Mtanzania akamatwa kwa madawa ya kulevya thamani ya shilingi 7.8 bilioni

Ukiona Mbongo kakamatwa SA, ujue Mbongo mwenzake katoa Mchongo Kwa Police.

Habari hii imegonga vichwa vya habari katika vyombo vyote vikubwa tajwa mahiri South Africa, na nchi yetu kuonekana baadhi ya raia wake ni vigogo wa biashara hii.
 
Kutafuta hakuna dini mkuu ukitaka kuamini viongozi wa kibongo wanaapishwa wameshika misahafu lakini hao hao ndiyo wezi wakubwa duniani hakuna.
Na wanapiga Hela kinoma 🤣🤣

Vile viapo ni unafki tu
 
Naomba asiwe na jina la kigalatia. Yani sijui tutaficha wapi sura zetu?

hydroxo adriz Mufti kuku The Infinity
Wewe jamaa. Hii mijadala unayoleta kwa kutumia UDINI siyo mizurii ila sijui lengo lako ninini? Haya mambo ya ugalatia yanatoka wapi mkuu??
Msilete udini kwenye hii nchi ni hatar sana. Tunaweza kujadiliana bila kutaja dini zetu ndo mana hata majina hapa hatujuani
 
Mbona awajataja majina ya mtanzania na huyu mrundi
 
Saturday, January 10, 2026

TANI 9 ZA DAWA ZA KULEVYA ZAKAMATWA NCHINI TANZANIA​


View: https://m.youtube.com/watch?v=O9h4gtVG0EETANI 9 ZA DAWA ZA KULEVYA ZAKAMATWA NCHINI TANZANIA, BASI LA KING MASAI LANASWA
*Raia wa Kenya akamatwa akitumia biashara ya chai kuficha uuzaji wa dawa za kulevya.
*Basi la King Masai linaswa likisafirisha skanka.
*Mirungi iliyofungwa kama majani ya mwarobaini yakamatwa.
*Watumishi wa serikali wanaswa wakihusishwa na usafirishaji wa dawa za kulevya.


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imetekeleza operesheni maalum mwishoni mwa mwezi Desemba 2025 na kufanikiwa kukamata jumla ya kilogramu 9,689.833 za dawa za kulevya, sawa na tani 9. Pia pikipiki 11 na magari matatu yamekamatwa, huku watuhumiwa 66 wakitiwa mbaroni kwa tuhuma za kuhusika na biashara hiyo haramu.

Katika operesheni iliyofanyika Sinza C, mtaa wa Bustani, nyumba namba 16 jijini Dar es Salaam, Jefferson Kilonzo Mwende mwenye umri wa miaka 35, raia wa Kenya, alikamatwa akiwa na gramu 131.88 za heroin. Uchunguzi umebaini kuwa mtuhumiwa huyo, ambaye aliishi Tanzania tangu mwaka 2023, alikuwa akitumia biashara ya kuuza chai kama kificho cha kuendesha mtandao wa uuzaji wa dawa za kulevya.

Katika eneo la Wailes, Temeke jijini Dar es Salaam, mamlaka ilikamata pakiti 20 za skanka zenye uzito wa kilo 20.03, zilizokuwa zimefichwa ndani ya balo la nguo za mitumba na kusafirishwa kwa basi aina ya Scania la kampuni ya King Masai Tours, lenye namba za usajili AAM 297 CA kutoka Msumbiji.

Basi hilo hufanya safari kati ya Nampula nchini Msumbiji na Tanzania. Watuhumiwa waliokamatwa ni Amasha Iddi Mrisho mkazi wa Buza, Dar es Salaam, pamoja na Seleman Juma Ally, raia wa Msumbiji.

Katika Kinyerezi, mtaa wa Majoka wilayani Ilala, watuhumiwa watatu Erick Ernest Ndagwa, Paul Blass Henry na Tido Emmanuel Mkude walikamatwa wakiwa wanasafirisha bangi yenye uzito wa kilo 193.66 kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam.

Kadhalika, kupitia ukaguzi uliofanyika katika kampuni za usafirishaji wa mizigo jijini Dar es Salaam, paketi 20 za mirungi zenye uzito wa kilo 9.54 zilikamatwa zikiwa zimefungwa na kufanana na majani ya mwarobaini yaliyokaushwa. Mizigo hiyo ilikuwa ikisafirishwa kutoka Kenya kuelekea Australia.

Katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Morogoro, Tanga, Lindi, Kilimanjaro, Njombe, Kigoma na Arusha, operesheni mbalimbali zilifanikiwa kukamata heroin gramu 37.34, skanka kilo 1.015, bangi kilo 7,969.98 na mirungi kilo 1,363.701. Pia mashamba ya bangi yenye ukubwa wa ekari 14 yaliteketezwa.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imesisitiza wananchi kutoa taarifa pale wanapoona viashiria vya biashara ya dawa za kulevya na kuepuka kubeba mizigo wasiyoijua. Mamlaka itaendelea na operesheni nchi nzima na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wahusika wote wa uhalifu huu.
 
Watafutaji wasioipora na kikihujumu Tanganyika kama afanyavyo Samia na genge lake, ajali kazini.
Warudi barabarani ila wamepoteza mzigo ambao sehemu kubwa polisi watauuza kwa kwa dealers wengine kwa bei mchekea, it's very likely competitors ndiyo wamewachoma na mzigo watauziwa wao kwa bei chee.
 
23 January 2026

JELA MIAKA 28 JELA KWA KUSAFIRISHA HEROINI KG 268.50​

Misalaba MediaJanuary 23, 20260


Na Mwandishi wetu.

Mahakama Kuu ya Uhujumu Uchumi, Divisheni ya Makosa ya Rushwa, imemhukumu kifungo cha miaka 28 jela mshtakiwa Isso Lomward Lupembe, baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki katika kusafirisha dawa za kulevya kiasi cha kilogramu 268.50 aina ya heroin. Mshtakiwa huyo alikuwa mshtakiwa wa kwanza kati ya watatu waliokuwa wakikabiliwa na shauri hilo la uhujumu uchumi.

Akisoma hukumu hiyo tarehe 22 Januari, 2026, Mheshimiwa Jaji Otaru Joachimu alisema mahakama imezingatia muda wa miaka mitano na miezi tisa ambao mshtakiwa amekaa rumande tangu alipokamatwa. Kutokana na hilo, mahakama imeelekeza kuwa atatumikia kifungo cha miaka 22 na miezi mitatu iliyobaki ili kukamilisha adhabu yake.

Katika hatua nyingine, mahakama hiyo imemuondolea mashtaka mshtakiwa Alistair Amon Mbele, baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake bila kuacha shaka yoyote. Mshtakiwa huyo alikuwa anashtakiwa pamoja na wenzake katika shauri la uhujumu uchumi namba ECO 36/2020.

Shauri hilo liliwahusu watuhumiwa watatu ambao ni David Kanayo Chukwu, raia wa Nigeria, Isso Lomward Lupembe, raia wa Tanzania, na Alistair Amon Mbele, pia raia wa Tanzania.

Kwa upande wa mshtakiwa David Kanayo Chukwu, ambaye ni raia wa Nigeria, kesi yake bado inaendelea katika mahakama hiyo baada ya kukana shtaka linalomkabili.

Upande wa Jamhuri katika shauri hilo uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali Elizabeth Muhangwa na Phoibe Magili.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, watuhumiwa hao walikamatwa tarehe 15 Aprili 2020, katika eneo la Mbezi, Kibanda cha Mkaa, na maafisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), wakidaiwa kusafirisha dawa za kulevya kiasi cha kilogramu 268.50 aina ya heroin.

Mahakama imeahirisha shauri hilo hadi tarehe 23 Februari, 2026, litakapopangwa kusikilizwa tena kwa ajili ya kuendelea na hatua za kisheria dhidi ya mshtakiwa aliyebaki
 
cc loose Nut, naona wagalatia mmeanza kuingilia dili kubwa bila koneksheni, ona sasa mnakamatwa kama kuku
Gunia mbili rumbesa za 130kg, duh, wangevushwa hao tungekoma mitaani na Vogue ya kutosha
 
cc loose Nut, naona wagalatia mmeanza kuingilia dili kubwa bila koneksheni, ona sasa mnakamatwa kama kuku
Gunia mbili rumbesa za 130kg, duh, wangevushwa hao tungekoma mitaani na Vogue ya kutosha
Hahahahahaaaaa huyo mbona wamekosea badala ya Issa wameandika Isso?
 

