Mtanzania apata ajali Michigan, Mahututi..

Status
Not open for further replies.

Posted by Mwazange: Mgonjwa tayari ameshatutoka?????


Unanambia mimi Kifimbocheza huku unaposti crippity crap kama hiyo ! Huwezi kusema kitu kama hicho mtu bado yuko Hospitali.

Nilishakufahamisha before kuwa hii sio nyuzi ya ligi...bado unatafuta point tu mkuu? tafuta nyuzi nyingine tukabishanie huko pindi hii ikikaa sawa...you will pick a topic then its going to be on...right my friend????

Kukujibu hako kahoja kako...ungenukuu post nzima nzima jinsi nilivyoandika.....niliomba maelezo zaidi mwishoni. Mbona hiyo hukuinukuu? Au haikuendana na mwelekeo wa hoja yako...(ya kuleta ubishi)?
 
Mgonjwa tayari ameshatutoka????? Hebu tupeni updates waheshimiwa........
Huyo JK na serikali yake achaneni naye kwanza...Tumfuatilieni mwenzetu.

Manzage, please lets keep praying.Dont anticipate....
 
Manzage, please lets keep praying.Dont anticipate....
That's what I've been trying to do.....Lets keep our hopes and prayers to almighty God......
Mwenzetu apone then tutarudi kwenye ligi za ubishi wetu.
Thanks for getting it.
 
Wana-JF,


Kwa masikitiko makubwa Familia ya Mohamed Nzaro na Balozi Eva Nzaro inatangaza kifo cha mtoto wao Ndalima Yusuph Nzaro kilichotokea siku ya Alhamisi Katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Michigan mjini Ann Arbor ambapo alikuwa amekimbizwa kutibiwa baada ya ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia Jumanne ya Oktoba 14, 2008.

Gari alilokuwa akiendesha marehemu liligongwa na gari nyingine wakati likisubiri taa za kuongozea magari.

Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania kwa mazishi inaendelea. Vile vile, utoaji wa heshima za mwisho mjini Detroit unatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 18 Oktoba, 2008. Muda rasmi utatangazwa baada ya maandalizi kukamilika.

Familia inapenda kutumia nafasi hii kuwashukuru na kuwaomba msaada wenu wa hali na mali katika kufanikisha safari hii ya mwisho ya kijana wao mpendwa Ndalima.

Michango kwa ajili ya msiba huu inaweza kupelekwa moja kwa moja kwenya akaunti maalum ifuatayo:

Bank Of America:

A/C Name: Philemon Mnzava ( jumatatu unaeza ukaongeza jina la Mboja Nzaro)
Routing No. 072000805
A/C No. 5407722411
Bank Location: Michigan


Swift Code: BOFAUS3N

Mawasiliano zaidi Kuhusu habari za msiba huu wasiliana na wafuatao:

Anna Royal Mfinanga 248-778- 6395
Abdul Kufakunoga 248-515- 5509
Salum Ndolanga 248-796-1267
Philemon Mnzava 248-417-5015
Leo The Saint 614-426-3422


Msiba huu kwa Detroit unafanyika nyumbani kwa binamu yake Ayubu Mfinanga.
Anuani ya Kwa Ayub:

22255 Hessel
Detroit, MI 48219


Tutaendelea kuwahabarisha kwa kadiri mipango inavyoendelea.

Asanteni kwa sala zenu, ushirikiano wenu na misaada yenu.


FAMILIA YA NZARO
 

Poleni sana bwana aliumba bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!!
 
ooh NO! Rest in peace brother......Tangulia na sisi twaja.
 
Mola amlaze mahala pema.....Poleni sana ndugu wafiwa....
 
Naungana na Familia yote ya Balozi Nzaro na wana JF wote.
POLENI SANA!.
 
Mwenyezi Mungu, Muumba wetu, Muumba wa Mbingu na Nchi ambaye alimpenda zaidi ndugu yetu na Mpendwa wetu Ndalima Nzaro zaidi yetu, hatimaye amemrudisha kwake.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen.

Poleni sana wanafamilia na wote waliokuwa karibu naye.

Mwenzetu ametangulia, nasi tu nyuma yake.
 
Samahani kuuliza.Hivi marehemu alikuwa na mahusiano na ukoo wa Balozi Eva Nzaro?
 
Marehemu Ndalima Nzaro apumzike kwa amani.

Wafiwa poleni sana.
 
May God Rest His Soul In Eternal Peace.

The whole Nzaro Family we are with U.
 
Ahsante sana kwa juhudi zako za kutupa taarifa kuhusu Mtanzania mwenzetu toka alipopata ajali mpaka anafariki. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN.
 
Ahsante sana kwa juhudi zako za kutupa taarifa kuhusu Mtanzania mwenzetu toka alipopata ajali mpaka anafariki. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN.

Thanks to you too bro.
Its in times like these that we pull together as one.
 
Mwenyezi Mungu amuweke Ndali mahali pema peponi, pia awape nguvu na faraja familia nzima ya Nzaro katika hichi kipindi kigumu....
 
Thanks to you too bro.
Its in times like these that we pull together as one.

Ab-Tichaz,

Pole na wewe pia. Je ulikuwa una ukaribu na Marehemu Ndalima?

Unaweza kunambia mawili matatu kuhusu Marehemu, the person, ambayo naweza kujifunza kwayo?
 
Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Ndalima Nzaro Mahala Pema Peponi.
 
Ab-Tichaz,

Pole na wewe pia. Je ulikuwa una ukaribu na Marehemu Ndalima?

Unaweza kunambia mawili matatu kuhusu Marehemu, the person, ambayo naweza kujifunza kwayo?

Kuhani,

Kwa ukweli marehemu alikua mshkaji wa kila mtu na hata siku moja
sikumuona akigomba wala nini.He was a very close friend of mine and
we used to discuss everything from politics to religion frequently.I
remember when he used to come to my house for a drink and we would
have a brotherhood like
no other.

Amongs his positive attributes was the fact that he was very down to earth
wala usingejua kama Mamake alikua balozi wala nini.He kept it simple.He was
also a reliable individual na nakumbuka pia alikuwepo kwenye msafara wa
harusi yangu some 7yrs ago.He never failed me when he made a promise and
he always had a smile on his face regardless of the circumstances...that
calming effect we would call it.

I believe kila mtu mitaa ya hapa kwetu anajambo positive la kusema kumhusu
Ndalima and they will share it as time goes by.Salum,Kaiza na Kevin were his
work buddies na najua they have nothing but glowing tribute for the brother.

He lives behind a son and a fiance.
God bless.

PS: I will be posting his picture later nikishatoka kazini maana hapa comp ziko
limited in terms of what I can do.
 

Mkuu Ab-titchaz,

Ubarikiwe kwa habari hizi, haya wananchi sasa tutume hela za kusaidia ndugu zetu wa hii familia ili wausafirishe mwili wa marehemu, hapa kila neno liko wazi kilichobaki ni kutuma tu,

Mungu amuweke pema marehemu!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…