa vitabu duniani ambayo ni WALMART kupitia link hii hapa Verify your identity

Kampuni ya tatu nyingine iliyoruhusu Kitabu cha Ujasusi kuingizwa na kuuzwa katika soko lake ni BARNES AND NOBLE kupitia link hii hapa Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi|Paperback

Kampuni ya nne nyingine iliyoruhusu Kitabu cha Ujasusi kuuzwa katika soko lake la kimataifa baada ya kujiridhisha ubora na upekee wa kitabu hiki ni THRIFT BOOKS kupitia link hii hapa chini Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi (Afrikaans... book

Kampuni ya tano nyingine iliyoruhusu Kitabu cha Ujasusi kuuzwa katika soko lake la kimataifa baada ya kujiridhisha ubora na upekee wa kitabu hiki ni BOL kupitia link hii hapa chini bol.com | Ujasusi Wa Kidola Na Kiuchumi, Yericko Nyerere | 9789976993608 | Boeken

Kampuni ya sita nyingine iliyoruhusu Kitabu cha Ujasusi kuuzwa katika soko lake la kimataifa baada ya kujiridhisha ubora na upekee wa kitabu hiki ni TANUM kupitia link hii hapa chini Ujasusi Wa Kidola Na Kiuchumi

Kampuni nyingine ya saba ambayo nayo imeruhusu Kitabu cha Ujasusi kuuzwa katika soko lake la kimataifa baada ya kujiridhisha ubora na upekee wa kitabu hiki ni EBAY kupitia link hii hapa chini

Kwa wale msiojua kitabu cha mtu ili kiuzwe na kampuni kama Walmart ni mziki mrefu kinatakiwa kitabu hicho kiwe katika ubora wa kimataifa na mwandishi awe alitulizana wakati wa kuandika. Vitabu vinavyouzwa katika masoko hayo hupitia hatua nyingi ndipo viruhusiwe.

Haya yanaweza kuonekana ni mafanikio yangu binafsi, lakini katika tafsiri haya ni mafanikio ya Taifa la Tanzania, ni mafanikio ya Afrika, ni Mafaniko ya Lugha ya Kiswahili. Ni mafaniko dhidi ya ujasuri na uthubutu.

Asanteni sana wadau wote mlioshiriki kwa namna yoyote ili kunifikisha hapa. Miaka mitano ya kukisafirisha kitabu hiki hadi soko la kimataifa ilikuwa migumu na yenye vikwazo vingi sana.

WAHI OFA MAALUMU.

1. Kitabu: Mtu baada ya Mtu, OFA ni 20,000 badala ya 80,000/=

2. Kitabu: Ujasusi, OFA ni 20,000 badala ya 80,000/=

Nunua kwa:

TigoPesa 0715865544
M-Pesa 0755865544
Airtel Money 0788887887
HaloPesa 0624452045
(Yericko Nyerere)

Tuma majina yako na ulipo

(Dar ni free delivery)

Nje ya Dar nauli 8,000/=

Instagram Follow @yerickonyerere
View attachment 1810853
Safiii
 
Back
Top Bottom