DEC nabs Tanzanian drug kingpin, seizes 1.4 tonnes of cannabis​

By Taonga Tembo,

View: https://m.youtube.com/shorts/xiasbmoaJW8
  • 4th February 2026
  • Drug Enforcement Commission director general Nason Banda making his remarks during a press briefing at the commission headquarters in Lusaka on Tuesday 3rd February 2026-Picture by Chongo Sampa
  • Local
  • Drug Enforcement Commission director general Nason Banda making his remarks during a press briefing at the commission headquarters in Lusaka on Tuesday 3rd February 2026-Picture by Chongo Sampa
THE Drug Enforcement Commission (DEC) has arrested a notorious Tanzanian drug trafficking kingpin of Lusaka’s Lilayi area, for being in possession of 1,380.8 kilogrammes of high-grade cannabis. Speaking to the media, Tuesday, DEC Director General Nason Banda identified the Tanzanian national as Ahmed Muharram, 40, who has been on the Commission’s watch list for a while. “The Drug Enforcement Commission (DEC), has recorded major successes in a series of intelligence-led controlled delivery operations conducted jointly between officers in Southern and Lusaka Province respectively, resulting in the arrest of several notorious drug traffickers and the seizure of large quantities of high-grade Cannabis and Benylin with Codeine. In one major operation, DEC officers, conducted a controlled delivery operation from Kazungula.
 
Drug Enforcement Commission director general Nason Banda making his remarks during a press briefing at the commission headquarters in Lusaka on Tuesday 3rd February 2026-Picture

03 February 2026
Lusaka, Zambia

DEC Yatibua Mipango ya Vigogo wa Makundi ya Madawa ya Kulevya | Bosi wa DEC aonesha madawa yaliyokamatwa​


View: https://m.youtube.com/watch?v=98Wrm2xeWeE
Tume ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya (DEC) Zambia, imefanya pigo kubwa kwa mitandao ya biashara ya dawa za kulevya kimataifa inayofanya kazi nchini Zambia.

Katika mfululizo wa operesheni zinazoongozwa na taarifa za kijasusi katika Mikoa ya Kusini na Lusaka, maafisa wa DEC walikamata zaidi ya tani moja ya bangi ya kiwango cha juu na kuwakamata washukiwa kadhaa waliohusishwa na vikundi vilivyojipanga vya mpakani.

Mkurugenzi Mkuu wa DEC Nason Banda anasema shughuli zilizoratibiwa zinaonyesha uwezo unaokua wa Zambia wa kuvuruga njia za kisasa za biashara ya dawa za kulevya na kulinda jamii kutokana na athari mbaya za dawa za kulevya.

Mapambano haya yanayoshirikisha njia za kiintelejensia na hatua madhubuti za utekelezaji wa sheria zinaweza kudhoofisha mitandao ya uhalifu ambayo inatishia usalama wa taifa na afya ya umma.

Katika video hii, tunaangazia yaliyotokea, mahali ambapo shughuli zilifanyika, na maana yake kwa mapambano ya Zambia dhidi ya uhalifu uliopangwa.
Source : Wilson Chishala.
 
Mzigo mzuri huo awagawie tu apotee kidogo.
Badae anarudi kivingine.
Kuna mburula Zambia huko wamemla kichwa na Bange kilo 1.3+ tu huku wengine hiyo ni dawa na mboga km matembele.😁👊
Wakili madele hapa hatakosekana kwenye kesi ya kimataifa.
 
03 February 2026
Mahakama Kuu ya Zanzibar
Tunguu
Zanzibar

REHEMA MWINYIMKUU ASHINDA KESI YA KILO 4 ZA HEROIN AKIWA HAYUPO MAHAKAMANI

Rehema Mwinyimkuu Mohamed aachiwa huru baada ya Mahakama Kuu ya Zanzibar kubaini kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kesi hiyo bila kuacha shaka yoyote, kama ambavyo inatakiwa kisheria katika mashauri ya jinai yanapoletwa mbele ya Mahakama kusikilizwa haki ipatikane .

