Mtanzania aliyewahi kuwa Jambazi sugu Kenya atoa ushahidi na kusimulia alivyofanya jambazi ikiwemo kuvaa sare za polisi, Kayachoka maisha ya uraiani?

Mtanzania aliyewahi kuwa Jambazi sugu Kenya atoa ushahidi na kusimulia alivyofanya jambazi ikiwemo kuvaa sare za polisi, Kayachoka maisha ya uraiani?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Mzee anajisnichi mwenyewe, ni kama anajivunia kwa kazi haramu aliyowahi kuifanya

uyu mzee ni kama vile sio mzima kwakweli, ana jitoa ufaamu wazi wazi.

anaonyesha hadi id yake aliyotumia Kenya pamoja na chapisho la gazeti kwamba ni "wanted".

chanzo ni Millard, ni credible source so nahisi hawatakua kama Hawa wengine wa kibongo wanaotupotezea muda na mb kwa zile video wanazolipa watu wanakuja kuleta shuhuda za uongo na upuuzi ili wapate viewers!

Hapo kwenye wizi wa simu miaka ya 1999 watanzania tusiwe wabishi, kwa nchi kama Kenya simu zilishaanza kusambaa tangu miaka ya 1997, mitandao iliyovuma ni kencell, telkcom, safaricom, n.k.

 
Kama ni kweli basi Sheria zifate mkondo wake, huku kwetu tunachukulia vitu simple sana, Kuna story 'pendwa' hapa jf mtu anaelezea matukio aliyoyafanya akiwa jambazi, yaani anaelezea location mpaka anataja watu majina

Nikiwa nasoma nikawa nawaza ' I hope it's not true' maana kaweka details zote, kama ni kweli tukio Hilo lipo on record mtu unaweza shikwa na ukafungwa vizuri tu

YouTube Kuna akaunti inaitwa A&E Kuna clip za 'cold case files' yaani polisi Kule Wana kitengo Cha kufatilia kesi zote ambazo hazikupata ufumbuzi(cold cases) hata kama ikiwa imepita miaka 40 mauaji yaliyotokea na hakuna aliyeshikwa Kuna kitengo wanaendelea na investigation, watu wengi wameshikwa baada ya zaidi ya miaka 10 au 20 baada ya kufanya uhalifu

Kwa hiyo kama anajitangaza alifanya uhalifu naamini records zitakuwepo na Sheria ifate mkondo wake, hua nashangaa Sana mtu kujitokeza eti nilikua jambazi,tuliua mtu au watu ila sasa hivi nimebadilika sijui blah blah, vyombo vya usalama kamateni Hawa watu wahoji kama ni kweli wapewe stahiki zao, nothing goes unpunished!!

Millard ni credible source so nahisi hawatakua kama Hawa wajinga wengi wa kibongo wanaotupotezea muda na mb kwa content za kijinga maana hua wanalipa watu wanakuja kuleta confessions za uongo na upuuzi ili wapate viewers! Unakuta heading eti 'shemeji alinikuta nimelala akaniingizia nyuma' upumbavu mtupu
 
Waandishi wa habari za youtube hapa bongo ni kupoteza mda yeye kumpa viwer tu.

Eti jambazi sugu tena wazi wazi na sura
 
Waandishi wa habari za youtube hapa bongo ni kupoteza mda yeye kumpa viwer tu.

Eti jambazi sugu tena wazi wazi na sura
namnukuu mdau comment iliyopita

Millard ni credible source so nahisi hawatakua kama Hawa wajinga wengi wa kibongo wanaotupotezea muda na mb kwa content za kijinga maana hua wanalipa watu wanakuja kuleta confessions za uongo na upuuzi ila wapate viewers! Unakuta heading eti 'shemeji alinikuta nimelala akaniingizia nyuma' upumbavu mtupu

 
Kama ni kweli basi Sheria zifate mkondo wake, huku kwetu tunachukulia vitu simple sana, Kuna story 'pendwa' hapa jf mtu anaelezea matukio aliyoyafanya akiwa jambazi, yaani anaelezea location mpaka anataja watu majina..
Ni kweli hapa bongo ukibadilika huwa tuna roho za huruma, kwa wakenya hali inaweza kuwa tofauti wakaja kumchukua mzee.
 
Stori ya uongo hii. 1999 watu waliporwa simu zao? Hiyo 99 simu zilikuwepo ila kwa watu wachache mno kiasi kwamba utakuta mji mzima wenyewe simu hawafiki 10.
 
Stori ya uongo hii. 1999 watu waliporwa simu zao? Hiyo 99 simu zilikuwepo ila kwa watu wachache mno kiasi kwamba utakuta mji mzima wenyewe simu hawafiki 10.
Ni Kenya sio Tanzania, Kwa kenya simu za mkononi zimeanza kuwepo tangu 1995

Tanzania hapa tupo nyuma sana kwenye teknolojia, hata tv zilianza kuwepo majumbani kuanzia miaka ya 90 wakati kenya ni tangu zamani, Muda huu kenya nyumba kibao zina fibre internet lakini huku kwetu bado.
 
Mzee anajisnichi mwenyewe, ni kama anajivunia kwa kazi haramu aliyowahi kuifanya

uyu mzee ni kama vile sio mzima kwakweli, ana jitoa ufaamu wazi waz...
Hivi zile simu kubwa zenye mkonga za mtandao wa mobitel kwa Tanzania nakumbuka kama sikosei zilianza kutumika mwaka 1995, zilikuwa kubwa kama kipande cha sabuni ya mche!
 
Maisha yanabadilika na watu hufika mahali na huona haja ya kutoa ushuhuda wa maisha yao hata kama yalikuwa ya hovyo kiasi gani.
 
Back
Top Bottom