Mambo Jambo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2008
- 1,100
- 82
Ningeshauri mtu mwenye picture ya late Ndalima Nzaro aiweke hapa ili na wasio mfahamu kwa sura wapate nafasi.
R.I.P Ndalima
R.I.P Ndalima
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ningeshauri mtu mwenye picture ya late Ndalima Nzaro aiweke hapa ili na wasio mfahamu kwa sura wapate nafasi.
R.I.P Ndalima
Ab-Titchaz,
Wakati tunaendelea kuombeleza ni vizuri pia mkashauriana na familia ya Marehemu kungalia uwezekano wa kuwachukulia hatua za kisheria Polisi waliohusika na hiyo high speed chase.
Katika hali ya kawaida na kulingana na kosa la huyo 15 years ( tunaambiwa aliwaonyesha ishara ya kidole cha kati polisi) halikuhitaji mafukazano yale hususan ktk dunia ya leo ya teknolojia wangeweza ku mtrack na kumpata kirahisi bila ya kusababisha madhara kwa public.
Hapa UK trafick offense ndogo kama hizo polisi huwa wana abandon chase na hasa mtuhumiwa akiwa anaelekea maeneo ya watu wengi, unless awe jambazi ambalo halitakiwi kuwa on the loose hata dakika moja.
Naamini polisi hapo wame act irresponsible na wana big share of blame. Something should be taken against them.
Naomba kutoa hoja
Ningeshauri mtu mwenye picture ya late Ndalima Nzaro aiweke hapa ili na wasio mfahamu kwa sura wapate nafasi.
R.I.P Ndalima
May all beings attain enlightenment.
A life senselessly and cruelly robbed.
Titchaz
Pole, majonzi na simanzi si kwako pekee. Anapofariki jamaa hukumbusha misiba mingi sana, ndio maana tunalia tunaposikia mtu katutoka hata kama hatumjui. Inaumiza sana kuondokewa na jamaa ghafla namna hii, few days back alikuwa na mzima mkicheka na kuongea, na imegeuka kuwa impossible...never again. Its so painful. Pole sana na wakati unaomboleleza jua huko peke yako.
Thank you so much for your kind words.
Natanguliza rambirambi kwa familia,ndugu na marafiki wa Ndalima, Mungu ailaze roho ya marehemu peponi. Ameen. Watanzania sote tulio nje tunakuwa wamoja hasa linapotokea jambo la kushikamana kama hili la msiba, kwani kifo hakitabiriki. Ombi kwa mkuu Ab-Titchaz na Mkjj ningeshauri kama inawezekana mkatupatia kiungo kwa mtu aliyeko hapa UK ili sisi tulio hapa tuwasilishe michango yetu? it is more convenient and quicker for those of us who are on this side. Ahsante.
I saw the snap, he was young and promising.....je ameacha mke au/na wa/mtoto? samahani kama naenda nje ya maudhui ya thread.
ndiyo ameacha mtoto mmoja wa kiume na mwenzi wake.
Kwa wana JF, Ndali alikuwa ni mmoja wetu hapa na mara nyingi tukikutana tunaendelea mazungumzo yetu ya JF nje ya hapa. So, siyo tu kwamba familia imempoteza bali pia familia ya JF imempoteza.
Wana-JF,
![]()
Kwa masikitiko makubwa Familia ya Mohamed Nzaro na Balozi Eva Nzaro inatangaza kifo cha mtoto wao Ndalima Yusuph Nzaro kilichotokea siku ya Alhamisi Katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Michigan mjini Ann Arbor ambapo alikuwa amekimbizwa kutibiwa baada ya ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia Jumanne ya Oktoba 14, 2008.
Gari alilokuwa akiendesha marehemu liligongwa na gari nyingine wakati likisubiri taa za kuongozea magari.
Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania kwa mazishi inaendelea. Vile vile, utoaji wa heshima za mwisho mjini Detroit unatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 18 Oktoba, 2008. Muda rasmi utatangazwa baada ya maandalizi kukamilika.
Familia inapenda kutumia nafasi hii kuwashukuru na kuwaomba msaada wenu wa hali na mali katika kufanikisha safari hii ya mwisho ya kijana wao mpendwa Ndalima.
Michango kwa ajili ya msiba huu inaweza kupelekwa moja kwa moja kwenya akaunti maalum ifuatayo:
Bank Of America:
A/C Name: Mboja Nzaro (Dada wa Marehemu)
Routing No. 072000805
A/C No. 5407722411
Mawasiliano zaidi Kuhusu habari za msiba huu wasiliana na wafuatao:
Anna Royal Mfinanga 248-778- 6395
Abdul Kufakunoga 248-515- 5509
Salum Ndolanga 248-796-1267
Philemon Mnzava 248-417-5015
Leo The Saint 614-426-3422
Msiba huu kwa Detroit unafanyika nyumbani kwa binamu yake Ayubu Mfinanga.
Anuani ya Kwa Ayub:
22255 Hessel
Detroit, MI 48219
Tutaendelea kuwahabarisha kwa kadiri mipango inavyoendelea.
Asanteni kwa sala zenu, ushirikiano wenu na misaada yenu.
![]()
FAMILIA YA NZARO