Kesi hiyo oliendelea kusikilizwa huku mtuhumiwa akiwa ametoroka na hivyo kuwakilishwa mahakamani na wakili wake.

Mshitakiwa, Rehema Mwinyimkuu Mohamedi, anashtakiwa kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya kinyume na kifungu cha 21(1)(d) cha sheria namba 8 ya mwaka 2022? wa Sheria za Zanzibar. Inadaiwa kuwa Januari 31, 2022 majira ya saa 2:10 usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA), Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Mshtakiwa anadaiwa kuingiza Zanzibar kifurushi cha plastiki cha njano kikiwa kimefungwa Sellotape ya njano, kikiwa na kifurushi cheusi chenye unga aina ya mawe (kitofali) yaliyotambulika kuwa ni heroin yenye uzito wa kilo 4, kilicholetwa kutoka Addis Ababa, Ethiopia.

Ili kuthibitisha kesi dhidi ya mshtakiwa huyo, upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Suleiman Yusuf Ali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, aliita mashahidi watano na kutoa vielelezo viwili vya kuunga mkono kesi yake.
Inafaa kueleza kuwa mshtakiwa ambaye aliwakilishwa na Bw. Hassan Kijogoo, wakili msomi alitoroka wakati kesi ikiendelea. Kwa hiyo, kwa mujibu wa kifungu cha 260(1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sheria namba 7 ya mwaka 2018, Mahakama iliendelea kusikiliza kesi hiyo bila yeye na hivyo kupelekea kutolewa kwa hukumu hii.

Ushahidi wa upande wa mashtaka unathibitisha kuwa mnamo tarehe 31 Januari 2022 majira ya saa 2:50 usiku mshitakiwa alifika Terminal II ya Abeid Amani Karume.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (AAKIA) kutoka Afrika Kusini ndani ya Shirika la Ndege la Ethiopia....


IN THE HIGH COURT OF ZANZIBAR
AT TUNGUU
CRIMINAL CASE NO 114 OF 2022

DIRECTOR OF PUBLIC PROSECUTIONS

VS

REHEMA MWINYIMKUU MOHAMED

JUDGEMENT OF THE COURT
09/07/2026 & 03/02/2026
KAZI, J.:

The accused, Rehema Mwinyimkuu Mohamedi, stands charged with the offence of trafficking in narcotic drugs contrary to section 21(1)(d) of Act No. 8 of 2022? of the Laws of Zanzibar. It is alleged that on 31st January, 2022, at about 2:10 p.m., at Abeid Amani Karume International Airport (AAKIA), West B District, Urban West Region, Unguja, the accused
imported into Zanzibar a yellow plastic package wrapped with yellow Sellotape, enclosing a black packet containing powder in the form of stones identified as heroin weighing a total of 4 kilograms, which was brought from Addis Ababa, Ethiopia.

To prove the case against the accused, the prosecution, represented by Suleiman Yusuf Ali, learned Senior State Attorney, called five witnesses and tendered two exhibits in support of its case.
It is pertinent to state that the accused, who was represented by Mr. Hassan Kijogoo, learned advocate, absconded during the course of the trial. Consequently, in terms of section 260(1) of the Criminal Procedure
Act, No. 7 of 2018, the Court proceeded to hear the case in her absence, leading to the delivery of this judgment.

The prosecution's evidence establishes that on 31st January 2022 at about 2:50 p.m., the accused arrived at Terminal II of Abeid Amani Karume
International Airport (AAKIA) from South Africa aboard Ethiopian Airlines.

Page 1



Rashid (PW2), a police officer attached to the Anti-Narcotic Section of the Central Police, Zanzibar.
PW2 testified that he became suspicious of the accused as she appeared fearful and hesitant while queuing to exit the airport. Acting on this suspicion, PW2 called the accused aside and interrogated her. During the
interrogation, the accused disclosed her name and confirmed that she had
arrived from South Africa by Ethiopian Airlines. PW2, suspecting her of trafficking in narcotic drugs, decided to conduct a search of her luggage, including a rucksack bag.

PW2 escorted the accused to the arrival scanning area and requested the presence of Fatma Haji Kombo (PW4), an Airport Security Officer stationed at the arrival luggage scanning area, to witness the search. PW2 testified that upon searching the accused’s red bag (rucksack), which had
three compartments, he found male clothes in the middle section and female clothes and shoes in the main section. After removing all the clothes, he noticed a zip underneath the bag, beneath which there was a glued black cover. Upon detaching the cover, he discovered a large
packet surrounded by a brown liquid and wrapped with yellow Sellotape.

PW2 further testified that upon opening the packet, he found a powdery substance in particle form. He showed the contents of the packet to both the accused and PW4. Thereafter, he returned the items to the bag and
retained custody of it. Believing the substance to be narcotic drugs, PW2 placed the accused under arrest and informed her that she was being arrested for the offence of trafficking in narcotic drugs.
PW2 stated that he escorted the accused to the Airport Police Station, where he sealed the bag and marked it with the identification mark ANSZ/IR/14/2022.

On the same day, he handed over the exhibit to WP 12215 DC Rebecca (PW5), the storekeeper at the Anti-Narcotic Section of the Central Police, Zanzibar.

Subsequently, the accused and
the exhibit were taken to the Central Police office, where the case was registered under file number ANSZ/IR/14/2022

Page 2


SOMA Zaidi Hukumu / judgement
Source : Director of Public Prosecutions vs Rehema Mwinyimkuu Mohamed (Criminal Case 114 of 2022) [2026] TZZNZHC 7 (3 February 2026)
 
22 March 2026
Dar es Salaam, Tanzania

Mahakama ya Rufaa imebatilisha kifungo cha miaka 20 jela iliyotolewa kwa raia wa Marekani, Lionel Rayford na kuamuru aachiliwe huru mara moja

Lonie Lionel Rayford vs Republic (Criminal Appeal No. 501 of 2023) [2026] TZCA 277 (10 March 2026)


Mahakama ya Rufaa imebatilisha hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela aliyopewa raia wa Marekani, Lionel Rayford,

Mnamo Machi 10, 2026, Mahakama ya Rufaa nchini Tanzania ilibatilisha hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela kwa raia wa Marekani Lionel Rayford , akiamuru aachiliwe mara moja.

Uamuzi huo, uliotolewa na jopo la majaji—Augustine Mwarija, Panterine Kente, na Zainab Muruke—uligundua kuwa mahakama ya chini yaani Mahakama Kuu, Kitengo cha Makosa ya Biashara na Uchumi, haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Maelezo Muhimu ya Hukumu:
  • Kesi yafutwa: Mahakama ya Rufaa iligundua kuwa idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) iliyotumika kuanzisha mashtaka haikuelezea kifungu sahihi cha kisheria kinachodaiwa kukiukwa, jambo lililofanya kesi ya Mahakama Kuu kuwa batili.
  • Hatia ya Awali: Rayford alikamatwa Julai 4, 2018, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa madai ya kubeba kilo 2.188 za heroini. Alihukumiwa na kuhukumiwa Mei 26, 2023.
  • Matokeo: Mahakama ya Rufaa ilifuta hukumu hiyo, ikatengua hukumu hiyo, na ikakataa kuagiza kesi irudiwe, ingawa walibainisha kuwa DPP angeweza kumfungulia mashtaka tena.
Uamuzi huu unatumika kama mfano muhimu wa kufuata masharti ya kiutaratibu (hasa idhini halali ya DPP) katika mashtaka ya kiuchumi na uhalifu wa kupangwa nchini Tanzania.

Awali Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ilimuhukumu Lione Lionel Rayford raia wa Marekani kifungo cha miaka 20 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin kiasi cha kilo 2.188.

View: https://m.youtube.com/watch?v=39es9RIikOYHukumu hiyo ya Mahakama Kuu ya Tanzania ilitolewa tarehe 26 Mei, 2023 kufuatia Shauri la Uhujumu Uchumi kesi Namba 17 la mwaka 2021 lililokuwa mbele ya Mheshimwa Jaji Isaya kumalizika pasipo shaka kwamba, mshtakiwa alijihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Lione Lionel Rayford alikamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Julai 5, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa ameficha dawa hizo katika moja ya mabegi aliyokuwa nayo.

More info :

10 March 2026
HUKUMU YA MAHAKAMA YA RUFAA :
Lonie Lionel Rayford vs Republic (Criminal Appeal No. 501 of 2023) [2026] TZCA 277 (10 March 2026)

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…